Foul
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 796
- 1,160
Nilikuwa natafuta comment kama hii, wajinga wanataka Wakulima wawe maskin ili wao wanunue chakula bei chee, utadhan wao wamepigwa matufuku kulimaKumbuka kwamba kama wewe unavyofanya biashara upate faida, kilimo nacho ni biashara. Elewa kwamba sasa ni fursa ya mkulima kupata faida.
Zingatia mkulima siyo punda wa taifa. Kama unaona vipi acha kupiga soga hapo mjini nenda kajilimie chakula chako.
Kwani hawayaoni mashamba? Nimekuwa nikiwaambia wajinga hivi, wanachojibu eti sina wa kunitegemea, nawacheka sana, wao wanafanyabiashara na wanataka faida, tena wanauza mpaka bidhaa fake ili wapate faida kubwa, lakin wanataka Mkulima auze bei ya chini
Serikali ina ya kufanya kupunguza bei ya chakula, lakin si kufunga mipaka
Mnajua kazi ya Maghala ya taifa? Basi serikali iyatumie hayo, ndio maana Serikal lazima ilaumiwe kwa vyakula kupanda bei, na dawa ya Serikali kutolaumiwa si kufunga mipaka, bali yenyewe inunue hicho chakula kinachoenda nje, kwa bei ile ile wanayonunulia hao wanaopeleka nje au bora zaidi, alafu wafanye kitu kinaitwa Market flood, zile sehemu ambazo chakula kimepanda sana, wapeleke mzigo sokoni, supply iwe kubwa kuliko demand, bei ishuke