SGR inahujumiwa kwa maslahi ya nani?

SGR inahujumiwa kwa maslahi ya nani?

Pamoja na kuwa ni biashara..lkn ni huduma, kutoa huduma kuna masharti yake, mfano huhitaji dalali(mtu wa kati) kwenye kutoa huduma..huyo anayenunua zote halafu si msafiri kwa lengo la kuuza tena ni dalali..si sahihi.
Muulize tu, huyo uliyemjibu; huyo "DALALI" anayemwita yeye kuwa ni mfanya biashara; anayo liseni ya biashara hiyo, analipa kodi stahiki ya biashara hiyo?
 
Sidhani kama kweli kuna watu wanazinunua zote halafu wao wauze kwa ongezeko la 5000 tu stesheni.

Kama behewa zinatembea nusu daily hiyo si ni biashara kichaa.

Faida wanapataje sasa?
 
Ukitaka ku-book tiketi ya Dar- Moro au Dom mtandaoni tiketi hamna ila ukienda stesheni unapata tiketi kwa kuongeza 5,000/- kwa mkatishaji tiketi. Nimepanda treni ya Dar- Moro mabehewa yapo nusu ila kwenye ku-book nafasi zimeshikiliwa/full hadi tarehe 18/07. Hakika Tutafika tumechoka.
Wananchi mnalalamika kama mna Rais
 
hujawahi kununua tiketi ya basi kwa bei kubwa kipindi cha skukuu?
Kwa hiyo hii ndiyo iwe sababu ya kuhalalisha ubovu wa TRC?
Kwa maana yako hii ndiyo iwe njia inayokubalika kufanya shughuli kama hizi ndani ya nchi hii?
 
Ukitaka ku-book tiketi ya Dar- Moro au Dom mtandaoni tiketi hamna ila ukienda stesheni unapata tiketi kwa kuongeza 5,000/- kwa mkatishaji tiketi. Nimepanda treni ya Dar- Moro mabehewa yapo nusu ila kwenye ku-book nafasi zimeshikiliwa/full hadi tarehe 18/07. Hakika Tutafika tumechoka.
Kama mradi wa Mabasi ya mwendo kasi umeshatushinda sebuse hiyo SGR.
 
Hizo ni fursa tu

Mtu ananua tiketi zote halafu anachuuza dirishani

Dawa yake ilitakiwa ziwe treni kama nane hivi zote zinaondoka kwa kufuatana kingewaka

Biashara hiyo mbona ni kama ya mazao nyie wajanja mnakuja kutuchuuza Bush huko mnaenda kuuza kinondoni supermarket kwa bei hata mara tano zaidi ya mlivyonunua
Mzee hakuna kitu kama hicho
 
Sasa biashara gani ununue tiketi 100 uuze nusu yake? Hakuna anayefanya hiyo biashara. Ni kwamba wakatisha tiketi wapo radhi train liende tupu kama hawapati mtu wa kuwapa rushwa.
LABDA IWE MWIKO KUUZA TIKETI MANUAL/ ZIUZWE ONLINE TU.ITAEPUSHA MENGI SANA.
 
Private sekta ndo unafanisha mradi wa serikali hizo treni zimenunuliwa kwa kodi za Wananchi serikali inatakiwa ipige marufuku vishoka wanaolangua ticket uoni hao vishoka wanagombanisha wananchi na serikali? Duniani kote kazi ya serikalini ni kukusanya kodi na kutumia kodi kuleta maendeleo na kufanya gharama za maisha kua nafuu sana kwa wananchi
hujawahi kununua tiketi ya basi kwa bei kubwa kipindi cha skukuu?
 
Mkuu ni rahisi sana kumdanganya Mtanzania. Imagine link ya kufanya booking iko online na ticket zipo (hata kesho royal ina siti baadhi) jumatatu asubuhi imejaa (watu wanarudi makazini dom au moro) lakini baadaye kuna siti kwenye baadhi ya route - jumanne na kuendelea siti zipo za kumwaga... lakini mtu hatacheki kwanza, atacomment hapa kukandia bila hata kufactcheck na vitu viko online. Inashangaza kidogo
Kwa kweli hata mimi nimeshangaa. Maana kabla ya ku comment nimeingia kukagua, nikakuta seats kibao.
 
Mkurugenzi bado ni mpya akitulia ofisini kitaeleweka.... sitaki kuamini maneno ya yule askofu wa kanisa!
 
..kuna shida gani ku-sub contract ukatishaji wa ticket na huduma zingine zote kwa SGR..vinywaji, chakula, mapokezi, ulinzi, wahudumu..nini shida? Bado ndani ya serikali kuna watu wanadhani serikali inaweza kufanya biashara ikafanikiwa? Labda punguani ndio bado anaamini hivyo.
 
Private sekta ndo unafanisha mradi wa serikali hizo treni zimenunuliwa kwa kodi za Wananchi serikali inatakiwa ipige marufuku vishoka wanaolangua ticket uoni hao vishoka wanagombanisha wananchi na serikali? Duniani kote kazi ya serikalini ni kukusanya kodi na kutumia kodi kuleta maendeleo na kufanya gharama za maisha kua nafuu sana kwa wananchi
ni kwel kabisa lakini angalia na wewe upande wako, kila mttu akinunua mapema unadhan hawa vishoka watatoa wap hili soko?
 
Back
Top Bottom