Serikali yatuma maafisa wake Poland na Hungary kunusuru Watanzania waliokwama Ukraine

Serikali yatuma maafisa wake Poland na Hungary kunusuru Watanzania waliokwama Ukraine

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri Mulamula amesema Serikali imepeleka maofisa wake katika nchi za Hungury na Poland ili kuratibu safari za wanafunzi waliokwisha vuka mpaka kutokea Ukraine.

Kadhalika kuna wanafunzi ambao wameamua kwenda kuishi kwa ndugu na jamaa zao huko Denmark, Slovakia na Sweden.

Wanafunzi 11 wako njiani wakirejea nchini na mmoja amebaki Poland baada ya kubainika ana Corona.

Chanzo: ITV habari
 
Yaani ndo kwanza wanaenda kuratibu mbona wamechelewa sana siku zote hizo karibu wiki mbili tangu vita vianze kama kutaabika watakuwa wameshataabika sana
 
Hao “maofisa” wako kwenye ndege ila mioyoni mwao wanawaza tu hizo padiem zao na namna ya kiextend 😅😅
 
Mungu awanusuru wahanga wa hii vita.

Mungu awape moyo wa imani viongozi wa Ukraine na Russia wakae na kumaliza tofauti zao bila vita
 
Nasikia kuna watanzania kibao wamebanwa ndani ya mzozo wa Rusisia na Ukraine na hali kwenye baadhi ya miji inakuwa mbaya.

Tiss walipaswa kujua hii hali mapema na kuwahamisha watz wote waliopo huko Ukraine.

Hii ndio kazi mojawapo ya Tiss ni kuhakijisha raia waliopo nje wanarudi nchini safe kabla ya majanga hayajatokea.

Hii ni failure to them.
 
Msijitie wajuaji sana. Nchi ngapi zili evacuate raia wake kabla ya bomu la kwanza kutua ukraine? Hao wote hawakupata taarifa?
 
Nasikia kuna watanzania kibao wamebanwa ndani ya mzozo wa Rusisia na Ukraine na hali kwenye baadhi ya miji inakuwa mbaya.

Tiss walipaswa kujua hii hali mapema na kuwahamisha watz wote waliopo huko Ukraine.

Hii ndio kazi mojawapo ya Tiss ni kuhakijisha raia waliopo nje wanarudi nchini safe kabla ya majanga hayajatokea.

Hii ni failure to them.
Big failure kwao pamoja na MI.
 
Back
Top Bottom