SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

SGR Mchakato wa Nauli ndiyo huu hapa, mtoto hadi Moro kulipa Tshs 12,400

Mkurugenzi mkuu wa TRC ndg Kadogosa alikuwa akiongea na kamati ya bunge walipotembelea mradi huo na kusema "Kuhusu mchakato wa nauli, sisi TRC tumemaliza sehemu yetu ambapo tumewasilisha kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) kila kinachohitajika."

View attachment 2948956

Alisema wanaelewa kuwa LATRA tayari imeshafanya vikao na wadau wa Dar es Salaam na Dodoma.

"Tunaamini kwamba kabla ya kuanza kazi Julai mwaka huu, tutakuwa tayari tumetangaza nauli," Kadogosa aliongeza.

LATRA imepewa jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa nchi kavu, haswa usafiri wa barabara, reli, na waya. Ina mamlaka ya kukagua na kuweka viwango na malipo.

Kando na hayo, pia inawaidhinisha madereva wa treni na wafanyakazi wa treni. Mwaka 2022 LATRA iliwaalika wadau wa sekta ya reli na wananchi kwenye mkutano wa kujadili mapendekezo ya nauli kwa kuzingatia nauli za abiria kwa treni ya SGR kutoka Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma-Bahi kwa ombi la TRC.

Nauli zilizopendekezwa na TRC kutoka Dar es Salaam-Morogoro zilikuwa kwa darasa la tatu 24,794/- kwa mtu mzima, na 12,397/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12.

Kwa Daraja la Uchumi, njia hiyo hiyo ilikuwa 29,752/- kwa mtu mzima na 14,876/- kwa watoto. Kwa darasa la tatu kutoka Dar es Salaam-Dodoma 59,494/- kwa mtu mzima na 29,747/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12. Darasa la Uchumi 71,392/- kwa mtu mzima na 35,696/- kwa watoto.

Kwa njia ya Dar es Salaam-Pugu, daraja la tatu 4,694/- kwa mtu mzima na 2,347/- kwa watoto kati ya umri wa miaka 4-12. Walipendekeza 5,632/- kwa kila mtu mzima na 2,816/- kwa watoto ambao wangependelea kutumia darasa la uchumi kwa njia sawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya TRC, Ally Karavina, alieleza kuwa ana imani na majaribio yanayoendelea na alisema treni hizo zitaanza kufanya kazi Julai mosi kama ilivyoagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Hawa tayari wamefeli hata kabla usafirishaji haujaanza
 
ni kama ndege tu, wenye uwezo wakapande saa moja na nusu wapo mwanza, na wengine wasioweza wakapande basi watembee masaa 16. nashauri nauli ziwe hivyo ili wapate pesa ijiendeshe, isihitaji kupigwa fund na bajeti ye serikali Kuu. reli ijiendeshe kama sherika. na wateja watapata wengi sana tu. hasa kwa DAR - DOM. hadi watu watakuwa wanapanga foleni.
Yaani safi kabisa!.

Huwezi mwendokasi 750/- kapande daladala za 400/- leo iko wapi?.

Haya njoo kwenye DART ilikuwaje mwanzo na watu walisemaje hadi leo tumefika wapi?.
 
Kwenye sheria ya bara bara, kwa usafiri wa gari/basi mtoto chini ya miaka 5 halipi nauli. Ila kwenye treni mtoto wa miaka 4 analipa nauli na msimamizi ni yule yule LATRA 😂😂.
Mchawi ni umaskini wa Watanzania tu mkuu asikudanganye mtu.

Sisi ni mafukara wa kutupwa hata hizo nauli siyo kubwa ila Sisi ndio mafukara, na infantry kulipa nauli kwenye train ni sahihi.

Shida inaanzia kwenye vipato, hawa wanachukuwa sample ya maisha ambayo first world kibaruwa analipwa USD 20 Kwa saa, akifanya kazi masaa 10 kila siku anaingia USD 200kwa siku, Kwa wiki Monday to Saturday mshahara wake ni USD 1200, hapo hata ukimkata Kodi bado ana serving nzuri ndio sababu wenzetu wanajimudu kimaisha.

Sisi tunaishi Kwa kudra za Mungu tatizo liko hapo, mtazunguka Sana lakini hamtopata jibu, ukweli ni huo na hizo bei ziko Sawa ila si Sawa Kwa Watanzania wanaonuka ufukara.
 
Morogoro hapo haraka ya nini,abood linatosha
Hata ulaya wazungu wanafanya hizi option, kuna miji train inakwenda Kwa masaa mawili, couch ni masaa matano, mzungu anaopt kupanda couch.

Hata train London kwenda Paris France ni miles kama 220 hivi au kilometres 340 ukikata ticket ya kwenda na kurudi ni $60 na ukikata one way NI $100 ni mwendo masaa 2 na nusu, sasa chaguo ni lako upande ndege au train.
 
Mchawi ni umaskini wa Watanzania tu mkuu asikudanganye mtu.

Sisi ni mafukara wa kutupwa hata hizo nauli siyo kubwa ila Sisi ndio mafukara, na infantry kulipa nauli kwenye train ni sahihi.

Shida inaanzia kwenye vipato, hawa wanachukuwa sample ya maisha ambayo first world kibaruwa analipwa USD 20 Kwa saa, akifanya kazi masaa 10 kila siku anaingia USD 200kwa siku, Kwa wiki Monday to Saturday mshahara wake ni USD 1200, hapo hata ukimkata Kodi bado ana serving nzuri ndio sababu wenzetu wanajimudu kimaisha.

Sisi tunaishi Kwa kudra za Mungu tatizo liko hapo, mtazunguka Sana lakini hamtopata jibu, ukweli ni huo na hizo bei ziko Sawa ila si Sawa Kwa Watanzania wanaonuka ufukara.
Mradi ungejiendesha kwa kusafirisha mizigo ila sasa huu unataka kujiendesha kwa kusafirisha abiria.

Anyway, serikali haziwezi kufanya biashara.
 
Back
Top Bottom