jsdkjadsdgs kasdudud ghaSJAHSJAKJas jASGasgaSJa, hapo ukisema hujaelewa rudi shule mzee.Acha wenge mdogo wangu. Upo nyuma ya keyboard hakuna anaekujua. Embu shusha nondo mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
jsdkjadsdgs kasdudud ghaSJAHSJAKJas jASGasgaSJa, hapo ukisema hujaelewa rudi shule mzee.Acha wenge mdogo wangu. Upo nyuma ya keyboard hakuna anaekujua. Embu shusha nondo mkuu.
jsdkjadsdgs kasdudud ghaSJAHSJAKJas jASGasgaSJa, hapo ukisema hujaelewa rudi shule mzee.
White fathers walikuja kueneza injili na si vinginevyoUjamaa...
Hayo maneno ni ya White Fathers soma historia yao.
Nimeipenda hiyo holly ghost father's nataman ungeielezea kiundanJiwe...
''Waingereza walipoja kuitawala Tanganyika (kama Tanzania inavyojulikana) baada ya kuondoka Wajerumani baada ya Vita Kuu ya Kwanza, Wajerumani walikuwa wameshafanya kazi ya kutosha ya kuiweka Tanganyika ndani ya mamlaka mbalimbali za Kikristo.
Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika mamlaka mbalimbali za Kikristo kutoka nchi tofauti za Ulaya.
Kanisa Katoliki ambalo ndilo lenye nguvu zaidi, lilikuwa tayari limeshajikita Tanganyika.
White Fathers walikuwa wapo Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers walikuwa Morogoro na Kilimanjaro; Benedictine Fathers walikwepo Peramiho na Ndanda; Capuchin Fathers walikuwepo Dar es Salaam; Consolata Fathers walikuwepo Iringa na Meru; Passionist Fathers walikuwa Dodoma; Pallotine Fathers walikuwa Mbulu; Maryknoll Fathers walikuwapo Musoma; na Rosmillian Fathers walikuwa Iringa.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Haya mashirika yapo mpaka leo.
Holly ghost father's ni kanisa la kitume???Hayo ni mashirika ya kitume,je yalikua chini ya east africa association ya kipindi hicho kabla ya kuvunjika?
Nanta...White fathers walikuja kueneza injili na si vinginevyo
Muuza Viatu ,Nimeipenda hiyo holly ghost father's nataman ungeielezea kiundan
Mchawi lughaMuuza Viatu ,
Ingia Google.
Utawasima.
Holly ghost father's ni kanisa la kitume???
Kwa nin wamechagua jina lenye maana mbaya au nimeshindwa kutafsir kiusahih
Nanta...
Ni kweli usemayo lakini ukisoma historia yao muasisi wa White Fathers anasema madhumuni ya kuja Afrika ni kueneza Injili na kuitoa Afrika gizani.
Anazungumza kuhusu, "Dark Continent."
Soma historia ya White Fathers utaongeza maarifa yako.
Huu sasa ni upuuzi, kuna watu wanatetea rasili mali za nchi, wengine wamekomalia udini.
Huyo kwenye video ndiye John Okelo ?
Huyu si ndiye sheikh masheikh wenzie, mwaipopo, majini walimtukana mno kuwa ni sheikh uchwara, mhuni, tapeli, mchawi, mwizi, fuska, na kadhalika? Walimwanika hadharani kweli kweli huyu.TAMKO LA SHEIKH WA MKOA MWANZA KUHUSU MJADALA WA BANDARI
Utangulizi
Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kumekuwa na mjadala kuhusu uwekezaji na uendeshaji wa bandari zetu na kampuni kutoka Dubai. Mjadala ulianzishwa na wanasiasa na wanasheria lakini baadae ukachukua sura mpya na ya hatari ambayo nchi yetu haijawahi kushuhudia.
Hoja na mwelekeo wake
Wakati mjadala ulipoanza, hoja kubwa ilikuwa Wazanzibari wawili wanauza bandari za Tanganyika. Baada ya muda si mrefu, mjadala ukachukua sura mpya na kusisitizwa kuwa ni waarabu ndio waliouziwa nchi. Wakati mjadala unaendelea, ulihama kutoka sura ya kisiasa na kuingia udini.
Sote tumeshuhudia viongozi mbalimbali waandamizi wa dini ya kikristo walivyokuwa mstari wa mbele kupinga suala hili na wengine wamediriki kumkejeli Rais Samia Suluhu Hassan. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini ya kikristo kumkejeli Rais Samia.
Baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo wamedai kuwa Rais Samia amevunja Katiba na kwa maana hiyo anastahili kuondolewa madarakani. Mmoja wao ameenda mbali zaidi kwa kutishia kufanyike Mapinduzi ya kumuondoa Rais Samia madarakani. Jambo la ajabu ni kuwa mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja ambaye ameupinga mkataba wa bandari kwa hoja za kiuchumi.
Wote waliozungumza na hasa viongozi wa dini ya kikristo wamezungumza kwa jazba na kumshambulia Rais Samia bila sababu za msingi. Kama viongozi hawa wana uchungu na wananchi, tuliwatarajia kupaza sauti zao wakati wa utawala uliopita ambao tumeshuhudia watu wengi kupoteza maisha yao bila maelezo. Pia tumeshuhudia serikali iliyopita imeingia kwenye miradi mikubwa kinyume cha utaratibu. Sote ni mashahidi, hakuna kiongozi hata mmoja wa kiislamu aliyeushambulia uongozi uliopita.
Wito
Mimi ninaamini kuwa mjadala huu umetawaliwa na UDINI na una lengo la kumtoa Rais Samia madarakani kabla ya muda wake. Hivyo basi, kama sheikh wenu wa Mkoa, natoa wito kwa kila mwislam popote alipo katika Mkoa huu, afunge kwa siku 3 na katika kila swala ya Ijumaa kuanzia Ijumaa hii ya tarehe 7 Julai 2023 misikiti YOTE 700 ya Mkoa wa Mwanza isome dua ya kunuti kuwalaani WATU WOTE wenye nia ovu na Rais Samia.
Sheikh Hassan Kabeke ………………………………..
Sheikh wa Mkoa, MWANZA
Tarehe 6 Julai 2023