Sheikh Muharam Mziwanda adai Kanisa Katoliki linahusika na upotevu wa makontena Bandari ya Dar

Sheikh Muharam Mziwanda adai Kanisa Katoliki linahusika na upotevu wa makontena Bandari ya Dar

Naunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikali hasa kupitia mkataba huu wa bandari. Lkn kupitia matamko haya ya yasiyoeleweka yanayoanza kutolewa kwa kujibidhana na Tec bila kuwa na majibu ya hoja walizotoa hii sio sawa... Hao mashekh hawakutakiwa kuwajibu tec, maana tec hawajawashutumu mashekh, ila wametoa maoni yao kwa serikali baada ya kuuchambua mkataba.

Vivyo hivyo mashekh walitakiwa wauchambue mkataba waje na maoni yao kwa serikali na sio kuwajadili maaskofu tena kwa kushindwa kutoa majibu fasaha kwa waraka wao. Kwenye hili iko wazi mashekh wanataka malumbano na maaskofu. Je! Hivi kwa akili ya kawaida tujiulize Hao Maaskofu walivyo na Maakili makubwa zinazoongozwa na Hekima pamoja na Maarifa watakuwa na muda wa hata kuwaongeresha hao mashekh kweli!???? ... Hapo inaonekana dhahiri kuwa maaskofu wa tec ni akili kubwa tofauti na hao walopokaji wengine...
 
Na hawa wakiongea hovyo hivi Serikali wala haioni wala kusema kitu. Na hawa hawawezi kuongea bila ya kuambiwa. Wao ndio wanazidisha moto uliopo wa udini. Badala ya kujibu ya mkataba wa bandari au waraka, wao wako kwenye Uarabu vs Uislam. Hii nchi imekuwa ya hovyo sana kwa awamu hii. Uswahili uswahili mwingi.
 
Binafsi ni muislamu lakini hiki kinachofanyika nikujidhalilisha tu..

Tunaonekana kituko kila mtu akishiba na kuvimbiwa ubwabwa basi anatafuta kipaza sauti.
 
Tujifunze tusikiliza na tusivyovipenda, serikali imekubali kupokea maoni ya makundi mbalimbali na watu binafsi kuhusu hili suala. TEC wametoa yao na wengine waacheni watoe yao. Haina haja ya dhihaka hakuna mwenye hati miliki ya kutoa maoni na asikilizwe peke yake.
 
Hawa mashekh mbona wanajidhalilisha kiasi hiki? Ina maana Hawa ndio think tank ya waislamu? Kazi ipo
 
kudadavua nani kaleta hoja hiyo. Niko kny Magroup& vikundi vya kijamii kadhaa vyenye Waislamu & Wakristo na wale wazee wa Dini za asili, na kote huko wote wanasema wanaungana na Waraka wa Maaskofu, tena Waislamu ndo wanarukaruka kwa furaha kabisaa wakisema TEC sio mnafiki, TEC imesimama na Maslahi ya nchi! Wanasema Waraka wa Maaskofu ndo tumaini pekee maana umebeba 'jambo letu wote'. Sisi watanzania tukubali tu sindano iingie, tuupokee ukweli na kama kujibu waraka tuujibu kwa hoja na sio kuanza ku-panic kwamba kasema nani, waraka kaandika nani!

Kwa taarifa yenu hata ingetokea TEC ikakalishwa 'meza maalum' na ikafanya 'handshake' na Serikali na ikafuta tamko, sisi watanzania hatutorudi nyuma, tutaendelea kuukataa Mkataba hivyo tutakomaa na maslahi ya nchi mpaka kieleweke. Mkataba ni haufai, haufai, regardless kasema nani, ilimradi katoa hoja kuonesha kwamba haufai. Full stop! Mnaoishambulia TEC jifunzeni kuupokea UKWELI na kuufanyia kazi. Na imekuwa kasumba yenu badala ya kuupokea ukweli mnajipofusha kwa kumshambulia msemaji. Job Ndugai hakuwa Askofu wala si Mkatoliki lakini alipowaambieni ukweli mkakimbilia kumng'oa kny Kiti chake, jambo ambalo kimsingi yalikuwa ni MAPINDUZI dhidi ya Muhimili mmojawapo, na Mapinduzi ni Uhaini wala hamkuwa na Haki ya kumng'oa. Badala yake mkamuweka Spika ambaye ni kituko asiyetambua maana ya Muhimili anaouongoza. Mnawakosea sana wananchi, ambao MAMLAKA YOOOTE INATOKA KWAO. Mnaliaibisha Taifa ambalo limejijengea Heshima kubwa sana nchini. Acheni mihemko
 
Jambo lishageuzwa kuwa la kidini tayari...umoja na udugu wetu ni bandia tu kina Nyerere walijifariji wametengeneza taifa, kumbe kilichotengenezwa ni unafiki mtupu wa kusubiriana kwenye angle ili kusutana na hili litafika mbali, moto ulianza kama cheche...watu wamekusanya chuki nyingi kwenye mioyo Yao Kwa miaka mingi naona kabisa mbeleni ngoma itapasuka, Kila jambo kubwa nchi hii lazima lihusishwe na dini hii inaonyesha namna udugu bandia tuliokuwa nao, mpasuko ni mkubwa na hakuna wa kuuziba. Jambo baya lituepuke mbali.
 
Dini ambayo haina hoja ila sababu aliyesaini ni wa dini yao, baadhi wanaona wanaonewa. Huu mkataba una nini cha kuamua kufa nao? Hatuoni unatugawa?
 
Jambo lishageuzwa kuwa la kidini tayari...umoja na udugu wetu ni bandia tu kina Nyerere walijifariji wametengeneza taifa, kumbe kilichotengenezwa ni unafiki mtupu wa kusubiriana kwenye angle ili kusutana na hili litafika mbali, moto ulianza kama cheche...watu wamekusanya chuki nyingi kwenye mioyo Yao Kwa miaka mingi naona kabisa mbeleni ngoma itapasuka, Kila jambo kubwa nchi hii lazima lihusishwe na dini hii inaonyesha namna udugu bandia tuliokuwa nao, mpasuko ni mkubwa na hakuna wa kuuziba. Jambo baya lituepuke mbali.

hata familia ya mume mwenye wake wengi,akikosa uimara ndipo mambo ya kupigana wake,watoto na hata kuleteana dharau huanza.

hapa ni ishara tu kwamba kiongozi tuliye naye sio thabiti.

maslahi mapana ya kitaifa,yanatetewa na watu kama mwijaku kweli!!!
 
Ninachoona ni kuwa waheshimiwa wengi hawajalala usingizi tokea TEC watoe waraka ule.

Wanajaribu kusoma mstari kwa mstari ili watoe majibu, dalili kubwa ni kwamba wamekwama.

Ushauri tu ni kuwa tekelezeni ya kwenye waraka wa TEC wasije wakaja na mengine magumu zaidi.
Waraka mgumu ule, kwani nukuu zilizomo ni za Katiba, Biblia, Sheria za Nchi, na historia ya makosa ya serikali ya 1990s na kunyolewa kwenye mahakama za kimataifa za biashara!!
 
Waraka wa TEC haujashambulia dini yeyote.Umetoa hoja zake na wameambatanisha vifungu mbalimbali.Shekh unadhalilisha upeo wako
 
Ninachoona ni kuwa waheshimiwa wengi hawajalala usingizi tokea TEC watoe waraka ule.

Wanajaribu kusoma mstari kwa mstari ili watoe majibu, dalili kubwa ni kwamba wamekwama.

Ushauri tu ni kuwa tekelezeni ya kwenye waraka wa TEC wasije wakaja na mengine magumu zaidi.
Nashindwa kupata picha ya mbunge wangu Musukuma
 
Back
Top Bottom