Serikali yampa ajira Mwanamke anayekumbatia Watoto njiti hospitali ya Amana

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imempa ajira ya mkataba Mariam Mwakabungu (25) kama sehemu ya kuthamini mchango wake kwa kujitolea kuokoa maisha ya Watoto wachanga (Njiti) waliokimbiwa na Mama zao katika Hospitali ya Amana ambapo amekuwa akiwakumbatia ili wapate joto na kuongeza uzito.

Waziri Ummy amesema Rais Samia amefurahishwa sana na upendo wa Mariam na licha ya kumpa milioni 2 jana ameridhia Serikali impe Mariam ajira ya mkataba, kwakuwa hana vigezo vya kuajiriwa moja kwa moja kwa sasa lakini wamemshauri ajiendeleze kwanza kielimu ili apewe ajira ya kudumu hapo baadae.

β€œKwakweli Mh. Rais ameguswa sana na moyo wa Mariam, Madaktari wanasema ana moyo wa kujitoa na anapenda kufanya hiyo kazi, ataingizwa katika utaratibu huo ili aweze kupata sifa, kwa sasa ana miaka 25 bado ana muda anaweza kusoma uuguzi ngazi ya astashahada akawa Muuguzi wa Watoto njiti”

AyoTV ilipotaka kufahamu kama Serikali inao mpango wa kutoa ajira hizo kwa Watu wengi zaidi ili kuokoa maisha ya Watoto njiti, Waziri Ummy amesema kwa sasa wataanza na wale wenye moyo wa kujitolea kwanza ndipo wafikirie kuwaajiri β€œTukipata Watu wenye moyo kama wa Mariam kwakweli tutakua tunawaajiri kwa mkataba, nikitoa wito watafurika wengi kwasababu wapo Watu mitaani hawana ajira”

Rais Samia alimpa Mariam milioni 2 jana kama pongezi huku Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Molllel akimchangia pia Mariam ambaye amekaa Hospitalini hapo kwa mwezi mmoja sasa akifanya huduma hiyo β€˜tumchangie chochote cha kumpa moyo kwenye 0782124700 (Alise Mwakabungu)”


Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
 
Hatupaswi endeleza huu ujinga, vifaa vinunuliwe
Ungetuliza makini ungepewa elimu, aliyekwambia vifaa hakuna nani? Unajua umuhimu wa joto la asili na hilo joto la mashine? Umeshawahi kuona watoto njiti na kuzijua changamoto zao? Hujachelewa nenda pale Muhimbili kitengo cha Kangaroo wakupe ABCD kuliko kujifanya mjuaji kwenye mitandao ya kijamii.
 
Hiyo airtel money namba ni yake

Ova
 
Mungu fundi sana, ninyi wenye matiti makubwa hadi mnakufuru Mungu jueni yaliumbwa hivyo kwa makusudi fulani. hakuna kitu kipo hapa duniani bila sababu.
 
Wanafanya Kila kitu kuwatoa mchezoni kuhusu DP WORLD naona watu hili swala lipo vichwani Mwa watu mwaka huu kazi ipo
 
Asomee ukunga moyo wa kujitolea anao, Ila kulala … kusoma darasani ukiwa mtu mzima?! Salalee 🀣😊😊
 
Aliyembusu mgonjwa akaachwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…