Eti wateule wa JPM.
Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais John Joseph Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Katibu wa CCM Morogoro kwa tuhuma za rushwa
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamidu Shaka amesimamishwa kazi na chama hicho ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kula rushwa zinazomkabili.
Hayo yamebainishwa jana Alhamis Februari 11,2021 na Rais John Magufuli wakati akizindua soko kuu la Morogoro ambalo amependekeza liitwe Soko Kuu la Chifu Kingaru.
Hata hivyo licha ya Rais Magufuli kutomtaja jina amesema kuwa katibu huyo atajadiliwa kwa tuhuma za kula rushwa kutoka kwa madiwani wakati wa mchakato wa upatikanaji wa meya wa Halmashauli ya Manispaa ya Morogoro.
“Na wewe mstahiki Meya (Pascal Kihanga) nataka ubadilike najua umeupata umeya wa bahati bahati hapa, mimi napenda kuzungumza ukweli kwani nasema uongo ndugu zangu? Aliuliza Rais Magufuli na kuongeza,
“Hukutakiwa kuwa meya aliyetakiwa sikumrudisha kuwa meya na bahati mbaya hata utafutaji wa meya hapa ulikuwa umejaa rushwa na ndio maana Katibu wa CCM wa hapa tumemsimamisha kazi atajadiliwa kwa sababu alikula rushwa kwa madiwani,” alisema Magufuli.