Serikali yampa ajira Mwanamke anayekumbatia Watoto njiti hospitali ya Amana

Kuna makala niliwahi kuangalia, ilisema kwa watoto njiti joto linalofaa zaidi ni la mwanadamu, linasaidia kwa haraka kuliko hizo incubator, sasa mnaomnanga huyu dada hebu tafuteni maarifa msiwe mnakurupuka tu
Tena staili inaitwa kangaroo, means ni ya kitaalamu pia,na natumai kabla mama kupewa fursa ya kukumbatiwa alipimwa magonjwa ambukizi kama homa ya ini,UKIMWI, TB n.k.

Kulinganisha incubator na joto la asili la mama ni sawa na kulinganisha maziwa ya mama yale ya miezi sita ya mwanzo na maziwa ya lishe.
Hivyo mimi ingawa sina utaalamu wa afya naona njia ya kangaroo ni nzuri zaidi.
 
Mkuu DR mkuu mwenyewe ndo amezengumza
Kwanza amesema shida sio INCUBATOR na wala hazipo chache
Shida ni vitanda vya mama watoto kulala hapo kuwa ni vichache na mtoto hii inafanya changamoto ya mama kuja na kurudi HOSPTARI kila siku sasa wazazi wengine wanatekeleza watoto hilo mosi

Pili kwa mujibu wa DR kumbatio la binadamu(kangaluu) lina matokeo CHANYA ya haraka zaidi kwa 100/% kuliko INCUBATOR

3 7bu iliyopelekea mpk huyo mdada kufanya hivyo alifika HOSPITAL kumuona rafikiye aliyejifungua ndo akapata taarifa kuna mtoto alitekelezwa kama sikosei au aliokotwa yupo kwenye INCUBATOR zaidi ya miezi 4 haongezeki Uzito wkt wa majadiliano ndipo nesi mmoja akasema endapo angetokea mtu akamkumbatia anauhakika ndani ya wiki angeongezeka uzito na akatoka hapo hosptari
Ndipo huyo dada akajitole kufanya Hvyo jwa wiki nzima na mtoto akaongezeka uzito akafikia LENGO la madaktari wenyewe walivyohitaji
Sasa baada ya hapo akaendelea na mishe zake ila akawaambia ikitokea kuna jesi nyingine kama hiyo wasisite kumpigia
Ndipo zikatokea kesi kama hizo mbili akaziandle kwa mtindo huo huo mpk juzi gazeti lamwananchi ilivyopublish ushujaa wake

Ajakulupuka tu kufanya hvyo MADAKTARI wana akili na wanajua wanachifanya walihakikisha yupo na AFYA njema ya kufanya jambo hilo ili isiwe na hathali zozote kwa mtoto

Zaidi pengine lina athari kwake 7bu haijulikani watoto wana magonjwa gani yeye alichofanya ni kukitolea

Sasa dr kasema kuna wazazi wanawatekeleza watoto wakishaona ni watoto NJITI kwa kushinda hiyo kazi ya kangaluu sasa huyo dada wala sio watoto wake lkani anakitolea kufanya hvyo
Je huoni kama ni ushujaa na alisatahili PONGEZI na motisha ili kurudisha IMANI kwa jamii kuwa
HUMANITY STILL EXIT
Kumbe sababu ni ukosefu wa vitanda...
Hapo ni swala la serikali
 
Tena staili inaitwa kangaroo, means ni ya kitaalamu pia,na natumai kabla mama kuoewa fursa ya kukumbatiwa alipimwa magonjwa ambukizi kama homa ya ini,UKIMWI, TB n.k.

Kulinganisha incubator na joto la asili la mama ni sawa na kulinganisha maziwa ya mama yale ya miezi sita ya mwanzo na maziwa ya lishe.
Hivyo mimi ingawa sina utaalamu wa afya naona njia ya kangaroo ni nzuri zaidi.
Watu hawaelewi wanakimbilia kuinanga serikali kama watafuta kiki lakini hiyo kangaroo inatumiwa hata na mataifa makubwa na inashauriwa kwa mama mzazi,, lakini hao watoto waliookolewa na huyu dada walitelekezwa na mama zao unaweza kuona ni namna gani amejitoa
 
Hapo issue ni kununua vifaa stahiki vya watoto njiti sio kutaka kupata misifa mitandaoni
 
tatizo wamelibeba hili jambo kihisia sana ndomana

Mwaka 2016 October nilijifungua mtoto njiti kwa njia ya oparesheni akiwa na uzito wa kg 1.2 tu, mimba ilikua ya miezi 6 na wiki mbili.

Amekaa kwenye incubator kwa muda wa siku 32 uzito ukibaki vilevile kg 1.2 pamoja na kufuata njia zote za “kitaaluma na kisayansi “ wanazoelekeza wauguzi.

Siku ya 31 nilimfata daktari mkuu wa NICU na kumuomba nijaribu njia za “kienyeji na kiutamaduni “ alizowahi kutumia mama yangu miaka mingi nyuma, baada ya mjadala mrefu na viapo vya kutokuwajibika likinikuta jambo wakanihamishia chumba cha uangalizi kuona kama method zangu zitasaidia.

Method ya kwanza, kila muda tuliopangiwa wa kwenda kunyonyesha na kuwahudumia vichanga wetu, nilimkumbatia mtoto ngozi kwa ngozi huku nikimpa maziwa kupitia bomba la sindano maana hakuweza kunyonya ziwa mwenyewe by then, zoezi hilo lilikua linadumu kwa muda wa saa nzima na dakika 45 na dakika 15 nazitumia kumsafisha yeye, Mimi na mazingira yake kwanza.

Ndani ya siku 4, mtoto uzito uliongezeka kutoka kg 1.2 mpaka kg 1.8 just like that! Baada ya kutimiza siku saba mtoto akiwa na kg 2.08 niliomba nifanye method namba mbili, kuhamia nyumbani ambapo chumba cha kulala kiliandaliwa cha kwangu na mtoto tu.

Chumba tulikifunga pote, madirisha yalizibwa kwa plastic sheeting kuleta joto, mifuko special ya kutunza maji ya moto ilikua inawekwa kuzunguka kitanda muda wote, maji yalibalishwa kila asubuhi.

Mtoto alikaa kifuani kwangu ngozi kwa ngozi kila mara maana kazi yangu ilibaki kulea tu. Huko waliingia wale wenye nasaba na mtoto tena wakiwa wasafi bila harufu yoyote ya manukato ya aina yoyote. Muda wote nilikua naosha mwili wangu kabla ya mshika na maji ya moto bila sabuni. Hatukuruhusiwa maziwa ya kopo Kwahiyo alitegemea maziwa yangu tu tena kila baada ya nusu saa (literally 30 minutes).

Siku saba baada ya kuhamia nyumbani tukarejea hospital kupima uzito na kuangalia maendeleo, mtoto alikua na kg 3.1 mwenye nuru na afya njema sana na alianza kunyonya mwenyewe.

Check up nyingine ambayo ilikua ya mwisho tukafanya mwezi mmoja baadae ambapo alikua na kg 5.4 na macho yenye kuona kila kitu. Hii ilifanya mpaka yule Doctor mkuu wa NICU kuja nyumbani kuona haswa tunafanya nini na mtoto analishwa nini maana maziwa ya kopo walinikatalia kumpa wakisema yanaleta matokeo fake.

Baada ya uongozi wa pale NICU kuona hiyo method inafanya kazi wakaiendeleza kwa pale na kuwaelekeza pia namna ya kufanya nyumbani kwa wale wenye uwezo.

My baby girl is doing perfectly fine Alhamdulillah, class 4 sasa!

Hakuna kitu kitaizidi asili, asili inaumba, asili inatibu, asili inasahihisha, ila tu ukiipa nafasi.

KTY; Tanzania hii wapo wasomi wenye uelewa wa pande zote za shilingi na wanatambua kabisa kwamba haina pande mbili tu, tuheshimu Utu!
 
Hongera sana
 
Anastahili pongezi hatukatai,,, lakini pia watu inabidi wawe wanawaza outside the box wajue namna ya kuboresha mfumo unaotumika...I don't think kama ataweza kukumbatia watoto wote pale muhimbili pekeyake
Crush wewe mtindi wa kuwabania njiti unao nkuunganishe hapa kwetu uje kuwakangaroo
 
"Tutampa ajira ya mkataba kwanza, changamoto iliyopo bado hana sita za kuajirika, tutamshauri ajiendeleze kielimu ili aweze kupata sifa za kuajirika Serikalini.
Inapendeza, ila hapo pa kumrudisha mtu shule wakati yeye kaamua kujitolea tunafeli...
 
Back
Top Bottom