Sheikh wa Mkoa Mwanza (Kuhusu Mjadala wa Bandari): Walaaniwe wote wenye nia ovu na Rais Samia


Taja hayo mashirika ambayo hayakuvunjwa.
 
Taja hayo mashirika ambayo hayakuvunjwa.
Jiwe...
''Waingereza walipoja kuitawala Tanganyika (kama Tanzania inavyojulikana) baada ya kuondoka Wajerumani baada ya Vita Kuu ya Kwanza, Wajerumani walikuwa wameshafanya kazi ya kutosha ya kuiweka Tanganyika ndani ya mamlaka mbalimbali za Kikristo.

Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika mamlaka mbalimbali za Kikristo kutoka nchi tofauti za Ulaya.
Kanisa Katoliki ambalo ndilo lenye nguvu zaidi, lilikuwa tayari limeshajikita Tanganyika.

White Fathers walikuwa wapo Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers walikuwa Morogoro na Kilimanjaro; Benedictine Fathers walikwepo Peramiho na Ndanda; Capuchin Fathers walikuwepo Dar es Salaam; Consolata Fathers walikuwepo Iringa na Meru; Passionist Fathers walikuwa Dodoma; Pallotine Fathers walikuwa Mbulu; Maryknoll Fathers walikuwapo Musoma; na Rosmillian Fathers walikuwa Iringa.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Haya mashirika yapo mpaka leo.
 
Mbona kama sheikh kazua taharuki mpya...
 

Hayo ni mashirika ya kitume,je yalikua chini ya east africa association ya kipindi hicho kabla ya kuvunjika?
 
Dhehebu la dini liitabaki moja tu halijihusishi na huu ujinga.
Haya asome na wafunge na kulaani

1. Ikitokea hakuna chochote kimewatokea waliopinga tuamini dini hiyo haabudiwi Mola ila ibilisi?

2. Je kama anaowatetea wana makosa wamefanya hata ya kibinadamu na mkataba huo ukahitaji marekebisho madogo. Laana zimuendee nani?

3. Ikitokea hakuna Laana upande wowote si wapingaji wala wapingwaji ibada yake itasimama upande upi?

ANGALIZO: Watu wa dini wajikite na mambo ya ibada sio siasa wala hatakati maana ndani ya waumini wao hayo makundi wanayo kama wafuasi, hao anawachochea kufunga ajue wengine ni wanasiasa wengine hawakubaliani na Mkataba huo.
Afundishe maadili mema haya matatizo na usiri wa kila jambo, ubabe wa madaraka, vurugu na matukano ni dalili ya ukosefu wa Maadili mema kwa waumini wake.
 
Hayo ni mashirika ya kitume,je yalikua chini ya east africa association ya kipindi hicho kabla ya kuvunjika?
Jiwe...
Sijakuelewa...
Hii East Africa Association unakusudia nini?

Hayo niliyoweka ni mashirika ya Kanisa Katoliki yaliyoko Tanzania.
 
Hawa masheikh wanaambiwa wasome na wapeleke watoto wao shule, kazi kucheza bao na draft tu..

Haya atuambie, nikiongozi gani wa dini au wa siasa alihusisha badbari na uislam ??
 
Umenichekesha sana mzee wangu.White fathers,Benedictine fathers,capuchin fathers si mashirika kama EAMWS.Those are religious congregations na wala hayajasajiliwa kama NGOs yanaoperate kwa mwamvuli wa kanisa katoliki
 
Suala la udini lipo na jana Slaa kaongea mambo ya uvatican na hichi kikundi cha SAUTI YA WA TANZANIA haya kaongea mwenyewe. Huyu mzee na wenzake kuwashika kuwabana mapumbu mpaka wawataje wote wanaofadhili hichi kikundi, Yeye mwenyewe kasema wanafadhiliwa na kikundi hichi hata mkutano wa tarehe 22 ni hawa. Sasa hapa ndio pakuanzia.
 
Leo ndiyo nimejua kumbe ww ni debe tupu. Hayo mashurika yamesajikiwa wapi? Ushawahi kuona ofisi ya White father. Nikusaidie hayo ni mashirik chini ya RC ni sehemu ya kanisa. Na ndiyo kanisa lenyewe
 
Leo ndiyo nimejua kumbe ww ni debe tupu. Hayo mashurika yamesajikiwa wapi? Ushawahi kuona ofisi ya White father. Nikusaidie hayo ni mashirik chini ya RC ni sehemu ya kanisa. Na ndiyo kanisa lenyewe
Nyan...
Wala hapakuwa na haja ya kunitukana ungeweza kunijibu kwa adabu.

White Fathers ni sehemu ya Kanisa Katoliki lakini unaijua historia na madhumuni yake na wapi ilipotokea?

Mimi nikikaribishwa kwa mazungumzo na Peter Smith ofisini kwake White Fathers, Attman House.

Isome historia ya White Fathers.
 
Asante kwa kukubali kuwa hayo mashirika ni sehemu ya kanisa, ni kama jumuia TU. Na ndiyo kanisa lenyewe.

Ok. Sorry kwa kukutukana.
Pia siitwi Nyan naitwa Nyabhera.
 
Umenichekesha sana mzee wangu.White fathers,Benedictine fathers,capuchin fathers si mashirika kama EAMWS.Those are religious congregations na wala hayajasajiliwa kama NGOs yanaoperate kwa mwamvuli wa kanisa katoliki
Nanta...
Nimeandika kuhusu White Fathers #115.

Swali langu ni hili: mashirika haya yametokea nchi gani na nani wanayafadhili na kuyaendesha?
 
Nanta...
Nimeandika kuhusu White Fathers #115.

Swali langu ni hili: mashirika haya yametokea nchi gani na nani wanayafadhili na kuyaendesha?
Mashirika haya yanafadhiliwa na sadaka za waumini na mission zao ni kuhudumia jamii kiroho na kimwili
 
Asante kwa kukubali kuwa hayo mashirika ni sehemu ya kanisa, ni kama jumuia TU. Na ndiyo kanisa lenyewe.

Ok. Sorry kwa kukutukana.
Pia siitwi Nyan naitwa Nyabhera.
Nyabhera,
Samahani kwa kukosea jina lako na kuondoa shida hii nitaliandika kwa kirefu siku zote.
Wewe unaweza kuwa na tafsiri yako ya suala hili ambayo iko kinyume na yangu.

Mimi nina paper nzima nimeandika nakuwekea hapo chini kipande:

''Wamisionari hawa walipotia mguu pwani ya Afrika ya Mashariki, nia yao hasa ilikuwa kuufuta Uislam.

Wakazi wa pwani hii iliyokuwa ikijulikana kama Zanj waliuona Ukrsto kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1498 Wareno walipofika sehemu hizo.

Mwaka 1567 wamishionari wa Augustinian waliingia Afrika ya Mashariki kupambana na Uislam ili Ukristo uwe dini ya dunia nzima.

Kadinali Lavigirie alianzisha The White Fathers, taasisi ya Kanisa Katoliki kwa kusudi maalum la kuupiga vita Uislam Wakati huo huo Church Missionary Society (CMS) ilikuwa imejitwisha kazi ya kuondoa ulimwengu kutokana na Uislam, ujinga na giza.

Hadi hii leo White Fathers wapo Tanzania wapo Tanzania wakiendelea kufanya kazi iliyowaleta Tanganyika zaidi ya miaka mia iliyopita.

Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.''

Wamishionari wamekuja kuwastaarabisha watu Pwani ya Afrika ya Mashariki wakawakuta watu tayari wamestaarabika kwa miaka mingi sana.

Hili halikuwafurahisha.

 
Ni lengo la Ukristo kuhubiri na kuwafanya mataifa wote kuwa Wakristo. Hilo si lengo la RC ama white father TU. Hiyo ndiyo mission ya Yesu kwa wanafunzi wake ya mwisho.

Katika kuhubiri na kubatiza huwalenga wote wasiolijua neno la Kristo wawe Wapangani, Budda ama Islamu.

Na hapo sioni kosa kwa kuwa katika kuinjilisha haijawahi kutumia mtutu wa bunduki ni kwa neno na utu TU.

Na naamini pia ni lengo la uslamu kuufanya ulimwengu mzima kuwa waislamu.

Hapa ushinda umekuwepo ila Dunia inataka ushindani uzingatie haki za binaadamu. Basi.
 
Sheakh Kabeke ninamfahamu huyu mha sijui mmanyema. Form four alifika lini.
Nyabhera,

Majivuno si uungwana.
Wewe kabila gani?

Uliitaka hiyo kabila yako?
Umejikuta umezaliwa na baba wa kabila hilo hukumchagua.

Kuwa Muha ni kosa?
Kwani kufika kidato cha nne ni kitu maalum?

Mbona unakuwa hivi ndugu yangu?
Watu wote tumeumbwa na Mungu na yeye ndiye aliyetuchagulia makabila na mataifa yetu.
 
Kabila husaidia kubaini aina ya makuzi aloyopitia mtu. Pia urithi wa kitamaduni katika kuchambua saikolojia ya mtu

Hivyo hapo nimekusudia kumuonesha Sheakh Kebeke hoja zake utamaduni wake na elimu yake.

Kutaja Umanyema wake inamaana kunasabisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…