Sasa hapo haki yake ni ipi zaidi ya kufukuzwa Kwa udanganyifu.
Yaani miaka yote alipwe Kwa udanganyifu halafu aje alipwe na fidia badala ya kurudisha zile alizotuibia.
Wewe huoni kuwa Nchi hii inakosa maendeleo Kwa sababu ya watu wengi kuwa na vyeti feki.
Hivi unahabari kuwa hata PhD na Masters nyingi ni za Kununua bila kufanya tafiti na wakipeleka vyeti wanaongezwa mishahara mikubwa Kwa kazi Ile Ile na ujuzi ule ule waliokua nao wenye digrii Moja au wasio hata na digrii.
Kwa Sasa watu maofisini wanashindana kutafuta PhD na Masters sio Kwa ajili ya kuweka utaalam au hata kufanya mapinduzi ya kiutendaji na kiufumbuzi Bali kuongeza mishahara wakitoka jioni wakalale kwenye mabaa na Wanawake mchezo imeisha halafu utasikia wakikuambia nasoma ili nipumzike nile mshahara mkubwa.Yaani badala ya kuongeza kazi na kusaidia jamii mtu anasema anataka apande Cheo na mshahara ili apumzike.
Hivi Kwa mfano Mwalimu wa shule ya Msingi akasoma mpaka akawa na PhD halafu akabaki kufundisha shule ya Msingi atakua na manufaa Gani ?
Tunataka mtu asome kihalali na afanye kazi zaidi na ionekena sio kuwaza mshahara na vyeo Kwa kununua tafiti za watu wengine. Hawezi hata kuzielezea.
Dereva darasa la Saba alitakiwa asome QT kama wangine.Lakini wenzake walipokua wanasoma yeye anampigia simu mtu wa baraza na kumpelekea laki Tano halafu akapewa cheti adhabu yake ni kufukuzwa na kurudisha mshahara au kufungwa.
Huoni JPM aliweka hashima mpaka Baraza hawauzi vyeti na vile vya stationary haviuziki Tena.
Tafuta cheti kafanye kazi Huko kwenye kampuni binafsi lakini sio kazi ya umma inayolipa Kwa Kodi ya watu wote na nafasi zipo Kwa ajili ya wote. Ukidanganya unatupwa nje wanapewa watanzania wengine waaminifu. Wapo wengi.