Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Daaah mkuu umenikumbusha mbali sana, me mwenyewe nimeshawahi wekewa jiwe daah acha tu maumivu yake usiombe
 
Kanzu na tobo vina hadhi sawa tu na goli
 
Sijui watoto wetu wamepumbazwa na ma-TV? Yaani wanacheza kwa kusuasua sana, wakati enzi zile tulikuwa tunatoka mtaa kwenda kushindana na mtaa mwingine au kijiji kimoja na kingine! Mkitoka suluhu zinapigwa ngumi angalau timu moja ionekane bingwa!!
Kulikuwa hamna bodaboda mkuu
 
ukikataa kutoka wanakwita nyama. hapo mtu yeyote anaruhusiwa kukuchezea rafu.
 
Kipindi hicho Jezi mnatajiwa rangi tu na kila mtu anaenda mtumbani kivyake kununua jezi yake.

Kupaka mafuta ya nguruwe mwilini hili timu pinzani wakiroga uchawi usitupate.

Kwenda kwenye mechi na upupu hili kumuekea mchezaji mkali wa timu pinzani.
 
Mpira wa utotoni raha sana.

Yaani mtu huchoki, hiyo hata kula huoni umuhimu wake.

Hasa siku ya Jumamosi, nakumbuka Muda wa kula ukifika nikisikia naitwa "HARUFU, we HARUFU Chakula tayari" hiyo lazima niende sehemu nikajifiche, Maana tulikuwa na Dada wa Kazi mmoja, Muda wa Chakula ukifika lazima aite kwa makelele kabla ya kufika eneo husika.

Nakumbuka mambo ya kubambikiana, kupiga madochi ukipiga kijiwe, au lami ujue mpaka vidole vinatoka vidonda.

Mara ngumi zinaanza mpirani, ukinitukana ujue lazima tuzichape. Kupigana mpirani ni jambo la kawaida sana.

Magoli madogo, Gombania Goli, Kuchonga Kona, N.K.

Jamani
 
Daaah hii imenikumbusha mbali, enzi hizo kipindi cha dochi
 
mgeni,ambaye kwao kuna tv kisogo,monita/kiranja wa shule,wote hao lazima wapate namba.
mi nilikua nakapenda sana ka mchezo ka "tobo ngumi" namvizia nisiyempenda apigwe tobo hapo ndio atajua makonzi ni nini nilikua naenda kukaba mti ili asiushike aendelee kudundwa tu,
 
Viwanja viko wapi mkuu? Labda kwa vijijini tu lakni mjini watu wamejenga kila sehemu
Viwanja sio issue tulikuwa tunacheza barabaran wakubwa wakipita tunashika mpira kwa kusema "heshima" wakishapita Ngoma inaendelea Na magari yakipita mwendo n huohuo
 
Liseman anatumia shati la mmoja wenu kama kibendera!!!
 
Viwanja sio issue tulikuwa tunacheza barabaran wakubwa wakipita tunashika mpira kwa kusema "heshima" wakishapita Ngoma inaendelea Na magari yakipita mwendo n huohuo
Wamachinga wameziacha hizo bara bara pia population imekuwa kubwa mno
 
Kasambala safi saana nimefurahi nimepunguza sumu mwilini pa 1 saana dah!
 
Hahahah! ! Si ruhusa kucheza na viatu kama wenzako wako peku
 
Nyie watu munenichekesha sana . Yaani nimecheka hadi mbavu zng zinauma!!!
 
Ubabe ulikuwa unakuja kama goli halina kamba kwa juu halafu mpira upite sehemu yenye utata kama ni goli au mpira umepita juu!
Hapo timu yenye wababe na waongeaji sana ndo wanaamua!
 
Ubabe ulikuwa unakuja kama goli halina kamba kwa juu halafu mpira upite sehemu yenye utata kama ni goli au mpira umepita juu!
Hapo timu yenye wababe na waongeaji sana ndo wanaamua!
Au magoli ya kuweka Mawe.

Jiwe moja kulia, jiwe moja kushoto.

Yale ndio hayafahai kabisa.

Ulalamishi unakuwa mwingi sana pale Mpira upite juu kidogo ya jiwe.

Hapo ndio mtaanza, wengine wanasema "Goli", wengine wanasema "sio Goli".

Ukifanya mchezo, kama ni Mechi inaweza kuishia hapo.

Nakumbuka haya Magoli ya Mawe, anaepima anaweka jiwe moja kwanza, kisha anaanza kupiga hatua zake mpaka atakapotaka yeye kuwekwa jiwe la pili. Na hapa napo kunakuwaga na Ulalamishi wake, ambao:-

Wengine watasema Goli kubwa lipunguzwe, wengine watasema liachwe hivyohivyo.

Maisha haya, tunatoka mbali sana
 
Dana dana kuhesabihana, iwe ya mguu mmoja au iwe ya miguu miwili.

Kontroo, Vichwa, Tobo bao.

Mtu kati (unasafa), hapa zipo za aina mbili. Kuna ile moja ukigusa tu Mpira kwa yule aliekuwa nao, ujue hapo umejikomboa na yeye inakuwa zamu yake kusafa.

Na kuna ile nyingine lazima unyang'anye Mpira ndio ujikomboe na yule uliemnyang'anya inakuwa zamu yake kusafa.

Hapa kwenye kusafa panakuwaga patamu, pale inapotokea mmoja wenu kusafa kwa muda mrefu, mpaka anaesafa anakasirika.

Kabla ya kuanza napenda zaidi pale mnapoanza kuweka uamuzi kusafa kwa aina gani, Kugusa au kunyang'anya.

Maisha haya.

Eti sasa hivi na mie HARUFU naitwa Baba.

Jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…