kudadavua nani kaleta hoja hiyo. Niko kny Magroup& vikundi vya kijamii kadhaa vyenye Waislamu & Wakristo na wale wazee wa Dini za asili, na kote huko wote wanasema wanaungana na Waraka wa Maaskofu, tena Waislamu ndo wanarukaruka kwa furaha kabisaa wakisema TEC sio mnafiki, TEC imesimama na Maslahi ya nchi! Wanasema Waraka wa Maaskofu ndo tumaini pekee maana umebeba 'jambo letu wote'. Sisi watanzania tukubali tu sindano iingie, tuupokee ukweli na kama kujibu waraka tuujibu kwa hoja na sio kuanza ku-panic kwamba kasema nani, waraka kaandika nani!
Kwa taarifa yenu hata ingetokea TEC ikakalishwa 'meza maalum' na ikafanya 'handshake' na Serikali na ikafuta tamko, sisi watanzania hatutorudi nyuma, tutaendelea kuukataa Mkataba hivyo tutakomaa na maslahi ya nchi mpaka kieleweke. Mkataba ni haufai, haufai, regardless kasema nani, ilimradi katoa hoja kuonesha kwamba haufai. Full stop! Mnaoishambulia TEC jifunzeni kuupokea UKWELI na kuufanyia kazi. Na imekuwa kasumba yenu badala ya kuupokea ukweli mnajipofusha kwa kumshambulia msemaji. Job Ndugai hakuwa Askofu wala si Mkatoliki lakini alipowaambieni ukweli mkakimbilia kumng'oa kny Kiti chake, jambo ambalo kimsingi yalikuwa ni MAPINDUZI dhidi ya Muhimili mmojawapo, na Mapinduzi ni Uhaini wala hamkuwa na Haki ya kumng'oa. Badala yake mkamuweka Spika ambaye ni kituko asiyetambua maana ya Muhimili anaouongoza. Mnawakosea sana wananchi, ambao MAMLAKA YOOOTE INATOKA KWAO. Mnaliaibisha Taifa ambalo limejijengea Heshima kubwa sana nchini. Acheni mihemko