John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, leo Alhamisi amesema atatoa leseni za kuanza kuchapishwa kwa magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima, Mseto na Mawio “Kifungo kimetosha. Kikubwa kazi iendelee,” amesema Nape.
"Agizo la Rais ni Sheria,leo nitatoa leseni kwa Mwanahalisi,Mawio,Mseto,Tanzania Daima ambayo yalikuwa yamefungiwa, tuanze kwa kufungua ukurasa mpya Ili tumalize kabisa jambo hili,kifungo kimetosha " Amesema Waziri Nape
===
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Leseni zitatolewa kwa Magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa. Magazeti hayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima.
Ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam leo Februari 10, 2022 katika Kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari na kusema, "Kifungo kimetosha".
Aidha, amesema Serikali inalenga kuboresha mahusiano kati yake na akieleza, "Rais ameelekeza kupitiwa #Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Sekta ya Habari na kuona namna ya kuzifanya ziwe rafiki na sio kikwazo katika shughuli za Wanahabari"
Amesema Serikali itatumia Bussra kuhakikisha mambo yanaenda sawa, na kwamba nia ya Serikali ya Awamu ya Sita ni njema hivyo watengeneze mahusiano na maridhiano mazuri, pia washikamane kwa pamoja.
Ameongeza, "Najua tulipotoka, wakati mwingine safari ya mabadiliko sio rahisi na inaweza kuchukua muda. Inapochukua muda haimaanishi safari imesimama maana ni rahisi kutuhumiana kutosonga mbele. Wakati mwingine unasafiri unakwenda unakutana na jiwe, ukikutana na jiwe using'ang'anie kulipasua, rudi hatua moja nyuma nenda kushoto au kulia unaenda mbele. Ukirudi hatua moja haimaanishi umeamua kuacha safari, bali unatafuta njia nzuri ya kuendelea na safari".
Zaidi, soma:
- Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia
- Serikali yasitisha leseni ya kuchapisha na kusambaza Gazeti la Tanzania Daima kuanzia Juni 24, 2020
- Serikali yalifungia gazeti la MSETO kwa miaka 3 kwa kuandika habari likitumia nyaraka za kugushi
- Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini
- MISA-Tanzania yatoa tamko kuhusu kufunguliwa kwa magazeti manne