SGR inahujumiwa kwa maslahi ya nani?

kweli wanazingua sana mie jumatano niltaka tiket ya Moro Dar ( Royal Class) inasema Bei ni 50,500 wakati nimeenda MORO kwa same class for 35500
 
Kama mfumo unaruhusu mtu kuweka booking kwa muda mrefu basi kuna changamoto, inapaswa pawe na limit ya muda ambao booking yako inakua inahesabika, mfano ni mifumo mingi ya mabasi inatoa dakika 15 tu za kulipia baada ya kuweka booking.

Kama tiketi zinakua zimelipiwa ili wapate chajuu basi hapo shirika halipotezi kitu, lakini kama zinashikiliwa bila malipo hilo ni tatizo kubwa sana.
 
Kama ni inside job,yawezekana online inaonekana imejaa,ila baadhi ya mabehewa yatakua yanaenda yakiwa pungufu.
 
Wanafanyaje? Maana kinahitajika kitambulisho kununua tiketi na wakati wa kupanda.
Na hela unalipia lwa control number. Hii ya kununua kwa mtu inakuaje?
 
MBUPU.............treni 8 hizo kwa njia ngapi???
nani atasimami???
mwendokasi ina majibu ya SGR 8
tuwe wakweli, mambo ya kiofisi ni ya wazungu,sisi watu weusi sio kujidharau, HATUWEZI mambo ya kiofisi sisi zetu NGOMA
 
Kama ni inside job,yawezekana online inaonekana imejaa,ila baadhi ya mabehewa yatakua yanaenda yakiwa pungufu.
Nawaza pia kama zingekua zimeshalipiwa kwa majina ya hao walionunua mwanzo, ingemlazimu mtu kupewa tiketi yenye jina la mtu mwingine.

Lakini kama ukiongezea hiyo 5000 unapewa tiketi yenye jina lako, basi kuna mtu kacheza na mfumo.
 
same way hata kwenye mabasiya mikoani haswa misimu ya skukuu watu hununua tiketi alafu utazinunua kwa bei kubwa ukiwa na haraka! huezi mlaumu mtu anafanya biashara na hajamzulumu mtu
Wakomeshe hili linampa mzigo MTANZANIA wa kawaida, wakati abiria anaingia ndani ya treni,tiketi aliyokata ilipaswa iwe inasoma jina lake halisi,kwa series za number ametumiwa,katika check -in.
 
Mleta uzi ameamua
mkuu,

Ukiingia kwenye website yo, Mbona Dar moro kesho royal ina nafasi? Keshokutwa ticketi bado zipo kwa baadhi ya route na siku inayofutia kila route bado ina situ zaidi 700?

Hii hadi tarehe 18 kuwa zimejaa/zimelanguliwa umeitoa wapi??? Factcheck kwanza..
 
huezi, izo ni biashara kama biashara zingine! yeye akinunua asipopata mteja wewe kama serikali bado utakua umepata mapato
Zikinunuliwa zote kwa mtindo huo wa kuhodhi na kulangua halafu watu wanakwenda mtandaoni wapo mbali kabisa na Dar, Moro au Dodoma wanataka kupangilia ratiba zao za kusafiri unafikiri mambo yatakuwa vipi sheikhe?
 
Nakuunga mkono mkuu.
 
Hii ndio Tanganyika ya CHURA a.k.a Dalali.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Zikinunuliwa zote kwa mtindo huo wa kuhodhi na kulangua halafu watu wanakwenda mtandaoni wapo mbali kabisa na Dar, Moro au Dodoma wanataka kupangilia ratiba zao za kusafiri unafikiri mambo yatakuwa vipi sheikhe?
still bado ulitakiwa ufanye mapema, hio ni biashara pia! unatafuta nyumba ya kupanga unapewa ila at a cost mfano mwezi mmoja wa dalali, ndo maisha yako ivo
 
Nakuunga mkono mkuu.
Mkuu ni rahisi sana kumdanganya Mtanzania. Imagine link ya kufanya booking iko online na ticket zipo (hata kesho royal ina siti baadhi) jumatatu asubuhi imejaa (watu wanarudi makazini dom au moro) lakini baadaye kuna siti kwenye baadhi ya route - jumanne na kuendelea siti zipo za kumwaga... lakini mtu hatacheki kwanza, atacomment hapa kukandia bila hata kufactcheck na vitu viko online. Inashangaza kidogo
 
still bado ulitakiwa ufanye mapema, hio ni biashara pia! unatafuta nyumba ya kupanga unapewa ila at a cost mfano mwezi mmoja wa dalali, ndo maisha yako ivo
Bila shaka unanufaika binafsi na udalali huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…