Wanaouza mazao wakati huu wala mkulima hahusiki kabisa tena ni mapesa toka nje yaliyoingia kununua mazao na kuweka stock mazao kwa mfano kijiji cha gwarama kule kakonko.
Wanyarwanda wamejenga magodown kupitia wafanyabiashara wa pale na kila mwaka huweka tani nyingi mno za mazao wakati kama huu husafirisha, haya pale nyakanazi kuna tajiri wa burundi anaitwa kamangaza ana magodown pale kupitia wazawa na hununua mahindi mengi sana na mtama, na huanza kusafirisha kwenye uadimu hali kadhalika.
Wafanyabiashara wakenya huingiza pesa nyingi sana kule chunya na songea nakuweka store tani nyingi sana za mazao, kwahiyo tunaposema mfunge mipaka tunamaana mnufaika kwa sasa sio mkulima kama mnavojidanganya, mavuno yangekua mengi ni sawa lakini mnakaza vichwa huko serikalini wakati hamna hata taarifa za kutosha.