Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Unajua kwanini nimekupa ushindi, nimegundua umeishiwa na hoja sasa unalazimisha tuingie kwenye ubishani. Nimekuambia bayana sio dereva tu kwenye ushahidi, bali hata Lissu anapaswa kuwa shahidi kwani yuko hai na kwenye shambulio alikuwepo. Sasa naona akili imehama umekuwa kama umekariri kwamba kila anayezungumzia hili jambo akiwa upande wa Lissu anagoma dereva kuhojiwa.
Vizur sana,nini majibu yako ktk post ya Mayala?
 
Umeelezea upande unaokufurahisha, lakini issue ya kutoka kwenye attempt ya kuuawa hasa kwa silaha inawezekana, Lissu siyo mtu wa kwanza, alishambuliwa Pope John Paul wa II tena akiwa ameangaliana na muwaji lakini akufa, sembuse lissu aliyekuwa kwenye gari? Ni Mungu tu ndiye anayepanga ufe au upone.
Naye alipigwa risasi 38 na Dereva wake alijificha chini ya uvungu wa gari?
 
Anayedhania wanaomdhania dereva wako sahihi naye yuko sahihi,hii ni kwakuwa wanaotakiwa kuwatambua wasiojulikana wameshindwa kuwatambua ama kwa bahati mbaya ama kwa maksudi
 
Si lisu aliwaambia police wa Tanzania hawawezi kumhoji huko Kenya?Au mmesahau?

..aliwaelekeza UTARATIBU wa kufuata ili kupata USHAHIDI wake.

..utaratibu huo umebainishwa ktk sheria iliyotungwa na BUNGE letu.

..hivi ingekuwa ni Mbunge wa CCM ameshambuliwa serekali angetenda hivi inavyotenda kwa Mh.Lissu?
 
Huu ni wakati wa teknologia hamna haja ya ku-speculate kuhusu yaliyotokea kuhusiana na mashambulizi ya TL. Leta Scotland au CIA wafanye uchunguzi. Dakika sifori tu wasiojulikana watajulikana tu. Lakini naona ganzi mkiambiwa tuwalete wataalam wa uchunguzi toka nchi zenye ujuzi na teknlogia ya kisasa. Mnaogopa nini? Kuumbuka?
 
Si lisu aliwaambia police wa Tanzania hawawezi kumhoji huko Kenya?Au mmesahau?

..huo siyo uamuzi wa Tundu Lissu.

..alichosema ndivyo sheria inavyoelekeza.

..lengo la kumhoji ni kupata MAELEZO / USHAHIDI wake.

..Je, Polisi waliwahi kujaribu kufuata huo utaratibu kama ulivyoelekezwa na sheria zetu halafu Mh.Tundu Lissu akakataa kuwapa ushirikiano?

..Mimi naona kunatafutwa kila aina ya "VIJISABABU" ilimradi tu Polisi wasifanye uchunguzi.

..@MISULI, hebu jiweke ktk nafasi ya Mh.Lissu. How would you feel kutendewa namna ile?

..How would you feel watu wangekuzushia uongo kama wewe unavyofanya hapa JF.

..Nakusihi ndugu kuwa na UTU ktk jambo hili.
 
Paskali tujibie maswali ya lissu:-
1.Pale kuna ulinzi masaa 24 lakini siku ya tukio kulikuwa hakuna ulinzi,nani alioamuru ulinzi uondoke kwa siku hiyo?
2.CCTV nani kaziondoa kwenye nyumba zilizokuwa karibu na eneo la tukio?
 
Mzee paskali kwenye bunduki majeshi yetu yanatumia sana Ak47
 
1. Tuchukulie kwamba dereva wa Lissu alihusika katika jaribio hilo la mauaji; je alishindwaje kummalizia bosi wake hata kwa kumziba pumzi tu alipokuwa "half dead" kwa kuchakazwa na risasi za wauaji wenzake badala yake akawa mstari wa mbele katika kuokoa uhai wa majeruhi? Kwa maana kama angekufa kabisa bado ingeonekana aliuawa kwa risasi?

2. Lakini mbali na wakati, kabla na baada ya tukio la jaribio la mauaji, dereva dereva yupo pale ambapo bosi wake alipo. Na ikiwa watu "wanaomuwezesha" dereva huyo kukwepa kuhojiwa na vyombo vya usalama na kuishia kumuweka pamoja na mlengwa wa mauaji yao hadi huko ulaya ndio hao hao waliomtumia dereva huyo katika jaribio lilifeli; iweje sasa washindwe kutumiza azma yao ya kummaliza hata kwa sumu wakati wana "free access" na "windo" lao? Je, wameamua kuachana na mpango wao wakumuua Lissu au wamesitisha kwa muda tu?

3. Kama ni kweli wadunguaji wa Lissu ni "wahuni tu" na sio "trained/professional gunmen" na kwahiyo "waliishia kulenga makalio" ya mlenga wao; je dereva wa Lissu nae tumchukulieje; "professional", "jasiri" au "fala" hata athubutu kujiweka pamoja na muhanga ambako risasi zilielekezwa yaani "the side of highest risk" wakati akijuwa kuwa wazi kuwa wadunguaji si "mafundi" wa kulenga na huenda naye angeathirika?

4. Ikiwa dereva alihusika, je kwanini alimjulisha bosi wake kabla ya "mvua ya risasi" kwamba alihisi gari ya nyuma yao ilikuwa inawawinda kwa namna alivyoiona kwenye driving mirrors na hata wakashauriana wasishuke garini kwa usalama wao?
 
Walipohisi kuna gari linawafuata na hawalielewi dereva alitakiwa aelekeze gari cha úsalama sasa kwann dereva aliendelea kupeleka gari nyumbani mahali pasipo na usalama? Hapo kuna masuala ya kujiuliza
 
Vizur sana,nini majibu yako ktk post ya Mayala?

Humu kwenye huu uzi tuko page ya 30+, yamehojiwa, kujibiwa mengi, kubeza na hata kusifia. Paskali mwenyewe mwenye uzi hajatokea kujibu concerns za watu wala kuchangia lolote. Sasa kama mwenye uzi ana maswali zaidi ya 10 lakini hajigusi kuongea chochote, mimi ni nani? Mimi huwa napenda kujikita kwenye mjadala wenye hoja, sio mjadala wa ubishani ili kutafuta ushindi.
 
..aliwaelekeza UTARATIBU wa kufuata ili kupata USHAHIDI wake.

..utaratibu huo umebainishwa ktk sheria iliyotungwa na BUNGE letu.

..hivi ingekuwa ni Mbunge wa CCM ameshambuliwa serekali angetenda hivi inavyotenda kwa Mh.Lissu?
Kwani aliyetakiwa kueleza utaratibu umekiukwa ni Serikali ya Kenya kupitia ubalozi wetu au lisu mwenyewe?Huku juu nimeeleza jinsi gani ujuaji wake unavyotia shaka ktk kupata haki yake.Sikuona umuhim wa lisu kuanza kutoa maelekezo kwa serikali nini wafanye coz hata serikali isingeweza enda kumhoji bila baraka za serikali ya Kenya.Ni maajabu sana mgonjwa kuwa mjuaji kuliko wanaotaka kumtibu kiasi kupanga dozi ipi apewe kwa utaratibu upi na vipi achomwe sindano
 
..huo siyo uamuzi wa Tundu Lissu.

..alichosema ndivyo sheria inavyoelekeza.

..lengo la kumhoji ni kupata MAELEZO / USHAHIDI wake.

..Je, Polisi waliwahi kujaribu kufuata huo utaratibu kama ulivyoelekezwa na sheria zetu halafu Mh.Tundu Lissu akakataa kuwapa ushirikiano?

..Mimi naona kunatafutwa kila aina ya "VIJISABABU" ilimradi tu Polisi wasifanye uchunguzi.

..@MISULI, hebu jiweke ktk nafasi ya Mh.Lissu. How would you feel kutendewa namna ile?

..How would you feel watu wangekuzushia uongo kama wewe unavyofanya hapa JF.

..Nakusihi ndugu kuwa na UTU ktk jambo hili.
Kwa akili yako unafikiri polisi Tz wangeenda moja kwa moja hospital kumhoji lisu bila taratibu zozote za kidiplomacy kufuatwa?Yani lisu ndiye anajua taratibu kuliko maafisa wote wa Tanzania na huko Kenya?Sikuona serikal ya Kenya ikitoa maelekezo yyt kuhusu yy.Mimi sipo Tz lkn naamini serikali ya Tanzania haiwezi kuja kunikamata hapa bila taratibu zozote za kidimplomacy kufanyika,ni kitu simple na kinaeleweka.Mwambieni huyo jamaa yenu apunguze ujuaji.
 
Kwani aliyetakiwa kueleza utaratibu umekiukwa ni Serikali ya Kenya kupitia ubalozi wetu au lisu mwenyewe?Huku juu nimeeleza jinsi gani ujuaji wake unavyotia shaka ktk kupata haki yake.Sikuona umuhim wa lisu kuanza kutoa maelekezo kwa serikali nini wafanye coz hata serikali isingeweza enda kumhoji bila baraka za serikali ya Kenya.Ni maajabu sana mgonjwa kuwa mjuaji kuliko wanaotaka kumtibu kiasi kupanga dozi ipi apewe kwa utaratibu upi na vipi achomwe sindano
Nafikiri hata wale uliopewa uwasaidie kufikiri wataanza kuelewa kuwa we lazima umehusika kwa namna moja au nyingine ktk risasi 38. Tunaofikiri bila msaada wa low iq kichaa jiwe na genge lake tunaelewa hizi comments zako ni sehemu ya kazi upate ridhiki na watoto wale, so hakuna lawama endelea pambana
 
Ndio shida yenu.Yani kila anayewakosoa ni anataka uteuzi.So unataka kusema wote tuimbe wimbo mmoja?
 
Back
Top Bottom