Serikali yaagiza Mtoto Charles Mathias arushwe Darasa kutoka Chekechea hadi Primary, Babu Tale aahidi kumlipia ada

Serikali mkoani Morogoro imeagiza mtoto Charles Mathias mwenye umri wa miaka 6 arushwe darasa kutoka Chekechea hadi darasa la kwanza baada ya kuonyesha kipaji kikubwa kwenye somo la Hisabati.

Afisa tawala wa mkoa bwana Kobehelo amesema agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja.

Naye mbunge wa jimbo la Morogoro kusini mashariki Hamis Taletale ameahidi kugharamia elimu ya mtoto huyo hapo kijijini.

Source: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
KAMA MH MB
AJUI ADA N BURE AMENITISHA SANA ATAKAVYOTETEA WANANCHI DODOMA
 
Akiandikiwa hizo hesabu anaweza kuzitolea majibu? Au anajua kuziongea tu
 
Hapo ajaruka kuruka angetoka chekechea hadi la 2 na kuendelea ikiwa na maana karushwa drs la kwanza sasa kutoka chekechea kwenda la kwanza karuka darasa gani najaribu kuwaza.
Usitafakari sana haya mambo, uyapokee tu na upige makofi kwa nguvu! 😂
Umri wa kuingia darasa la kwanza ni miaka 6, sasa tujiulize kwanini alikuwa mtoto anapelekwa chekechea??

Everyday is Saturday................................😎
 
No background info,umeandika kama vile kila mtu anamjua huyo mtoto
 
Hapo ajaruka kuruka angetoka chekechea hadi la 2 na kuendelea ikiwa na maana karushwa drs la kwanza sasa kutoka chekechea kwenda la kwanza karuka darasa gani najaribu kuwaza.
Usanii wa viongozi wa ccm kutafuta kiki
 
Serikali mkoani Morogoro imeagiza mtoto Charles Mathias mwenye umri wa miaka 6 arushwe darasa kutoka Chekechea hadi darasa la kwanza baada ya kuonyesha kipaji kikubwa kwenye somo la Hisabati.

Afisa tawala wa mkoa bwana Kobehelo amesema agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja.

Naye mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale ameahidi kugharamia elimu ya mtoto huyo hapo kijijini.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Kwani elimu si ni bure?sasa anamlipia nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ajaruka kuruka angetoka chekechea hadi la 2 na kuendelea ikiwa na maana karushwa drs la kwanza sasa kutoka chekechea kwenda la kwanza karuka darasa gani najaribu kuwaza.
Mimi mtoto wangu wa kwanza kaanza darasa la kwanza akiwa na miaka mitano.

Hawa watu ni matapeli watupu, usiwachukulie serious.
 
Serikali mkoani Morogoro imeagiza mtoto Charles Mathias mwenye umri wa miaka 6 arushwe darasa kutoka Chekechea hadi darasa la kwanza baada ya kuonyesha kipaji kikubwa kwenye somo la Hisabati.

Afisa tawala wa mkoa bwana Kobehelo amesema agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja.

Naye mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale ameahidi kugharamia elimu ya mtoto huyo hapo kijijini.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Kitu chochote ambacho kinaenda vizuri, ccm wakishajichomeka tu, lazima pavurugike.
 
Sasa hii ndio habari ya kuleta hapa, wakati kuna watu tuliishia darasa la 5 tukafanya paper ya std 7 na tukachaguliwa shule za vipajai maalum.
Umenikumbusha mbali mkuu niliwahi kutana na mwanafunzi wa hivi Tabora boys school aliishia la nne kafanya mtihani wa wilaya kama jaribio akawaongozea na wakamua kumsajili kufanya mtihani darasa la saba na akatoboa na kuletwa Tabora boys japo alikutana na wehu waliokubuhu ila form 4 aligonga one 9 tu
 
Anstahili kuanza la 3. Anafanya pepa ya la nne. Kisha arushwe la 6.
 
Back
Top Bottom