SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

Dunia nzima usafiri wa train ni rahisi kuliko usafiri wowote na sababu ziko wazi kwakuwa train inabeba watu wengi na mizigo mingi inapunguza gharama za uendeshaji, sasa ni lazima waweke bei chini ya usafiri wa ndege au magari hii itachochea sana wingi wa abiria na mizigo na hata parcels ndogo ndogo waweke utaratibu wa mzuri watabeba soko lote wafanye wepesi bila urasimu yaani service bora kuliko waliopo. Itasaidia kuwa na train kwa siku hata mara 4 na kila trip zikiwa nyingi gharama za operation zinashuka. Wasiliuwe shirika kama walivyofanya reli ya kati na Tazara.
Za ndege zinapanda na madeni maradufu, kweli gharama za tren ndo ziwe nafuu kwa uendeshaji?
 
Nauli zilizopendekezwa na TRC kutoka Dar es Salaam-Morogoro zilikuwa kwa darasa la tatu 24,794/- kwa mtu mzima, na 12,397/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12.

Kwa Daraja la Uchumi, njia hiyo hiyo ilikuwa 29,752/- kwa mtu mzima na 14,876/- kwa watoto. Kwa darasa la tatu kutoka Dar es Salaam-Dodoma 59,494/- kwa mtu mzima na 29,747/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12. Darasa la Uchumi 71,392/- kwa mtu mzima na 35,696/- kwa watoto.

Kwa njia ya Dar es Salaam-Pugu, daraja la tatu 4,694/- kwa mtu mzima na 2,347/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12. Walipendekeza 5,632/- kwa kila mtu mzima na 2,816/- kwa watoto ambao wangependelea kutumia darasa la uchumi kwa njia sawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya TRC, Ally Karavina, alieleza kuwa ana imani na majaribio yanayoendelea na alisema treni hizo zitaanza kufanya kazi Julai mosi kama ilivyoagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Sielewi hayo madarasa uchumi na tatu wanamaanisha nini
 
Kwa garama izi wabinafsishe tu maana hawajielewi
Kwa akili za wale matapeli wanaojiita manabii, "nazoom naona wafanyabiashara wa mabasi, nawaona wameweka msisitizo nauli ya treni iwe juu kuliko mabasi"

"... kisha mbele kidogo naona mzigo kwa serikali kuendesha mradi huu utakuwa mkubwa na garama zitakuwa kubwa, hivyo naona CAG akitoa taarifa za hasara kupitia SGR, ndipo roho mchafu anayetawala sasa anasema mradi ubinafsishwe haraka sana kwa mwerarbeu"
 
Tafuta hela uache makasiriko, masikini hawana chao cha haraka
Haya ndo yanasababisha hata viongozi wanaopewa dhamana kula pesa na kuacha wananchi wanahangaika kwa vitu vidogo ambavyo serikali ilitakiwa iwatimizie kama hizi social service, inamaana huoni kuna haja ya mwananchi kuounguziwa gharama za usafiri? Unaona ni haki kabisa
 
Kwa akili za wale matapeli wanaojiita manabii, "nazoom naona wafanyabiashara wa mabasi, nawaonw wameweka msisitizo nauli ya treni iwe juu kuliko mabasi"

"... kisha mbele kidogo naona mzigo kwa serikali kuendesha mradi huu utakuwa mkubwa na garama zitakuwa kubwa, hivyo naona CAG akitoa taarifa za hasara kupitia SGR, ndipo roho mchafu anayetawala sasa anasema mradi ubinafsishwe haraka sana kwa mwerarbeu"
Huyo mwerarbeu ndio maarab ama sijakupata?
 
Ingekuwa watu wangekuwa na mawazo kama wewe kusingekuwa na ndege wala wapanda ndege
Kungekuwa na garama reasonable fare ya ndege kama fast jet sidhani kama ndege ingeondoka to Mwanza na abilia 40 au kuhairishwa au kubadilishwa kwa safari.

Kuna mabasi kwenda mwanza nauli 55,000 na lingine 120,000/- na watu wanalipa unajua kwa nini?.
 
Serikal imetumia trillion za pesa afu watu mnaraumu kulipa nauli ndogo iyo
Iv wabongo tuna upungufu wa akili sometime kwaiyo mlitaka mpande bure au mlitaka waweke nauli za mabasi ya mwendo kasi kwenye treni ya umeme

Tufikie hatua wabongo tuache kulalamika sana km nauli ya treni bei kubwa si unapanda tu basi mbona iyo njia ina mabasi meng tu

ATCL wana bei kubwa kuzid precisio Air na hujawai kusikia watumiaji wa ndege wanalalamika
Nauli za daladala mlalamike nauli za mabasi mlalamike nauli ya treni nayo mnalalamika
 
Back
Top Bottom