Shaka Hamidu Shaka, mrithi wa Polepole nafasi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM

Shaka Hamidu Shaka, mrithi wa Polepole nafasi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM

Eti wateule wa JPM.

Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais John Joseph Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Katibu wa CCM Morogoro kwa tuhuma za rushwa

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamidu Shaka amesimamishwa kazi na chama hicho ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kula rushwa zinazomkabili.

Hayo yamebainishwa jana Alhamis Februari 11,2021 na Rais John Magufuli wakati akizindua soko kuu la Morogoro ambalo amependekeza liitwe Soko Kuu la Chifu Kingaru.

Hata hivyo licha ya Rais Magufuli kutomtaja jina amesema kuwa katibu huyo atajadiliwa kwa tuhuma za kula rushwa kutoka kwa madiwani wakati wa mchakato wa upatikanaji wa meya wa Halmashauli ya Manispaa ya Morogoro.

“Na wewe mstahiki Meya (Pascal Kihanga) nataka ubadilike najua umeupata umeya wa bahati bahati hapa, mimi napenda kuzungumza ukweli kwani nasema uongo ndugu zangu? Aliuliza Rais Magufuli na kuongeza,

“Hukutakiwa kuwa meya aliyetakiwa sikumrudisha kuwa meya na bahati mbaya hata utafutaji wa meya hapa ulikuwa umejaa rushwa na ndio maana Katibu wa CCM wa hapa tumemsimamisha kazi atajadiliwa kwa sababu alikula rushwa kwa madiwani,” alisema Magufuli.
Uchunguzi ulitoa majibu gani? Je alikuwa bado amesimamishwa kabla ya uteuzi huu!!
 
Shaka Hamdu wewe utakuwa umepata fundisho kutoka kwa mtangulizi wako,Polepole alijitengenezea maadui kwa sababu ya maneno ya kejeli na vitisho kwa watu.
Jifunze kwa Januari Makamba na ikibidi mfanye awe rafiki yako,utavuna busara nyingi kabla hujafungua kinywa.

Nakutakia kika la kheri.
 
Ila yatima hadi mnatia huruma bado mnaota labda kuna siku baba atarudi, mlijaa viburi sana mkiongozwa na chakubanga na bashiru, ila Mungu ni fundi sana.
Kwa hiyo point yako ni nini sasa?

Lisu na chadema waekuwa Rais?
 
Kule saccos mnaanza lini kisafisha, au mzee wa faru John kashawasafisha nyote?.
Yaani kika anayemkubali Mh. Samia ni CHADEMA? Kwa taarifa yako nina kadi ya chama miaka mingi kabla hujazaliwa wewe. Na kuwa mwana CCM siyo tiketi ya kukubali kila uozo wa chama. Toka zile enzi za wizi wa EPA, ESROW na akaingia tena Dikteta sikuafikiana na upuuzi ule. Na haimaanishi kuwa kama sikubaliani na nikipinga basi ni Mpinzani.

Mimi nililelewa kwenye familia yenye maadili sana na niko makini kwenye kila kitu. Siwezi kushabikia maovu hasa uuaji wa binadamu. Kamwe hata uwe mzuri kiutendaji kakini ukikatili basi siwezi kukushabikia.

Hivyo Elewa niko home kabisa na sitegemei kuondoka home ila wakiharibu nitasema. Na msiniunganishe na Wapinzani.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu na siku zote Kweli itatuweka huru.
 
Hwa jamaa walijiona kwamba wao ndio ccm yenyewe na ambao wanaweza kufanya jambo lolote wakt wowote bila bughdha ya mtu yoyote, toka popote pale.
walifanyaje, ebu nipe matukio hata mawili tu
 
Mimi niko nyumbani sijawahi kuhama. Sema upuuzi sikuendekeza kabisa. Na sitauendekeza. Kiongozi yoyote ambaye anaenda kinyume na uTanzania wetu sitamuunga mkono. Kiongozi mkumbatia mafisadi hawezi kuwa karibu nami. Hivyo toka awamu ya 4 ya wizi Iue mkubwa basi nilichafukwa nikawa naangalia tu. Hivyo kwa sasa nina amani kuwa mambo yatabadilika hasa kwa upande wa uhuru na amani. Mambo ya majizi Tanzania ni Mzizi mgumu sana unahitaji moto mkubwa wa coal.
CCM ni ileile toka enzi ya Baba wa Taifa! Wala usiumize sana kichwa chako,hata Mama nae muda ukifika mtaanza kuona hafai na mtatamani Jiwe arudi tena!!
 
Back
Top Bottom