Shaka Hamidu Shaka, mrithi wa Polepole nafasi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM

Shaka Hamidu Shaka, mrithi wa Polepole nafasi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM

kivip, au wew ni kati ya watu uliedhulumu watu. haiwezekani watu wapate haki zao kupitia hiki kipindi alafu wew hutaki

Katika Uongozi wa Dk. Magufuli kipindi hiki cha kutatuwa kero za raia live kwa kupitia kipindi cha TV/Radio kilicho kuwa kinaongozwa na Mzalendo Polepole kipindi hiki kilikuwa na umuhimu sana kwa ustawi wa Taifa letu, ni viongozi wachache wange endeleza tabia zao za kupuuzia kutatuwa matatizo ya raia au kujingiza kwenye tabia ya kuwaonea raia bila sababu.

Tuwe wakweli hapa - kipindi hiki Polepole alikuwa anakiweza sana na alikuwa mfatiliaji mahili - who ever advised our President to replace Polepole amekosea sana, sioni aibu kulisema hilo - je, kuna baadhi ya viongozi wetu kwenye mashirika ya umma na Serikalini hawataki Kufatiliwa kwa karibu LIVE/TV kwa kupitia vyombo vya chama tawala?

Binafsi, sioni mantiki ya muzzle avenue hii ambayo ilikuwa kimbilio la kweli kwa watu WANYONGE - hakuna mbadala tusije tukajidanganya hapa, imenisikitisha sana sana.
 
you so stu-pid and lazy. hii ni point nayo unaongea. sasa kuna tatizo gani kama anatatua matatizo ya wananchi. ndio maana wakenya wanasema tuna kila kitu lakin hatuwapiti kwa maendeleo, kwa akili kama yako hatuwezi fika.
Polepole hakuwa mtendaji wa serikali au hilo hujui.
 
Tulisema kuwa huu ndiyo mwisho wa waramba miguu wa jiwe watu wakatubishia ona sasa kina Bashiru na Polepole wanatupiwa virago mchana kweupeeeeee
Siasa Hatari Sana hawa watu ndiyo basi tena
 
MATAGA chapuo yao eti ilikuwa;

KATIBU MKUU: Paul Makonda a.k.a Albert Bashite

KATIBU ITIKADI NA UENEZI: Ole Sabaya

KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA: Dotto James (Mtoto wa dada wa Mwendazake)

haa haa haa, but every thing went astray....everything is turned upside down...
 
Shaka Hamidu Shaka, ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akichukua nafasi ya Humphrey Polepole ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa.

=======

Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amemteua Shaka Hamdu Shaka kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.Shaka Hamdu Shaka ndiye Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi CCM akichukua nafasi ya Humphrey Polepole aliye teuliwa kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Aliwahi kusimamishwa kazi na Mwenyekiti wake Rais Magufuli wakati huo akiwa Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro kwa kosa la kula rushwa.

1} Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka asimamishwa kwa tuhuma za rushwa
mbona kama mtoto sio riziki
 
Ml rushwa Kumbe?/CCM wallah ni ile ile
 
Safi kabisa,nimependa chama tawala kimejipanga tena bila kunyoosheana vidole wala kufukuzana kwenye chama,Tanzania bila CCM haiwezekani.
Vyama pinzani wana chakujifunzi kutoka CCM.
 
Polepole ana shida zake nyingi tu, hafai kuendelea kubaki katika hiyo nafasi ila sio kwa kumleta Shaka... Hivi Shaka ana ushawishi gani huku bara ambapo ndio kwenye mtaji wa kura... Shaka akishawahi kuwa katibu mkuu wa uvccm nadhani je alitumia nafasi hiyo kufanya nn cha maana
Ukatibu mkuu na uenezi ni post mbili tofaut hata kimajukumu... Tumpe muda mkuu, amini kuwa hatuwezi kujua kila kitu!
 
Back
Top Bottom