Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakumbuka sana hiyo namba 8Sisi tulikuwa na sheria chache.
1.faulo pekee hata penati ni kushika
2.mpira ukitoka anaewahi ndio anarusha
3.hamna kona
4.hamna half time
5.giza ndio linaamua mpira uishe
6.mwenye mpira lazima acheze
7.mnyonge ndio kipa
8.hamna jezi,mwendo ni kuvaa au kuvua shati
9.hamna kucheza na viatu
10.anaejua yaani fundi lazima acheze mara nyingi huwa wanaringa sana
acha mkuuu....wazungu wametuhalibu sana..........Sijui watoto wetu wamepumbazwa na ma-TV? Yaani wanacheza kwa kusuasua sana, wakati enzi zile tulikuwa tunatoka mtaa kwenda kushindana na mtaa mwingine au kijiji kimoja na kingine! Mkitoka suluhu zinapigwa ngumi angalau timu moja ionekane bingwa!!
Umenikumbusha mbali kweliSheria 15 za mpira za kipindi cha utotoni;
1. Mkubwa hachezi na akicheza mnaingia wawili.
2.Mwenye mpira hatolewi hata akicheza vibaya.
3.Inaruhusiwa kubadili kipa kama penati imetokea na baada ya penati. anaruhusiwa kurudi wa mwanzo.
4.Yule mtaalam wa soka hakosi namba hata siku moja.
5. Dogo mnene lazima awe golikipa.
6.Mwenye mpira ataamua nani asicheze.
7.Penati itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.
8.Mechi itaisha kama kila mchezaji atakuwa amechoka.
9. Hakuna free kick, refa wala offside.
10. Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako mdogo kuliko wote uwanjani.
11.Mtaalam wa timu akipewa kazi na wazazi wake lazima mumsaidie ndo mwende kucheza.
12.Ukiumia kidonda kinawekwa mchanga.
13.Kipa anaruhusiwa kudaka popote.
14. Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mipira ikitoka.
15. Mwenye mpira akikasirika mechi ndo inakuwa imeisha.
Hilo rede balaa lake lilikuwa pale akina dada wanapo nyanyua vigauni vyao juuKweli kabisa yani kwa wasichana siku hizi hata rede,makida na mdako ni nadra sana kukuta wakicheza..utandawazi pia umetuathiri tunajenga nyumba ndani tiles nje vitofali vile chini hatubakizi ata kasehemu ka mchanga na udongo mtoto ata achimbe shimo la mdako na vishimo vya bao au achore kipande aruke aruke mtoto siku hizi akishika tu udongo mzazi anafoka minyoo akienda kucheza rede anaambiwa chokoraa...nitoe wito kwa wazazi watoto ni michezo ukiruka stage za mchezo utotoni matokeo yake ukikua sasa unaanza kuruka ruka kama mtoto
Umenena vyema sana mkuu alafu mbaya zaidi wanakomalia kichizi uwachangie wanakwambia jioni kuna bonge la game.., baadae wanakimbia kwa mhindi kwenye mkeka bet kufanya yao *****Kuna hawa wa siku izi kila siku unakita wametandika kitambaa chini kila anayepita anaombwa pesa utasiki, Kaka mkubwa tuchangie wanao leo Tuna mechi bana, ukiwapa badae wanaenda kubet yaani ni kero sana watoto wa siku hizi hakuna kitu
Yaani hawa ni kero sana, hii betting inaharib sana hichi kizaziUmenena vyema sana mkuu alafu mbaya zaidi wanakomalia kichizi uwachangie wanakwambia jioni kuna bonge la game.., baadae wanakimbia kwa mhindi kwenye mkeka bet kufanya yao *****
Maisha ni ya ajabu sana.Ukweli ni kwamba, unapokunywa bia moja ni sawa umekula matofali 2 ya kujengea kama utatumia tofali la 6inch kujengea, kwani bia 1 ni wastani wa tsh,2500 na tofali moja la watu grade ya chini ni tsh. 1200-1500 plus usafiri. Na kwakuwa wanywaji voltage hazipandi mpaka upige zaidi ya bia moja yaani lazima upige nyingi nyingi (na zile za ''waiter wazungushie!'') hapa kwa wiki unaweza kunywa kama bia 35, ukizidisha mara 1month unapata bia 140 ambazo ni sawa na tsh. 350000 ambazo unaweza pata tofali wastani wa 300, hivyo kwa kila mwezi utakuwa unaingiza tofali 300, Kwa mwaka utakuwa unaingiza tofali 3600 sawa na nyumba kamili (Self container) ya kupangisha. Hisabu hii ni kwa wanywaji daraja la kati.