Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Nimegundua kwamba kumbe Chadema inaongoza na CCM inatawala. Kumbe Chadema ina viongozi wengi kiasi hiki nchini? Wananunuliwa hawaishi tu? Yaani kila siku kuna tunasikia kiongozi fulani wa Chadema amajiuzulu. Kwani sasa CCM ina viongozi eneo gani la nchi? Yaani kwa mkupuo mmoja na siku moja unasikia wenyeviti 20 wa vijiji na vitongoji wa Chadema wajiuzulu. Sasa mbona hawaishi? Kila anapokanyaga mzee anakutana na viongozi wa Chadema. Hii inamfanya akate tamaa ya kutawala maana walio chini yake wote ni Chadema, tena wanatawala maeneo nyeti kiuchumi. Hongera Chadema kwa kuongoza na wao kutawala. Haiwezekani kila kona ya nchi ni viongozi wa Chadema tu. Sasa CCM ilishinda wapi? Hii inaonyesha jinsi ambavyo kweli bao la mkono lilipigwa 2015. Hii nunua nunua imetufumbua macho kushuhudia jinsi Chadema ilivyoshinda maeneo Mengi nchini mwaka 2015.
 
SIACHI KUKUHUSUDU KIONGOZI WANGU ILA KWA HILI BANDIKO KIUKWELI SI LA VIWANGO VYAKO.
 
Ulikuwa role model wangu mbona hivyo tena...hata mnyama anaona sehemu salama ya kukimbilia ni nyumbani! huoni dereva alipoona anafuatiliwa akaona sehemu salama ni nyumbani kwake lissu ambako pia ni makazi ya serekali yenye ulinzi masaa.24?
 

Hili nimelizungumza sana watanzania elimu yao ni ya mashaka sana, watu hawana reasoning, hawana uwezo wa kufanya analysis. Ni elimu ya hovyo isiyojenga independent thinking. Uzi huu wa pasco niliusoma kisha nikasoma comments nikajishangaa sana, jamaa kamaliza chini kwa kuweka wazi kila kitu ila watu hawaelewi kitu.
 
Mkuu ukisema kutiliwashaka inawezekana ila kwa jinsi Kiongozi Mayalla hoja alivyozipanga naona kama zimepwaya pwaya!
 

mwenyewe hujaelewa kama wanaomtukana pasco, hebu soma para mbili za mwisho uone pasco anamaanisha nini
 
Someni vizuri hitimisho lake. Ndipo point yake ilipo. Wasiojulikana wanajulikana na ndio maana hawataki uchunguzi. Hiyo ndiyo pointi ya Paskal
 
Umasikini ni jambo baya sana...
 
Haya ni maswali ya msingi sana.
Mimi nina swali moja..

Risasi alizopigwa Lissu tokea upande
Habari zote za zilizo hadharani za mashuhuda tangu siku ya tukio na hata Lissu mwenyewe anasema washambulizi wake walikuwa upande wa kushoto.
Ni dereva tu aliyeruka na kujificha upande wa kulia.

Risasi alizopigwa Lissu tokea upade wa kulia zilirushwa na nani?
Bila kumhoji vizuri dereva wala hatutajua.
Na katika maswala ya uhalifu na uchunguzi hili swali lazima lijibiwe tena lijibiwe kwa kikamilifu.

Swali la pili ni hizo risasi (slugs) zilizotolewa huko nje ya nchi je zimefanyiwa uchunguzi (Ballistic examination and analysis) wa kitaalam kuwa ni za aina gani na zilitumiwa na bunduki ipi?

Tuache bla bla kwenye hili swala. Tunaoliangalia kwa jicho kavu tunapata mshangao na maswali kuliko majibu.
 
Mkuu pasco... hapo kwenye hitimisho unatukera sana sisi buku 7 ilhali tulianza vizuri kabisa huu uzi.
 
Mkuu Lissu alilaza kiti halafu akalalia tumbo so automatically unaelewa upande wa kulia ulipigwaje risasi.

Mnaacha kuuliza camera na walinzi wa pale home kwake walikua wapi mnakuja kuuliza mambo yasiyo na logic
 
Someni vizuri hitimisho lake. Ndipo point yake ilipo. Wasiojulikana wanajulikana na ndio maana hawataki uchunguzi. Hiyo ndiyo pointi ya Paskal
Na hao wasiojulikana kwa tukio kama hili walikuwa na mtandao wao tena mpana..
Sasa kwa nini hatutaki kupanua jicho na fikra?
 
Umesomeka
 
Mkuu Lissu alilaza kiti halafu akalalia tumbo so automatically unaelewa upande wa kulia ulipigwaje risasi.

Mnaacha kuuliza camera na walinzi wa pale home kwake walikua wapi mnakuja kuuliza mambo yasiyo na logic
Hapo ndipo utakapojua kuwa logic hailipi.
Ingekuwa hivo angepigwa risasi nyingi sana upande wa kulia ambao ndio ungelikuwa umewaelea washambulizi (waliokuwa kushoto mwa gari).
Pamoja na hivo haijibu swali la kwa nini mwili uliingiliwa na risasi shambulizi toka pande mbili tofauti. Zile bullet entry wounds za upande aliokuwepo dereva (na sio washambulizi) wazielezeeje?

Na pili swala la walinzi na kamera linaonyesha tu jinsi mtandao wa washambulizi ulivyo mpana na wenye nguvu. Tutaufuchuaje bila kujua story ya dereva..shahidi muhimu tena ambaye risasi shambulizi zimetokea upande aliokuwepo pia?
 
Mtu mwenye akili timamu na ambaye hana chembe hata kidogo ya kichaa ++ angeanza hivi;Siku hiyo walinzi walienda wapi?Je,wamechukuliwa hatua gani?Je, aliposema kuwa anafuatiliwa kwa siku za nyuma kabla ya tukio,taasisi husika ilichukuwa hatua gani?Je,ni kwanini taasisi husika ilisema kuwa haifanyi kazi kwa taarifa za mtandaoni,bali ataje kuwa alienda kuripoti kituo gani?Je,ni kwanini Lisu na wengineo wamewahi kukutwa na makosa kwa kupitia taarifa za mtandaoni?Ni kwanini dereva hajakamatwa wakati kuna sheria inayoruhusu mtu kuhojiwa na hata kukamatwa akiwa nje ya nchi yake?Acha niishie hapa kwakunukuu maneno ya aliye wahi kuwa rais wa Afrika kusini ajulikanaye kama P. Botta alisema"Mwafrika hata akisoma hawezi Acha upumbavu wake".
 
Mkuu Lissu alilaza kiti halafu akalalia tumbo so automatically unaelewa upande wa kulia ulipigwaje risasi.

Mnaacha kuuliza camera na walinzi wa pale home kwake walikua wapi mnakuja kuuliza mambo yasiyo na logic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…