Malalamiko ya Fatma hayahusiani na tamko lolote la Lema. Fatma amekasirika kwa nini wakina Martin wamehoji kauli ya Bashe kuwa sukari itapatikana kabla ya mwezi wa Ramadhani. Yeye akaona kuwa Bashe anahojiwa kwa sababu ni muislamu na kuwa ni uthibitisho kuwa CDM hawafurahii jambo lolote linalowafaidisha waislamu. Anacho sahau ( kwa makusudi) ni kuwa Martin si msemaji wa CDM. Na alichouliza kimetokana na Bashe kuingiza suala la Ramadhani katika juhudi za kuondoa uhaba wa sukari. Kuna waliosema mbona waziri wa nishati aliyekuwa mkristo aliwahi kuwaagiza Tanesco wasikate umeme siku ya Krismasi na hamna ambae alilalamika. Mimi sidhani kama mtu unaweza kulinganisha nafuu ya siku moja na hii ya kuondoa kabisa kero iliyoendelea kwa muda mrefu. Waziri aliteleza. Angesema tu sukari itapatikana ndani ya wiki moja bila kuingiza suala mfungo wa dini moja. Kwa kusema hivyo kunakaribisha maswali kuwa kama ni rahisi hivyo kwa nini hakuhakikisha sukari inapatikana wakati wa Kwaresima? Ni tatizo la kujitakia na Fatma should know better kuliko kuongeza kuni kwenye suala la udini.
Amandla...