Umedhihirisha wewe ni mbaguzi, na ni mdini vile vile, mimi ni muislamu na Mwenyezi Mungu ametutaka tupendane na sio kuwekeana chuki, eti nimchukie mwarabu halafu nimpende only mwafrika[emoji1], unachekesha sana,, ni kwamba huna imani ndio maana unawachukia waarabu, kwa taarifa yako nawapenda binaadam wote bila kujali rangi ya mtu, udini na ukabila. Ilaa ilaa nachukia matendo maovu
Usome Uislamu vizuri upate kujua, waarabu ni ndugu zetu, siwezi kuona mwarabu anaonewa au kutukanwa na mkristo mtu ambae hana undugu na waislamu halafu nimuangalie tu, never never. Tena ondoa akilini hilo mzee
Huko kanisani ndivyo mnafundishwa kuchukia waarabu kiasi hicho? Huko makanisani mnafundishwa kuchukia wazanzibari kiasi hicho? Kisa waislamu!! Sikiliza bwana, tena watu kama wewe na wenye vimelea vya ubaguzi, udini na ukabila na kuchochea chuki dhidi ya waarabu na Uisilamu kwa ujumla, dawa yenu mkamatwe na kuswekwa ndani, ili iwe fundisho kwa wengine. Uisilamu ni dini iliyokamilika, usome vizuri upate kujua.
Elimu elimu elimu,
Maneno meeengi, in short jirekebishe na auache ubaguzi, udini na ukabila
Wewe ndiye mdini na umejipambanua wazi kuwa huwezi kumsaidia mkristo Badala ya Mwarabu ámbaye ni muislam mwenzako.
Sina upumbavu huo Wa kuwa mtumwa Wa Matajiri Toka nje.
Hapo unachokinyenyekea ni utajiri Wa Waarabu na SIO Dini.
Dini Kila mmoja Ana madili yake na Mungu wake. Wapo Waarabu wanaotumia Dini kujilimbikizia Mali bila na kuwanyanyasa watu kama mbwa.
Nimeweka wazi kuwa sitakubali kamwe nchi Yetu kuuzwa Kwa wageni Kwa Sababu tu ya Dini .
Sijapiga uislam Wala uarabu lakini napinga MTU yeyote anayegawa Mali za nchi Kwa kushindwa kusimamia watu aliowateua mwenyewe.
Wangeanza kuuza bandari za ndugu Wa Waarabu kule Zanzibar kabla ya zile za bara zenye mchanganyiko Wa wasio na Dini Wala nasaba za Kiarabu Kama tunaangalia udini na uarabu.
Tujifunze Kule Sudani ambapo wote ni Waislam lakini weusi wananyanyaswa kwenye bara lao na nchi Yao ya asili.
Zanzibar hawataki chama kingine kitawale na hawataki usultani wakati watanzibar wote ni Waislam.
Muungano ndio unawapa jeuri ya kuwaonea Wakristo kuwa SIO ndugu zao lakini Amini na kuambia Siku Muungano ukivunjika watanzibar watabaguaja Kwa rangi Kwa misingi ya Uarabu na Uafrika Kama wataanza kuchanganya mambo ya siasa Dini ,maendeleo na kutegemea Waarabu nje ya Zanzibar ndio wawaamulie kuhusu maendeleo ya nchi Yao.
Karume hakuwa mkristo lakini aliifanya Mapinduzi Kupinga dhulma za Waarabu. Hakupinga Dini ya kiislam.
Mimi sipingi kamwe uislam .
Na Karne hii hakuna mkristo anayehangaika Kupinga uislam. Wakristo na watu Wote wanaojitambua hawana muda Wa kuchanganya masuala ya Dini na uchumi ,watu Wanapinga kugawanywa Kwa rasilimali za nchi Yao Kwa Wageni bila kujali Dini . Wachina hawana Dini tulizo nazo lakini wameshika miradi mingi Kwa mikataba ya muda mfupi na ya kueleweka.
Huu mkataba uachwe haraka mana umejikita kwenye udini na Uarabu . Utaharakisha Amani na usalama Wa nchi.
Dubai ni mawakala Wa Marekani miaka mingi . Tanzania hatufungamani na nchi yoyote . Kuwakaribisha Wamarekani kupitia mgongo Wa Dubai ni kuhatarisha Amani ya ukanda Wa Bahari ya Hindi Kwa kupora Madini ya Urenium na kumiliki mafuta na gesi.
Dunia imejaa Matajiri Wanaowaza kulimbikiza Mali na Sio kuwasaidia WAAFRIKA. WAAFRIKA wakiamka Hawa watakua wamehamia Mars .