evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,035
- 8,218
Mkuu hapa kwa nilivyofuatilia hili jambo raia sio kwamba wamefurahishwa au hata kukasirishwa kwa kuchomwa kwa picha hiyo.Mimi nadhani dhumuni la adhabu ni kukomesha kosa kama Hilo lisifanyike tena.
Chaula amejirekodi alichokifanya na kukituma mtandaoni.
Maneno yake na vitendo vyake vinaweza kusababisha chuki,taharuki na hasira kwa umma.
Tatizo mnadhani watu wote hapa Nchini hawampendi Rais,na wamefurahishwa na picha yake kuchomwa,sio kweli.
Watu wamekasirishwa kwa kitendo cha Serikali kuonekana kufuatilia vitu vidogo vidogo sana wakati kuna matatizo makubwa sana ambayo yamefungiwa macho mfano ubadhirifu unaoibuliwa na CAG kila mwaka.
Serikali ingeachana na mambo madogomadogo kama hayo huyo kijana kama sio RC wa mbeya kukurupuka na kutaka akamatwe habari yake hata isingesambaa.
Huko mitandaoni mbona watu wanapost mambo ya ajabu ajabu na wala hawafuatiliwi.
Baadhi ya viongozi liwe fundisho kwao waache kukurupuka kama hii ishu ya huyu kijana imewapa sintofahamu wenye mamlaka kwamba wananchi wameamua kumchangia fedha kwamba wamefurahia kitendo cha huyo kijana kuchama picha ya Rais wao.
RC wa mbeya ujue umekurupa na umemdhalilisha Rais na bosi wako kwa kuweka wazi kwamba wananchi wengi hawampendi hadi wanafurahi kuchomwa kwa picha yake