Uchaguzi 2020 Serikali ya Marekani yaonya "Vitisho na mabavu dhidi ya upinzani si dalili nzuri ya Uchaguzi Huru Tanzania Oktoba 2020"

Jumuia za kimataifa zinatakiwa kuziingilia nchi zote zenye Utawala wa kikomunisti na kidikteta na kuwafurusha watawala waliokosa malezi Bora utotoni ambayo yanapelekea uvunjifu wa amani na kuipa dunia gharama kubwa Sana za kuhudumia wakimbizi ili kuokoa pesa hizo zikatumike kwenye project zingine duniani, watawala wa kiafrica wanachojua ni kuzalisha wakimbizi duniani na sio kuhudumia wakimbizi wanaachiwa mzigo wengine.
Hawa watu waliokosa malezi Bora utotoni ndio uisumbua dunia.
 
sasa hivi vyombo vya habari vimepigwa kofuli.

bunge live lilifungwa na wabunge wa upinzani kila kukicha kufukuzwa bungeni, kupigwa hadi kuvunjwa viungo nk.

Kodi za wananchi kutumika kununua wapinzani mfano arumeru, ushahidi ukatupwa na wanunuzi wakapandishwa vyeo.

mtu mmoja anaamua mipango yote ya serikali ikiwemo bajeti ambazo zinatakiwa zipangwe na kuamuliwa bungeni.

watu wanateuliwa na kutenguliwa hovyo bila kufuata sheria na taratibu zilizowekwe.

watu wapo magerezani miaka na miaka hawafikishwi mahakaman ili wajitetee na kama wana makosa waHukumiwe kwa mujibu wa sheria....madhila ni mengi mkuu....yaan uchochozi ni wapinzani, risasi wapigwe upinzani, ofisi zichomwe za upinzani, mikutano ya kisiasa wazuiliwe kufanya wapinzani, mali ziharibiwe ni za wapinzani mfano mali za mbowe.. nyumba zibomolwe ni za wapinzani, tume huru hakuna, maonevu ya jeshi la polisi ni kwa wapinzani...yan yote hayo hakuna hata moja anafanyiwa ccm ni upinzani tu....dah!! Mkuu acha USA, the hegi na dunia watusaidie tu sababu hatuna namna..kodi zetu wenyewe zinatumika kutuminya kila
kona tufanyeje sasa? hivi unafikiri wanaojilipuaga kule mashariki ya kati wanapenda sana kufa? Mkuu paka mkimbize atakimbia lakini akifika kwenye kuta nne hana pa kwenda tena ndo utauona mziki wake
 
Kama mtu anaendesha gari kwenye barabara nzuri ya Lami, hawezi kusimama ghafla barabarani na kuanza kushangaa kwa nini Tairi za gari lake yanazunguka vizuri; akifanya namna hiyo, kila mtu atamshangaa kwani ataleta foleni kwenye barabara au watu watasimama ili kumsaidia;LAKINI kama atasimama kwa sababu TAIRI LIMEPATA PANCHA au limepasuka, kila mwenye NIA njema ataguswa kutoa mchango wake ama kuziba pancha, au kumpatia tairi la spea; Sasa hivi tupo kwenye Uchaguzi ni lazima tuangalie,Je Gari/tairi letu lina pancha au linatembea vizuri bila matatizo? Kama mtu atakuwa kwenye shida au atakuwa anakwenda kutumbukia kwenye shimo ni lazima Jumuiya zote za Kimataifa kutusaidia kuepukana na hujuma za maadui ama wa Ndani au wa Nje? Sisi Tanzania tunao akili timamu na tunapaswa kujiangalia wenyewe bila kuingiliwa na watu wasiojua mila na desturi zetu; Tupo Imara na tunaijua Nchi yetu vizuri isipokuwa kama tairi/gari limepata pancha;tunapaswa kuziba pancha na kuendelea na safari; tusiwakaribishe watu kutushangaa kwa kuangalia gari /tairi letu kuwa halina pancha ila tunalishangaa
 
Ila hawasemi,
Afrika inasumbuliwa na utumwa wa fikra, wafuasi wa upinzani wanafurahia kuona tunaingiliwa Mambo ambayo inapaswa tujisimamie wenyewe
acha tuingiliwe bana, miafrika ndivyo tulivyo hatujitambui bila kulazimiswa. yan wananchi tuonewe halafu tukae tu kimya ina maana mnataka mpaka mtunyee mdomoni au?
ni kweli tunasumbuliwa na utumwa wa fikra maana tumejaa ubinafsi, roho mbaya kati yetu, hatupendi uhuru wala demokrasia..ni wapenda giza giza tu. acha watuingilie maana tunashindwa kujitawala wenyewe.
 
Sasa mbona mkuu unakuwa hueleweki unavamia tu kila hoja bila utaratibu.
Hapo nimekuuliza maswali umejibu lipi ? Naona unarudia yale yale niliyokwisha kukujibu.
Haya mkuu mimi naishia hapa we wasubiri USA waje wakuletee democrasia.
 
ni mchakato!
Kwa mtu wa kawaida mwenye uelewa wa kujadili JF, unawezaje kuamini kwamba kuna mtu anaitwa Lissu ni maarufu na ana uwezo kuliko wewe? Huoni hiyo ni kasoro kichwani mwako.

Binadamu, kimaumbile ana tabia ya kujiamini kabla ya kuamini mtu mwingine. Leo hii unaamini Lissu atakukomboa baada ya kushitaki US? bora uishi zizini na nguruwe tu!
 
kabisa. tupaze sauti hadi watusikie waje kutusaidia..tumeonewa vya kutosha.
 
Sasa mbona mkuu unakuwa hueleweki unavamia tu kila hoja bila utaratibu.
Hapo nimekuuliza maswali umejibu lipi ? Naona unarudia yale yale niliyokwisha kukujibu.
Haya mkuu mimi naishia hapa we wasubiri USA waje wakuletee democrasia.
kwani wakituletea demokrasia ni vibaya mkuu? kwa hiyo mkuu wewe hutaki demokrasia?
 
Ila hawasemi,
Afrika inasumbuliwa na utumwa wa fikra, wafuasi wa upinzani wanafurahia kuona tunaingiliwa Mambo ambayo inapaswa tujisimamie wenyewe
Si uliona wakijikusanya ubalozi wa EU eti wanashitaki juu ya uchaguzi? Ni aibu kuwa na watu wa aina hii ktk siasa.

Kila anayejitambua akiingia ktk vyama hivi anatoka. Leo hii hatuwasikii akina Baregu, Safari, wote wamewaachia upuuzi wao. Ni vigumu kumshauri mtu aliyekulia maisha ya 'misheni tauni'. Hata ndani ya familia hatuwezi!
 
ndiyo demokrasia Mkuu, mtu anakusanyika anapoona patamfaa mradi havunji sheria na haingilia uhuru wa mtu mwingine kinyume cha sheria. wewe ni nani hadi upangie wenzako pakukusanyika? wewe hujakusanyika huko EU na hakuna anayekuuliza sasa wewe wanaokusanyika wanakuwashia nini? kwan nchi ni ya kwako peke yako mkuu?!!!
 
Tendeni haki kwa kukamata walio muuwa mawazo, Ben Saanane, waliompiga Lissu risasi, walionvunja Mbowe miguu, waliomvuja Ester Bulaya mikono, waliomvunja halima Mdee mikono, waliochoma ofisi za Chadema Arusha na Lindi. Baada ya hapo waambie USA kuwa tuna usawa na amani
 
nikiishi zizi la nguruwe nitanenepa kwa kula kitimoto daily, so poa poa tu..

kama kawaida yenu, MATAGA mlichobaki nacho sasa baada ya Lissu kuwashika kunako ni matusi tu... hoja kwishnei!
 
Wakuache uwe unawabambikia kesi unawapiga risasi unawapora ushindi wakurugenziccm kufocha form kama kule ubungo?
 
Wewe ndiyo ulitumwa kwenda kumpiga risasi? Mtu ana uchungu wa mabaya mliomtendea mnadai anamdharau Rais? Lisu hamdharau Rais bali husema mapungufu yake kwa uwazi ndipo nyinyi wanafaika wa mfumo kandamizi mnaenda kumchochea awahujumu chadema muendelee kutafuna pesa za kutokomeza upinzani Tanzania
 
Hugo Chavez alikuwa anawaletea dharau nadhani unajua kilichomkuta,endeleeni kuleta nyodo zenu
 
Waambie USA wamkamate Bush kwanza wampeleke the Hague. Acheni kuwa mandondocha wa nashoga.
Waanze kuwakamata waonevu wanawabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani kwanza ndipo waende huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…