Sipatii picha bus linapita kitonga usiku na sehemu kama hizo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kuna siku nilipanda IT kutoka Dar, tukafika msamvu dereva akapakia abiria wengine wawili wote wa kiume safari ikaendelea na story nyingi.
Hapo mdada nipo peke yangu. Tulivyofika Mikumi wakatokea abiria wengine wawili nao wanaume tupu. Dereva akaingia tamaa walitaja pesa nyingi akawapakia hivyo hivyo kwa kubanana.
Mimi sikuwa na muda nao si nimekaa zangu mbele kwa dereva.
Shuhuli ilianzia tulivyozianza zile kona za Iyovi wale majamaa yaliyopakiwa Msamvu yakaanza kuongea lugha tusizozielewa. Muda huo dereva yupo speed, mbele katikati tukaona wale wakaka waliokuwa wanaongea kilugha wamechomoa MAPANGA yamenolewa kote kote yanang’aa.
Wanamwambia dereva paki gari pembeni, dereva anatetemeka panga liko shingoni mimi muda sielewi kitu nilikumbuka kusema Mungu nisaidie.
Lakini cha kushangaza wale wakaka wengine wao wametulia, nikaangalia kwenye kioo mmoja wa wale majamaa wengine anamuonyesha ishara dereva lakini sijaielewa.
Dereva akapaki gari tukashuka wote, wale majambazi wanaitaka gari na walishachorewa ramani na watu wao. Kabla hawajachukua gari tukashangaa wale wakaka wengine wanachomoa silaha za kazi [emoji23][emoji23][emoji23] woiiiih!!
Nikasema hii movie ya Damme leo naiona live.
Wakawaambia nyie wangese aliewaambia gari inaibiwa kijinga namna hii nani? Haya tupa mapanga chini kabla hatujamwaga ubongo wenu. Wakatupa zile panga yule mwenzie akazichukua, tukaambiwa we sister na suka ingiieni kwenye gari. Wale majambazi wa mapanga wakaomba basi bro tusameheane usiku saa hizi porini hapa tupeni lift mkatuache hata Ruaha Mbuyuni [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wale majambazi wa bunduki mmoja akamuuliza dereva, “Oya suka hawa maboya wamekulipa nauli yako?” Dereva akasema hawajanilipa, akaulizwa unawadai shingapi? Akajibu, tulikubaliana elfu 60,000 wote wawili. Wakaambiwa leteni pesa hizo wakatoa lakini kwa manung’uniko. Akaambiwa oya mwanangu suka chukua pesa zako. Na nyie maboya mnabaki hapa mtajua wenyewe mnatoka vipi.
Safari ikaendelea ila hatujui hawa kina Van Damme na mwenzie Dolph tunamalizana nao vipi??
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]