Serikali yaongeza mara mbili zaidi mzunguko wa fedha (M3) kutoka 6.5% hadi 12.7%

Saruji,nondo,mabatafuta ya kula, square pipe,umeuliza bei?
 
Huu mzunguko unauonaje?haya ni makaratasi tu,hayana uhalisia na maisha ya kitaa,vitu vimepanda bei,soda zimehadimika,rushwa imerudi kwa nguvu,
 
Hakika kama mambo yataendelea kuwa hivi Rais Samia Suluhu Hassan atashinda Uchaguzi Huru na Haki wa 2025 kwa zaidi ya 76%
 
Tanzania tuko katika uelekeo sahihi sana tuendelee kumwombea rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan,

Tunakila sababu ya kujivuna,
 
Kaziindelee Tanzania
 
Hakika kuhusu money supply bado sana na Samia ashaambiwa ushauri wa bure na Shabiby bungeni mishahara ongeza, lipa madeni,lipa wazabuni, lipa wastaafu, lipa malimbikizo, weka bajeti ya taasis kufanya seminar na vikao, nunua mazao ya wakulima, pesa za tarura na madarasa zinaenda kwa wahuni wachache
 
Vitu vimeoanda bei lakini salary zimebaki palepale, huo mzunguko wa pesa umeongezekaje Waungwana mbona wengine bado tunataabika.

Sisi saidia fundi tunalipwa elfu tano ileile Kwa siku na vitu vimepanda bei, tuoneeni huruma hata kama kuna wenzetu mnapata na kizidishiwa tutazameni wachini.

Tunalima pia Ila hatujui bei hii ya mbolea kama tutaweza kununua maana mahindi tuliyovuna tuliuza 20,000 Kwa gunia Kwa kuwabembeleza wanunuzi walau wanunue Kwa bei hiyo.

Mtuombee Kwa mheshimiwa rais walau atusaidie aweke karuzuku flani kwenye mbolea ili tusiingie kwenye njaa mwakani.
 
Tatizo haha mambo

Hizi issue za uchumi mnazo publish ziko too theoretical kiasi cha kushindwa kurelate na maisha halisi ya watu.
 
Mkuu tuendelee kumwombea Rais huyu mambo yanakuja mazuri mazuri
 
Kazi nzuri sana Rais wetu kipenzi,
 
Wewe mchambuzi mpumbafu tu, Huna hoja kabisa,


Mimi nafanya vitu serious wewe unaleta UCHADEMA kwenye vitu serious,
We need practical and tangible facts but not paper and wishfully thought phenomena. "Haya ni mambo ya bear-feet economists tu". Pesa ni "kawaka" to a grass-root citizen.
 
Nonsense
 
Huo mzunguko uko kwenye mifuko ya wana Lumumba na nyie chawa buku 7!

Maana mzunguko wa fedha mtaani hakuna kabisa kila mtu analia noki!
 
Bora hata mchambuzi, kwanza mkongwe humu ndani. Wewe sijui hata umetokea wapi. Unaleta vitu ambavyo havina ukweli. Mtaani kugumu, vitu vimepanda bei, vipato ni vilevile, halafu unaleta utopolo wako?
Huyu dogo mchawi kweli yani naona anantaftia ban tu na sifa zake za kindezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…