Sheikh wa Mkoa Mwanza (Kuhusu Mjadala wa Bandari): Walaaniwe wote wenye nia ovu na Rais Samia

Sheikh wa Mkoa Mwanza (Kuhusu Mjadala wa Bandari): Walaaniwe wote wenye nia ovu na Rais Samia

Kabila husaidia kubaini aina ya makuzi aloyopitia mtu. Pia urithi wa kitamaduni katika kuchambua saikolojia ya mtu

Hivyo hapo nimekusudia kumuonesha Sheakh Kebeke hoja zake utamaduni wake na elimu yake.

Kutaja Umanyema wake inamaana kunasabisha.
Nyabhera,
Chunga ulimi wako.
 
Kwahiyo Mohamed Said Na wewe mzee wangu na akili zako zote ukameza hizi pumba nzima nzima kama zilivyo?
Sasa una tofaut gan na yeye ? [emoji23][emoji23]
Hadi sasa sijamuona kiongozi yeyote kutoka mama wa kambo akijadili content za mkataba zaidi ya propaganda za udini na kulalamika.Kuwa muumini wa dini fulani hakukupi immunity ya ufisadi.
 
Hadi sasa sijamuona kiongozi yeyote kutoka mama wa kambo akijadili content za mkataba zaidi ya propaganda za udini na kulalamika.Kuwa muumini wa dini fulani hakukupi immunity ya ufisadi.
Wazanzibari kila siku hawautaki muungano ila sisi wabongo huwa tunapiga kimyaaa , sasa safari hii wabara wameamua kionyesha waz kuwa hata wao hawautaki muungano nashangaa jamaa wame step back wakat ndio wamepata sapoti ya kuvunja muungano ilitakiwa washangilie ila kama wameingia ubaridi hiviii akina Mohamed Said Wanawaza sijui watakwenda wapi wakishapokwa sifa za kumilik mali huku ugenini watasnda kujazannia wapi kwenye tule tuviwanja twao tuwili twa 20 x 20 pemba na unguja..mwisho wa siku watazipiga tu wao kwao.


Yan na choko choko zao zooote za muungano safari hii wamekua kimyaaa ndio watetezi namba 1 wa muungano wanaouitaga koti linalowabana.

Yule bwana mmoja Jusa hapo kat akajitutumua kujifanya mbwai mbwai naona kapotea kimyaaaaaa nadhan wamemtia kimiani wakamwambia "tutakwe da ishi wapi tukivunja muungano", hao waarabu wanaojitapa nao hawana hifadhi ya kuwapa
 
Sheikh njaa njaa tu hana point. Ajenda ya dp world ishajulikana
 
Umenichekesha sana mzee wangu.White fathers,Benedictine fathers,capuchin fathers si mashirika kama EAMWS.Those are religious congregations na wala hayajasajiliwa kama NGOs yanaoperate kwa mwamvuli wa kanisa katoliki
Ana uelewa very limited huyu mzee.Mpaka kuna muda unamuonea huruma kwel kwel sijui alisoma somaje hii elimu yake mpaka hizo masters
 
Nyabhera,
Samahani kwa kukosea jina lako na kuondoa shida hii nitaliandika kwa kirefu siku zote.
Wewe unaweza kuwa na tafsiri yako ya suala hili ambayo iko kinyume na yangu.

Mimi nina paper nzima nimeandika nakuwekea hapo chini kipande:

''Wamisionari hawa walipotia mguu pwani ya Afrika ya Mashariki, nia yao hasa ilikuwa kuufuta Uislam.

Wakazi wa pwani hii iliyokuwa ikijulikana kama Zanj waliuona Ukrsto kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1498 Wareno walipofika sehemu hizo.

Mwaka 1567 wamishionari wa Augustinian waliingia Afrika ya Mashariki kupambana na Uislam ili Ukristo uwe dini ya dunia nzima.

Kadinali Lavigirie alianzisha The White Fathers, taasisi ya Kanisa Katoliki kwa kusudi maalum la kuupiga vita Uislam Wakati huo huo Church Missionary Society (CMS) ilikuwa imejitwisha kazi ya kuondoa ulimwengu kutokana na Uislam, ujinga na giza.

Hadi hii leo White Fathers wapo Tanzania wapo Tanzania wakiendelea kufanya kazi iliyowaleta Tanganyika zaidi ya miaka mia iliyopita.

Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.''

Wamishionari wamekuja kuwastaarabisha watu Pwani ya Afrika ya Mashariki wakawakuta watu tayari wamestaarabika kwa miaka mingi sana.

Hili halikuwafurahisha.


Hongera kwa kupambna na kanisa ila pole sana mapambano yako niya bure mfumo wa kanisa dunia ya sasa huwezi ukwepa wala kuuangusha,all road leads to rome.
 
Mzee saidi,mbona unachuki sana na kanisa,wakati hata elimu unajinasibu nayo umeipata kupitia kanisa,je ndio kusema mfadhiri mbuzi,
 
Suala la udini lipo na jana Slaa kaongea mambo ya uvatican na hichi kikundi cha SAUTI YA WA TANZANIA haya kaongea mwenyewe. Huyu mzee na wenzake kuwashika kuwabana mapumbu mpaka wawataje wote wanaofadhili hichi kikundi, Yeye mwenyewe kasema wanafadhiliwa na kikundi hichi hata mkutano wa tarehe 22 ni hawa. Sasa hapa ndio pakuanzia.

Mkuu Mbona sijaelewa ulichokiandika hapa. andika upya kwa ufasaha tupate kuelewa.
 
Hongera kwa kupambna na kanisa ila pole sana mapambano yako niya bure mfumo wa kanisa dunia ya sasa huwezi ukwepa wala kuuangusha,all road leads to rome.
Jiwe...
Uislam unanikataza kufanya uadui.
Sijapata kupambana na kanisa na ningefanya hivyo ningeshondwa miaka mingi kwani hakuna mtu angependa kunisoma.

Lei nisingekuwa hapa JF.

Mimi naeleza ukweli wa historia yetu kama ilivyokuwa sipambani na yeyote.

Ndiyo naona hata unaponitukana na kunikejeli nanyamaza kimya.
 
TAMKO LA SHEIKH WA MKOA MWANZA KUHUSU MJADALA WA BANDARI

Utangulizi

Kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kumekuwa na mjadala kuhusu uwekezaji na uendeshaji wa bandari zetu na kampuni kutoka Dubai. Mjadala ulianzishwa na wanasiasa na wanasheria lakini baadae ukachukua sura mpya na ya hatari ambayo nchi yetu haijawahi kushuhudia.

Hoja na mwelekeo wake

Wakati mjadala ulipoanza, hoja kubwa ilikuwa Wazanzibari wawili wanauza bandari za Tanganyika. Baada ya muda si mrefu, mjadala ukachukua sura mpya na kusisitizwa kuwa ni waarabu ndio waliouziwa nchi. Wakati mjadala unaendelea, ulihama kutoka sura ya kisiasa na kuingia udini.

Sote tumeshuhudia viongozi mbalimbali waandamizi wa dini ya kikristo walivyokuwa mstari wa mbele kupinga suala hili na wengine wamediriki kumkejeli Rais Samia Suluhu Hassan. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa dini ya kikristo kumkejeli Rais Samia.

Baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo wamedai kuwa Rais Samia amevunja Katiba na kwa maana hiyo anastahili kuondolewa madarakani. Mmoja wao ameenda mbali zaidi kwa kutishia kufanyike Mapinduzi ya kumuondoa Rais Samia madarakani. Jambo la ajabu ni kuwa mpaka sasa hakuna hata mtu mmoja ambaye ameupinga mkataba wa bandari kwa hoja za kiuchumi.

Wote waliozungumza na hasa viongozi wa dini ya kikristo wamezungumza kwa jazba na kumshambulia Rais Samia bila sababu za msingi. Kama viongozi hawa wana uchungu na wananchi, tuliwatarajia kupaza sauti zao wakati wa utawala uliopita ambao tumeshuhudia watu wengi kupoteza maisha yao bila maelezo. Pia tumeshuhudia serikali iliyopita imeingia kwenye miradi mikubwa kinyume cha utaratibu. Sote ni mashahidi, hakuna kiongozi hata mmoja wa kiislamu aliyeushambulia uongozi uliopita.

Wito

Mimi ninaamini kuwa mjadala huu umetawaliwa na UDINI na una lengo la kumtoa Rais Samia madarakani kabla ya muda wake. Hivyo basi, kama sheikh wenu wa Mkoa, natoa wito kwa kila mwislam popote alipo katika Mkoa huu, afunge kwa siku 3 na katika kila swala ya Ijumaa kuanzia Ijumaa hii ya tarehe 7 Julai 2023 misikiti YOTE 700 ya Mkoa wa Mwanza isome dua ya kunuti kuwalaani WATU WOTE wenye nia ovu na Rais Samia.

Sheikh Hassan Kabeke ………………………………..

Sheikh wa Mkoa, MWANZA

Tarehe 6 Julai 2023
1. Elimu
2. ELimu
3. Elimu
 
Mzee saidi,mbona unachuki sana na kanisa,wakati hata elimu unajinasibu nayo umeipata kupitia kanisa,je ndio kusema mfadhiri mbuzi,

Kuna muda unasoma maandishi yake unaamua kukaa kimya. Eti ukristo uliletwa nia yake ni kuuwa uislam.
Waarabu walikuja kueneza islam waliwakuta wenyeji tayali wana mila na desturi zao ikiwamo dini zao, vile vile wazungu walikuja kueneza ukristo kwa minajili ile ile ya Islam ya kusambaza dini yao, hakuna mvaa kobazi na vipedo alipigwa ili awe christians na ndio maana wazungu wakaenda zaidi sehemu ambazo arab hawakupita kwa wingi.
Mzee shida yake ni kutaka kuona wote tunakuwa waislam, hicho kitu hakitakaa kitokee sasa kama uislam uliletwa nini kinamuuma ukristo kuletwa, huu ni ujinga wa akili.
 
Kuna muda unasoma maandishi yake unaamua kukaa kimya. Eti ukristo uliletwa nia yake ni kuuwa uislam.
Waarabu walikuja kueneza islam waliwakuta wenyeji tayali wana mila na desturi zao ikiwamo dini zao, vile vile wazungu walikuja kueneza ukristo kwa minajili ile ile ya Islam ya kusambaza dini yao, hakuna mvaa kobazi na vipedo alipigwa ili awe christians na ndio maana wazungu wakaenda zaidi sehemu ambazo arab hawakupita kwa wingi.
Mzee shida yake ni kutaka kuona wote tunakuwa waislam, hicho kitu hakitakaa kitokee sasa kama uislam uliletwa nini kinamuuma ukristo kuletwa, huu ni ujinga wa akili.
Ujamaa...
Hayo maneno ni ya White Fathers soma historia yao.
 
Back
Top Bottom