Sheikh wa Mkoa Mwanza (Kuhusu Mjadala wa Bandari): Walaaniwe wote wenye nia ovu na Rais Samia


Na wewe una msimamo gani kuhusu hii issue ya bandari? Maana kama udini, Profesa Issa Shivji toka lini amekuwa mkristu na amepinga hadharani vipengele vya makubaliano hayo?
Hivi wakristu sio watanzania? Kwanini wasisimame na kupinga kitu ambacho hakiko sawa?
Mtu anayekimbilia udini mara nyingi huwa hana hoja, hana maono mapana, na ni mbabaishaji.
Dini gani wanayoisema hapa kwenye suala la bandari?
 

Na wengine wanaosema wamesoma wanalibeba kama lilivyo na kulipigia debe🤣🤣🤣🤣
 
Ile vita yake ya maneno na mwaipopo iliishia wapi?
 
Haya maswali magumu sana sidhani kama atakujibu. Sidhani kama bila hicho chama walichoasisi babu zake Tanganyika isingepata uhuru.
Cpt,
Ukiona nimemkalia mtu kimya simjibu si kuwa sina jibu.
Huo ukimya ndilo jibu lake.
 
Funga mwenyewe
 
Shida sio waarabu wawekezaji, shida ni muda wa ukomo
 
"Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini ya kikristo kumkejeli Rais Samia."

Ni Rais yupi ajwahi tukanwa or kejeliwa akiwa madarakani? Nyie ndio wadini kutaza swala hili kidini.
 
Sasa hapo umekiri mwenyewe kuwa michango ya dr vedasto, lawi sijaona,john rupia, denis phombeah imefutwa na chakushangaza hawakuwa waislamu,sasa unasemaje kuwa historia ilifutwa kisa waislamu?
 
"Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini ya kikristo kumkejeli Rais Samia."

Ni Rais yupi ajwahi tukanwa or kejeliwa akiwa madarakani? Nyie ndio wadini kutaza swala hili kidini.
Zakaria kakobe,severin niwemugizi,na yule anaesema mwanakondoo ameshinda tumfuate hawa wote walimkabili mkristo mwenzao magufuli
 
Sasa hapo umekiri mwenyewe kuwa michango ya dr vedasto, lawi sijaona,john rupia, denis phombeah imefutwa na chakushangaza hawakuwa waislamu,sasa unasemaje kuwa historia ilifutwa kisa waislamu?
Mna...
Mchango wa Denis Phombeah akiwa Meneja wa Ukumbi wa Arnautoglo 1952 huwezi kuufananisha na mchango wa babu zangu walioanza harakati hizi kwa kuunda African Association 1929 na kujenga ofisi ya AA kati ya 1929 na 1933.

Vedasto Kyaruzi kaingia katika uongozi wa TAA 1950 kama Rais na Abdul Sykes Katibu.

Aliyesimama kidete kuhakikisha kuwa uongozi wa wazee Thomas Plantan Rais na Clement Mohamed Mtamila Katibu unatoka madarakani na vijana wadogo Dr. Kyaruzi na Abdul wanachukua uongozi wa TAA alikuwa Schneider Abdillah Plantan mdogo wake Thomas Plantan.

Huyu Schneider Plantan alikuwa mwandishi wa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir katika taasisi aliyeunda Mufti - Daawat Islamiyya (Wito kwa Waislam).

Hawa ni watoto wa Affande Plantan aliyekuwa mkuu wa Germany Constabulary na aliingia Germany Ostafrika na Hermann von Wissman mwishoni mwa mwaka miaka ya 1800.

Affande Plantan akijulikana kwa jina la Chief Mohosh Shangaan alikuwa kiongozi wa jeshi la mamluki wa KIzulu waliletwa na Wajerumani kuja kupigana na Bushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa.

Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa miaka hiyo.


Ufunguzi wa ofisi ya African Association 1933​
 
Huyo sheikh fala kweli, hao ndio nasheikh wapuuzi

Yaani yeye atuamrishe waislamu tufunge na tukunuti kisa mambo ya siasa??

Ndio maana sinaga muda wa kuwasikiliza masheikh wa BAKWATA
 
Kwahiyo mchango wa nyerere na bibi titi upi ni mkubwa ?
 
Kwahiyo mchango wa nyerere na bibi titi upi ni mkubwa ?
Mna...
Mwalimu Nyerere mchango wake ni mkubwa sana.
Yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa mapambano ya kudai uhuru.

Bi. Titi alikuw ubavuni kwa Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru lakini huwezi kusema kuwa mchango wa Bi. Titi ni mkubwa kupita Mwalimu Nyerere.


Bi. Titi Mohamed na Julius Nyerere wakihutubia katika mkutano wa TANU Viwanja Vya Jangwani​
 
Zakaria kakobe,severin niwemugizi,na yule anaesema mwanakondoo ameshinda tumfuate hawa wote walimkabili mkristo mwenzao magufuli
Viongozi wengi wa kikristo walimshambulia Magufuli. Sasa kama ukitaka kila kiongozi wa dini flani lazima amshambulie huo utakuwa utaahira. Watu wanashambulia or kukosoa kufuatana na sababu za msingi walizo nazo wao na sio lazima ziwe za msingi kwa kila mtu na huu ndio msingi mkubwa wa uhru wa kutoa maoni.
 
Pamoja na kuandika gazeti Hapa hakuna hoja ya maana zaidi ya kukingia kifua UISLAMU.
 
Tunatambua uhuru au mapambano yeyote hauwezi kuwa peke yako lazima uwe na wenzio... mfano kwenye soka leo dunia inaamini messi ndie mchezaji bora kuwahi kutokea ila je akicheza pekeyake?
 
Samia tena sio Tanzania ?

Nilidhani tunaiombea Tanzania sasa kila ambaye akiwa na nia ovu (ovu ni subjective) alaaniwa huoni kama Samia atafanya Samia anachotaka wakati anachotaka sio necessarily kina manufaa.... Huyu badala ya kuzima moto anaendeleza kutibua tu....

Mbona watu walivyokuja juu kwamba Bagamoyo inataka kuuziwa wachina watu hawakusema kwamba ni ubaguzi; au waarabu ni Tusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…