Kuna majuha yataunga mkono huu ujinga, hayajui taifa linakosa mapato na wawekezaji kwasababu ya sheria za kipuuzi puuzi. Hata mimi situmi hela nikiombwa picha.
Hizi sheria za kipuuzi zinatungwa kwasababu tu ya uchaguzi #2020, kuwabana wapinzani, ila CCM hawafikirii madhara baada ya uchaguzi. Nchi inaongozwa kwa "FIKRA MASIKINI NA ZA KIJUHA".
Sheria za KODI kila mwaka zinabadilishwa, hazipo "STABLE" na hazipo kwaajili ya "LONG TERM", zinatungwa kwaajili ya mwaka husika tu halafu mwaka ujao zinatungwa nyingine tena au zinafanyiwa mabadiliko, hakuna hata mwaka mmoja hazija badilishwa sheria za kodi (atakae nithibitishia mwaka mmoja ambazo sheria za kodi hazija badilishwa nampa zawadi).
Raia akitaka kutoa USD 1,000/=$ lazima mpaka akaonane na "BANK MANAGER". Anapoteza siku yake ya kufanya shughuli zake ili akaonane na manager kwasababu ya USD 1,000/= (millioni 2 na nusu).
Wanatumiwa "MASIKINI" kuwachukiwa "MATAJIRI", wanatumiwa masikini kupumbazwa kwa vitu vichache ambavyo ni "HAKI" zao. Masikini anatumiwa kupumbazwa kwa "MADARAJA, BARABARA, NDEGE" wakati ni haki yao hivo vitu, mtu kachagua kiongozi ili amfanyie hayo yote iweje alazimishwe kupiga makofi na kudanganywa kwa haki zake. Mtu hachagui kiongozi ili akakae tu "MAGOGONI" au "OFISINI" kwenda kunywa chai na kupokea mshahara au kupiga picha na kukenua meno.
Watanzania bado tupo "PRE-COLONIAL ERRA" katika akili zetu, tunaishi kwa mazoea, tunashangalia haki zetu za msingi kwa viongozi, wakati ni "WAJIBU" wao kutufanyia hayo wanayofanya. Tunatakiwa tujifunzi kuangalia tofauti ya "HAKI YA RAIA, NA VITU VYA ZIADA".
Tuache kuangalia "BARABARA, MADARAJA, NDEGE, TRENI, ELIMU", hivo ni haki zetu za msingi. Tuangalie "AJIRA, MZUNGUKO WA HELA, UHITAJI WA KILIMO, KODI" ambavyo ni akili ya ziada na uwezo wa viongozi wetu.
#Itafika hatua nchi hii hata ukitaka kujamba basi lazima upige picha ya kitambulisho chako. Au akitaka kutoa hela ya kwenda kumnunulia mtoto baiskeli lazima akaonane na bank manager).