Sheikh wa Mkoa Mwanza (Kuhusu Mjadala wa Bandari): Walaaniwe wote wenye nia ovu na Rais Samia


Umeongea pumba na kupoteza bando. unajua yanayotendeka au unakalia kusoma habari za michezo
 
Umeongea pumba na kupoteza bando. unajua yanayotendeka au unakalia kusoma habari za michezo
Unafanya yaleyale niliyosema hamtaki mtu mwingine kuwa na maono mengine ndio maana nasema nyinyi kamwe hamtashika nchi JPM hata bungeni tu aliwasafisha.
 
Ubaguzi ni upi na wakiarabu ni upi?

Kama wewe ni Mwafrika achana na biashara za Kiarabu na kuwabagua waafrika wenzako .
Umedhihirisha wewe ni mbaguzi, na ni mdini vile vile, mimi ni muislamu na Mwenyezi Mungu ametutaka tupendane na sio kuwekeana chuki, eti nimchukie mwarabu halafu nimpende only mwafrika😄, unachekesha sana,, ni kwamba huna imani ndio maana unawachukia waarabu, kwa taarifa yako nawapenda binaadam wote bila kujali rangi ya mtu, udini na ukabila. Ilaa ilaa nachukia matendo maovu
Leo hii ikitokea ajali au janga lolote linalowahusu watanzania maskini weusi hakuna Mhindi Wala muarabu anayekusaidia wewe mmatumbi zaidi ya mmatumbi mwenzako .
Usome Uislamu vizuri upate kujua, waarabu ni ndugu zetu, siwezi kuona mwarabu anaonewa au kutukanwa na mkristo mtu ambae hana undugu na waislamu halafu nimuangalie tu, never never. Tena ondoa akilini hilo mzee


Huko kanisani ndivyo mnafundishwa kuchukia waarabu kiasi hicho? Huko makanisani mnafundishwa kuchukia wazanzibari kiasi hicho? Kisa waislamu!! Sikiliza bwana, tena watu kama wewe na wenye vimelea vya ubaguzi, udini na ukabila na kuchochea chuki dhidi ya waarabu na Uisilamu kwa ujumla, dawa yenu mkamatwe na kuswekwa ndani, ili iwe fundisho kwa wengine. Uisilamu ni dini iliyokamilika, usome vizuri upate kujua.

Elimu elimu elimu,

Maneno meeengi, in short jirekebishe na auache ubaguzi, udini na ukabila
 
Wewe ndiye mdini na umejipambanua wazi kuwa huwezi kumsaidia mkristo Badala ya Mwarabu ámbaye ni muislam mwenzako.

Sina upumbavu huo Wa kuwa mtumwa Wa Matajiri Toka nje.
Hapo unachokinyenyekea ni utajiri Wa Waarabu na SIO Dini.
Dini Kila mmoja Ana madili yake na Mungu wake. Wapo Waarabu wanaotumia Dini kujilimbikizia Mali bila na kuwanyanyasa watu kama mbwa.
Nimeweka wazi kuwa sitakubali kamwe nchi Yetu kuuzwa Kwa wageni Kwa Sababu tu ya Dini .
Sijapiga uislam Wala uarabu lakini napinga MTU yeyote anayegawa Mali za nchi Kwa kushindwa kusimamia watu aliowateua mwenyewe.
Wangeanza kuuza bandari za ndugu Wa Waarabu kule Zanzibar kabla ya zile za bara zenye mchanganyiko Wa wasio na Dini Wala nasaba za Kiarabu Kama tunaangalia udini na uarabu.

Tujifunze Kule Sudani ambapo wote ni Waislam lakini weusi wananyanyaswa kwenye bara lao na nchi Yao ya asili.

Zanzibar hawataki chama kingine kitawale na hawataki usultani wakati watanzibar wote ni Waislam.
Muungano ndio unawapa jeuri ya kuwaonea Wakristo kuwa SIO ndugu zao lakini Amini na kuambia Siku Muungano ukivunjika watanzibar watabaguaja Kwa rangi Kwa misingi ya Uarabu na Uafrika Kama wataanza kuchanganya mambo ya siasa Dini ,maendeleo na kutegemea Waarabu nje ya Zanzibar ndio wawaamulie kuhusu maendeleo ya nchi Yao.

Karume hakuwa mkristo lakini aliifanya Mapinduzi Kupinga dhulma za Waarabu. Hakupinga Dini ya kiislam.

Mimi sipingi kamwe uislam .
Na Karne hii hakuna mkristo anayehangaika Kupinga uislam. Wakristo na watu Wote wanaojitambua hawana muda Wa kuchanganya masuala ya Dini na uchumi ,watu Wanapinga kugawanywa Kwa rasilimali za nchi Yao Kwa Wageni bila kujali Dini . Wachina hawana Dini tulizo nazo lakini wameshika miradi mingi Kwa mikataba ya muda mfupi na ya kueleweka.

Huu mkataba uachwe haraka mana umejikita kwenye udini na Uarabu . Utaharakisha Amani na usalama Wa nchi.
Dubai ni mawakala Wa Marekani miaka mingi . Tanzania hatufungamani na nchi yoyote . Kuwakaribisha Wamarekani kupitia mgongo Wa Dubai ni kuhatarisha Amani ya ukanda Wa Bahari ya Hindi Kwa kupora Madini ya Urenium na kumiliki mafuta na gesi.

Dunia imejaa Matajiri Wanaowaza kulimbikiza Mali na Sio kuwasaidia WAAFRIKA. WAAFRIKA wakiamka Hawa watakua wamehamia Mars .
 
Unamnukuu Mohamed Said bila kumpa heshima yake.


Wengi ya uliowataja kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Tanganyika kawataja Mohamed Said.
 

 
Sema wafuasi wa bakwata wakiibuka kuongelea mambo ya kitaifa huwa wanatema upupu kuliko hata watoto wa primary school.

Tatizo nini ?
[emoji3526][emoji23][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji3526][emoji16][emoji4][emoji6][emoji6][emoji3526][emoji23][emoji38][emoji38]
 
Mohamed Said salam sheikh
Naanza kwa tahadhari kwamba unapoleta jambo ni vema ukajiridhisha na uthabiti wake.



Mag3 Fundi Mchundo JokaKuu Pascal Mayalla

Mbona umesahaukuwaiota kina pascal Mayala, Mzee Mwanakijiji, Yericko Nyerere, Mushi nani sijuwi. Waje kukusaidia?

Hao uliowataja pamoja na wewe bado, hamumuingii Mohamed Said. Unafikiri tumesahau alivyowahenyesha mpaka mkasema mtaenda kuandika kitabu chenu cha kumpinga? Kiko wapi?


Matokeo yake Yericko Nyerere akafanya plagiarism mtindo mmoja, sema akamkuta Alama Mohamed Said muungwana hakutaka kumsasambuwa, Mzee Mwanakijiji akaenda kuandika article hayohayo, plagiarism mwanzo mwisho.

Bado hamjaelimika. Ikiwa ma profesa wenu kina Issa Shivji wanaenda kupiga goti kwa Mohamed Said kuchota elimu, itakuwa nyinyi?
 
Unamnukuu Mohamed Said bila kumpa heshima yake.


Wengi ya uliowataja kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Tanganyika kawataja Mohamed Said.
Haiendi hivyo. Ninachopaswa kufanya ni kusema ni wapi nimetoa hayo niliyoandika na si vinginevyo. Kwa vile hii nilikuwa siandiki academic paper silazimiki kufanya hivyo. Vile vile siwezi vile vile kusema nani alikuwa wa kwanza kuwataja bila kufanya utafiti wa kutosha.

Amandla...
 
Tatizo la wengi wanaotetea mkataba upitishwe ni kwamba wanawapinga watoa hoja na sio hoja zinazoletwa
 
Faiza siku hizi umezidisha uongo. Lini nimewahi kusema kuwa nitaandika kitabu kushindana na Mohammed Said? Hebu weka hilo bandiko ambamo mimi au Nguruvi3 tumesalimu amri kwa Mohammed? Moja tu.

Hilo la Issa Shivji kumpigia magoti ni lako na wala halituhusu.

Amandla...
Nguruvi3
 
Mlikuwa wengi wengi tu tu siyo peke yako.

Wewe pia piga goti uulize upewe elimu. Unaijuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika ilianzia wapi? Hiyo unayoijuwa wewe utueleze na chanzo chako, thubutu kama hujarudi mule mule tu.

Huna ujanja huo.
 
Mlikuwa wengi wengi tu tu siyo peke yako.

Wewe pia piga goti uulize upewe elimu. Unaijuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika ilianzia wapi? Hiyo unayoijuwa wewe utueleze na chanzo chako, thubutu kama hujarudi mule mule tu.

Huna ujanja huo.
Faiza, sina haja ya kurudia rudia niliyoandika. Mimi na Mohammed Said tumejadiliana masuala mengi tu na sio historia ya Tanganyika peke yake. Nadhani mwisho wa siku tumekubali kuwa yeye hawezi kunibadili kama vile mimi nisivyoweza kumbadili.

Hii ni tofauti na mtu kama wewe ambae unaamini kuwa sehemu yote tunayoijua sasa kama Tanganyika ilikuwa chini ya Sultan wa Zanzibar. Mtu kama wewe ni vuvuzela maana unarudia tu bila kufikiri yale yanayosemwa na wale unaowaabudu. Mbaya zaidi ni muongo.

Amandla...
 
huna jipya, nimekuuliza swali dogo umeshindwa kulijibu.

Wewe unakijuwa nini kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika cha kuweza kubadili mawazo ya mtu?

Mengine hayo nakuona unabwabwaja na kuhororoja bila mpango.
 
huna jipya, nimekuuliza swali dogo umeshindwa kulijibu.

Wewe unakijuwa nini kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika cha kuweza kubadili mawazo ya mtu?

Mengine hayo nakuona unabwabwaja na kuhororoja bila mpango.
Faiza, ndio maana kujibishana na wewe ni kupoteza muda. Nitakujibu ukiniambia Chifu Mkwanyivika Munyigumba Mwamunyinga wa Wahehe alianza lini kumtumikia Sayyid Barghash bin Said al-Busaid aliyekuwa Sultan wa Zanzibar?

Amandla...
 
Faiza, ndio maana kujibishana na wewe ni kupoteza muda. Nitakujibu ukiniambia Chifu Mkwanyivika Munyigumba Mwamunyinga wa Wahehe alianza lini kumtumikia Sayyid Barghash bin Said al-Busaid aliyekuwa Sultan wa Zanzibar?

Amandla...
Hakuna "Chifu" aliyemtumikia Sultani, nijuavyo Sultani ndiye anawatumikia raia zake.

Kwanza hata jina "chifu" halikuwepo wakati wa utawala wa Masultani, kumbuka hilo.

Hakuna reality kwenye swali lako.
 
Bila maelezo Mengi.. hata Kwa Magufuli Kuna baadhi ya maamuzi viongizi WA kikristo walisimama kukemea hadharani pasipo unafki

Kwa huu mkataba hiyo inferiority complex yenu isitufanye tukaonekana tunao udini.. hapana

Na kama huyo shekh amaetamka hayo Mambo kweli ameonyesha udhaifu mkubwa kama kiongozi Kwa kufikiria jambo hili kidini..

Ukifatilia hoja za watanzania Ni kuhusu namna ambavyo mkataba umekaa kinyonyaji.. tunataka tuingie mkataba ambao wakizingua na Sisi tunawazungua yani Kwa kifupi

Nampa Sheikh mfano atakao uelewa Zaidi.. kama ilivyo ndoa ya kiislamu Talaka Ni ruksa
 
Hakuna "Chifu" aliyemtumikia Sultani, nijuavyo Sultani ndiye anawatumikia raia zake.

Kwanza hata jina "chifu" halikuwepo wakati wa utawala wa Masultani, kumbuka hilo.

Hakuna reality kwenye swali lako.
Faiza, wewe ni muongo au haujaelimika au vyote viwili. Nitajaribu kukuelimisha ingawa najua hauwezi kuelewa. Sultani au absolute Mfalme/ Malkia hajawahi kuwatumikia watu wake. Ndio maana watu hao wanaoitwa "subjects" wake na sio raia wake. Mifano hai tunaiona Saudi Arabia, Brunei, Eswatini, Morocco n.k. ambako neno la mfalme ni la mwisho.

Kama unasema hakuna Chifu aliyemtumikia Sultani utasemaje Sultani alitawala sehemu yote iliyokuja kujulikana kama Tanganyika? Ukweli ni kuwa Sultani wa Zanzibar hajawahi kutawala sehemu yote hiyo isipokuwa miji michache iliyokuwa katika pwani ya sehemu hiyo na michache iliyokuwa mwambao. Sehemu kubwa ya sehemu hiyo ilikuwa chini ya utawala wa viongozi wa kiafrika wa kiasili ambao kwa kiingereza waliitwa "chiefs" au machifu kwa kiswahili. Viongozi hao waliitwa majina mengine ( Mangi, Mtemi, Kabaka n.k.) kwa lugha za makabila yao.

Baadhi ya viongozi hao ndio walioingia mikataba ya maghumashi na Karl Peters. Karl Peters alifanya hivyo kwa sababu alitambua kuwa walikuwa viongozi huru na hawakuwajibika kwa huyo Sultani wako. Kuonyesha jinsi Sultani wako alivyokuwa hana nguvu, hakuhusishwa hata kwenye makubaliano ya Heligoland na Zanzibar! Najua hata hiyo Treaty hauijui.

Amandla...
 
Tatizo huuelewi Usultani wala Ufalme.

Na huelewi kuwa hakukuwepo hata neno "chifu" kwenye utawala sultani. Hata hao "machifu" wenyewe walikuwa hawalijuwi neno "chifu" mpaka alipokuja Muingereza.

Rudi kafanye homework kabla hujaja kulumbana na mimi..

Naona hoja ya neno "chifu" ilikukwida umekuja na kubwabwaja na kuhororoja mpaka povu. sasa mimi tu linakutoka povu, wewe ndiyo wa kumuelimisha Alama Mohamed Said kuhusu historia ya Tanganyika?

Usianzishe vichekesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…