Serikali ya Rais Samia imeleta tabasamu na matumaini katika kila Sekta

Serikali ya Rais Samia imeleta tabasamu na matumaini katika kila Sekta

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu, Mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni, Serikali ya Rais Samia imeleta Tabasamu na matumaini katika kila secta, Leo hii ukiangalia na kufuatilia kila secta utagundua na kuona kuwa Rais Samia amefanya uwekezaji na mapinduzi makubwa katika kila secta inayogusa maisha ya mtanzania, kila eneo utakuta mkono wa Rais Samia, kila mahali utakuta maagizo ya Rais Samia, kila eneo utakuta kazi ikiendelea kwa Kasi ,kila Kona utakuta Alama za Rais Samia, Hakuna utakapokwenda ukakuta kumesahaulika na serikali ya Rais wetu, Hakuna utakapokwenda ukakuta hakuna uwekezaji wa Kodi za mtanzania, Ni kazi kila mahali, Ni uwekezaji kila Kona na matumaini kila eneo.

Ukienda katika Elimu unakuta Ni Tabasamu na matumaini makubwa kwa watoto wanaotoka familia za kipato Cha chini Kuendelea mbele kielimu na kimasomo baada ya Rais huyu shupavu, Jasiri, imara, Hodari na mzalendo wa Dhati kuamua kuifanya Elimu kuwa bure Hadi kidato Cha sita,Utakuta wanafunzi wa vyuo vikuu wakiwa na Tabasamu baada ya kupatiwa mikopo kwa wakati kwa wote waliokidhi vigezo.

Wazazi wenye kipato Cha chini hawana wasiwasi juu ya watoto wao kutimiza Ndoto zao maana wanajuwa habari njema iliyoletwa na jemedari wetu Rais Samia kwa kuamua kuwa kila mtoto bila kujari familia aliyotokea anapata haki ya Elimu bila kikwazo au kizuizi.

Ukienda katika kilimo unawakuta wakulima wakiwa na Furaha na kumshukuru Rais wao Mama wa shoka Rais Samia kwa kuwapatia mbolea za Ruzuku kwa kutoa mabillioni ya pesa za kitanzania Takribani billioni Mia moja hamsini huku bajeti ya Wizara ikiongezeka Mara dufu katika historia ya nchi yetu na kufikia billioni Mia Tisa na point,Sasa wakulima ni Tabasamu na matumaini makubwa mioyoni mwao ya kuongeza na kufanya kilimo Chao bila kikwazo baada ya kupatiwa unafuu wa Bei ya mbolea, lakini pia Wana uhakika wa soko la mazao yao baada ya Rais wetu mpendwa kuimarisha Diplomasia yetu ya uchumi na kuifungua nchi yetu kiuwekezaji na kibiashara, Sasa wakulima wanafaidika na jasho lao baada ya kuwa juani na kwenye mvua wakati wote wa kilimo, utawaambia Nini wakulima juu ya mama yao Rais Samia wakuelewe?

Hakika kama unataka ugomvi na wakulima jaribu umseme vibaya Rais Samia utakiona Cha mtema kuni.

Ukienda katika secta binafsi ni mafanikio matupu kwani kwa Sasa secta hii imeimarika vizuri na kukua vyema na kutoa fursa za ajira kwa vijana, Husikii habari za kufungwa kwa biashara za watu ,au kupunguza wafanyakazi au muwekezaji kuondoka nchini, kwa Sasa unasikia uwekezaji katika kila nyanja, ujio wa wawekezaji wakubwa na masuala mengine Kama hayo.

Ukija katika Afya nako Ni Matumaini na mafanikio matupu, vituo vingi vya Afya vimejengwa kila Kona ya nchi yetu,kila sehemu huduma za Afya zimesogezwa karibu ya mwananchi, upatikanaji wa Dawa, vifaa Tiba ni wa uhakika bila kusahau uwepo wa wataalamu na wahudumu mudaa wote. Hivi majuzi tu vimejengwa vituo vya Afya takribani 234 nchini vilivyotokana na Tozo zetu chini ya usimamaizi madhubuti wa Rais Samia na serikali yake.

Hayo ni kwa uchache Kati ya mengi ni wapi utakwenda usikute kazi ya kutukuka ya Rais Samia? Ni wapi Rais Samia na serikali yake hajapeleka fedha?

Ni Nani na kwa namna gani hajaguswa na juhudi na utumishi wa kutukuka wa Rais Samia? Ni Nani hajafikiwa na huduma?

Ni Nani hajaona juhudi za Rais Samia katika kuijenga nchi yetu? Ni Nani Haoni namna Rais Samia anavyofanya kazi bila kupumzika?

Ni Nani asiyeona upendo wa dhati na mkubwa alionao Rais Samia kwa Taifa letu?

Mnataka Rais wetu mpendwa afanye Nini kwetu ili Turidhike? Mnataka atuletee Nini ili Tushukuru kwa uwajibikaji wake uliotukuka? Kwanini Tusimpongeze ndugu zangu? Hamjuwi hata yeye Ni mwanadamu? Hamjuwi hata yeye ana moyo wa nyama? Nawaombeni watanzania wenzangu Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia na Tuwe na Subira tupitiapo changamoto fulani Kama Taifa.

Kazi Iendeleee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
 
Tabasamu kwa wazanzibari na mafisadi tu
Tuna imani na Rais wetu na tunaamini Hakuna fisadi atakaye salimika na kubaki salama akibainika kugusa fedha za umma,pia Tambua kuwa sisi wote Ni watanzania acha habari zako za uzanzibar
 
Tuna imani na Rais wetu na tunaamini Hakuna fisadi atakaye salimika na kubaki salama akibainika kugusa fedha za umma,pia Tambua kuwa sisi wote Ni watanzania acha habari zako za uzanzibar
Mbona amezungukwa na mafisadi na ndio washauri wake wakuu
 
Unakuta ni muhitimu wa Chuo kikuu.

Mjinga mjinga Fulani, ambaye kusoma kwake kote aliamini kuajiriwa .

Mambo yakawa sivyo.

Baba yake akamwambia, Mwanangu, Ingia CCM, sifia tuu, utapata uteuzi.

Mavijana kama wewe ni boga kabisaa .

HIVI WEWE KIAZI, BADALA YA KUA UNAANDIKA MAANDIKO AMA YAKUSHAURI,AU KUCHALLENGE WATU WAJIREKEBISHE, AU BASI WAANDIKIE WATAWALA NAMNA FAN YA KUMFANYA MTANZANIA AJIKWAMUE .

wewe kwakua baba yako kakuambia sifia, basi ni kusifia tuu

Hapo akili yako inakutuma " hata nikioewa 'UDED' poa tuu .

Siuwambie wakuteue tu, ili uanze kupiga matarumbeta.
 
Wapi nilipozungumzia habari za uteuzi
 
Tatizo la vijana wa kitanzania hamtaki mtu aandike ukweli kuusu serikali kama Serikali inafanya mambo mazuri acha watuwaseme wakifanya mambo mabaya tutasema pia
 
Kabla mbolea Magufuli aliacha mfuko wa DAP tsh. 60 mpaka 65 elfu.
Alipoingia huyo mbolea ikapaa mpaka laki 1.3.
Baada ya ruzuku mfuko huo unaupata kwa 70 elfu.
Sasa unacho sifia ni nn??
Hiyo elimu unayoisema sijui bure mara uhakika wa mkopo, total ni kaburi baada ya kuzalisha wasomi uliiwafundisha kuajiriwa na kuwapotezea muda bure.

Issue ya vituo labda useme anamalizia alivyoanzisha mzee Magu ila sio yeye ajenge vipya sijakiona hata 1.
Zaidi deni limekua na pesa inaingia mifuko ya akina Mwigulu na ukoo wa Makamba.
 
Kwenye siasa upinzani wamekiri katika marais wote waliopita Rais Samia Suluhu ameonyesha nia ya dhati ya kufanya mazungumzo na kupata mariadhiano ya kitaifa
 
Back
Top Bottom