Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto

Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
1644486870061.png


Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, leo Alhamisi amesema atatoa leseni za kuanza kuchapishwa kwa magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima, Mseto na Mawio “Kifungo kimetosha. Kikubwa kazi iendelee,” amesema Nape.

"Agizo la Rais ni Sheria,leo nitatoa leseni kwa Mwanahalisi,Mawio,Mseto,Tanzania Daima ambayo yalikuwa yamefungiwa, tuanze kwa kufungua ukurasa mpya Ili tumalize kabisa jambo hili,kifungo kimetosha " Amesema Waziri Nape

===
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Leseni zitatolewa kwa Magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa. Magazeti hayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima.

Ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam leo Februari 10, 2022 katika Kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari na kusema, "Kifungo kimetosha".

Aidha, amesema Serikali inalenga kuboresha mahusiano kati yake na akieleza, "Rais ameelekeza kupitiwa #Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Sekta ya Habari na kuona namna ya kuzifanya ziwe rafiki na sio kikwazo katika shughuli za Wanahabari"

Amesema Serikali itatumia Bussra kuhakikisha mambo yanaenda sawa, na kwamba nia ya Serikali ya Awamu ya Sita ni njema hivyo watengeneze mahusiano na maridhiano mazuri, pia washikamane kwa pamoja.

Ameongeza, "Najua tulipotoka, wakati mwingine safari ya mabadiliko sio rahisi na inaweza kuchukua muda. Inapochukua muda haimaanishi safari imesimama maana ni rahisi kutuhumiana kutosonga mbele. Wakati mwingine unasafiri unakwenda unakutana na jiwe, ukikutana na jiwe using'ang'anie kulipasua, rudi hatua moja nyuma nenda kushoto au kulia unaenda mbele. Ukirudi hatua moja haimaanishi umeamua kuacha safari, bali unatafuta njia nzuri ya kuendelea na safari".

Zaidi, soma:
- Gazeti la MwanaHALISI lafungiwa kwa miaka miwili, wahukumiwa kwa kuandika habari za uzushi kuhusu Mwakyembe na Makinikia

- Serikali yasitisha leseni ya kuchapisha na kusambaza Gazeti la Tanzania Daima kuanzia Juni 24, 2020

- Serikali yalifungia gazeti la MSETO kwa miaka 3 kwa kuandika habari likitumia nyaraka za kugushi


- Gazeti la Mawio lafungiwa kwa miezi 24 kwa kosa la kuwahusisha Mkapa na Kikwete sakata la madini

- MISA-Tanzania yatoa tamko kuhusu kufunguliwa kwa magazeti manne
 
TITLE YA KWANZA YA TANZANIA DAIMA

1. Shaidi wa serikali kesi ya Mbowe akimbia kizimbani

2. Mashaidi wa kesi ya kubumba watoka nduki mahakamani
Sasa akina Bonny ndio watakuwa waandishi wa Tanzania Daima.

Sitashangaa likifungiwa tena na huyo huyo aliyelifungulia!
 
Wayafungulie tu kwani wakisemwa wanakufa? kuambiwa ukweli wakati mwingine kunakusaidia kuona matundu katika nguo yako, ni aibu kubwa sana na mamisaada mengi nchi imenyimwa kutokana na kuruhusu mtu mmoja tu aamue nani aseme na nani asiseme, shame on us, wapige kazi sasa nao wasiingie kwenye mkumbo ule wa mulaga.
 
Agizo la Rais siyo sheria Nape Nnauye umepotosha lasivyo wenzio wangekuwa wameyafungulia toka mwanzo!

Nchi hii haiwezi kuendeshwa na matamko ya Rais siyo nchi ya kifalme hii ni nchi inayo endeshwa kwa sheria na taratibu na katiba ya nchi siyo matamko!

Suluhu hapa ni kubadilisha sheria husika ya magazeti msiwageuze watu watumwa kutegemea huruma ya mtu mmoja kwa sababu ni Rais....
 
Ni hatua nzuri katika kuendeleza dhana ya uhuru wa habari.Gazeti la Mwanahalisi lilikuwa linawakosesha usingizi viongozi mbalimbali wa serikali kutokana na habari zake za kiuchunguzi kuwa za kweli na uhakika.Hongera sana kaka yangu Nnape.
 
Anatafuta namna ya kujibu maswali atakayoulizwa na waandishi wa habari makini huko ulaya, akirudi anauafungia tena au anayaziba midomo
 
Basi Mwanahalisi itaanza na madudu ya Makonda, Tanzania daima itakuwa inaweka yaliyojiri mahakani kesi ya mbowe na kifuatilia ugonjwa wa afande Swila
Habari njema sana, nitaanza tena kununua magazeti. Itakuwa burudani kubwa kuwasoma tena akina KONDO TUTINDAGA, NARONYO KICHEERE, SAED KUBENEA, na wengineo. Hawa jamaa huwa hawaogopi kabisaaa kufukua kinyesi, mizoga na yooote yaliyoooza na kuvunda ila yamefichwa!!
 
Back
Top Bottom