Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Daah wengine hatujapitia izi mambo kabisa.
 
Habari za Muda huu wadauu Kwa wale Ambao
Tuliowahi kucheza cha Ndimu Uswahilini
Tukumbushane zle Sheria Zetu za Cha Ndimu

1.Mwenye Mpira lazma Acheze Hata kama hajui

2.Wale Ambao Waliokuwa Hawajui Kucheza kazi yao ilikuwa kuokota Mipiraa

3.Mabonge Ndo Makipa

4.Mwenye Mpira Akikasirika tu Basi Na Mpira umeishaa

5.Kuchimba ilikuwa kitu cha Kawaida Mnoo

6.Mpaka Mpira ukiisha Idadi Ya Magoli Inafikia hata 15

7.Kuna watu Hata Wakichelewa Lazma Namba wapate !

8.Magoli ya Miti Tena Mianz / Wavu NETI !

Tuongezee nyingineee Ambazo unazikumbukaaaa
 
SHERIA 11 ZA MPIRA WA UTOTONI
Kati ya hizi ulipenda ipi hasa,
1 Mwenye Mpira Lazima Acheze Hata Kama Hajui Kucheza

2 Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa

3 Mwenye Mpira Ataamua Nani Acheze Na Nani Asicheze

4 Kama Hujashiriki Kufuma Mpira Inawezekana Usipate Namba

5 Idadi Ya Wachezaji Inategemeana Na Uwanja

6 Mwenye Mpira Akikasirika Apoapo Mpira Utamarizika

7 Inaruhusiwa Kubadilisha Golikipa Kama Ikitokea Penat Na Kisha Ataendelea Kukaa Yule Yule

8 Mechi Itaisha Pale Giza Linapoingia

9 Wale Ambao Wamekosa Namba Kazi Yao Kuokota Mpira Ukitoka

10 Hakuna Mapumziko Wala Offsaid

11 Huruhusiwi Kuvaa Viatu

Mwenye nyongeza karibu
 
Kama mwenye mpira kapewa kazi na mam yake wote mnamsaidia ili nae aende pamoja nanyi kwenye gemu
 
Mwenye mpira ndio mwenye maamuzi ya wapi uwanja uwe.
 
Mpira unarusha kwa mkono mmoja au unajirushia mwenyewe
 
Ukicheza rafu sana wanakuziria mechi mpaka uombe samahani kwamba utacheza rafu tena au utoke nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…