Sheria mpya za kutuma pesa kutoka nje zitapunguza mapato

Sheria mpya za kutuma pesa kutoka nje zitapunguza mapato

Sikuwai kujua km kuna app unaweza kutuma hela ukiwa nje ya nchi kuja bongo free of charge ngoja niifuatilie hii
Tena inaingia kwenye simu kwa njia ya mpesa au Eatel maney ndani ya sekunde kadhaa tu
 
Maneno mengi lakini porojo tupu.
Unaponunua wimbo kwa kutumia PayPal unadhani hiyo akaunti ya PayPal hawajui ni ya nani?
Unapotumiwa au kutuma pesa kwenye simu unadhani hiyo simu hawajui ni ya nani?
Unaponunua kitu online kwa kutumia credit cards unadhani hawajui hizo card ni za nani?
Mkuu, changanya na zako.

Sawa kabisa!

Unapofanya transaction yoyote ile online kwa kutumia credit na debit cards kunakuwa hakuna usiri wowote ule.

Watu wa mamlaka wakitaka kujua wala hakuna ugumu wowote ule.

Hizo kadi hutolewa na benki au taasisi za kifedha. Hizo taasisi zinajua nani na nani wamempa kadi zao.

Hivyo, kimsingi, ni vigumu sana kufanya transaction online halafu eti isijulikane mhusika ni nani.....labda itokee mtu aibe kadi zako halafu akazitumie sehemu ingine...na hata wezi na matapeli wanaofanyaga hivyo huwa wanaishia kukamatwa tu.
 
Hivi mkurupukaji hapa ni mimi au ni wewe? Unataka watu wawe wanatuma pesa kuja Tanzania kiholela, eti unaogopa nchi za dunia ya kwanza watatushangaa! Mi nakwambia hivi, hata hizo nchi unazoziita za dunia ya kwanza hawawezi kuruhusu pesa toka nchi za kigeni kuingia nchi mwao kiholela. Kama unataka kuhakikisha jaribu kutuma pesa kiholela kwenda USA uone kama hawatataka kujua wewe ni nani.
Tunapojadili maswala ya msingi kama haya jaribuni kuweka pembeni mihemuko yenu ya kisiasa, labda mtaweza kuleta hoja zinazojadilika badala ya pumba hizi za kila siku.

Ni rahisi sana.

Mtu ajaribu tu siku moja kwenda Walmart au popote pale palipo na wakala wa Western Union halafu ajaribu kutuma hela aone kama hataombwa ‘valid form of identification’.

Hii hapa chini ni kutoka FAQ section ya WU.

AA0C59D8-7095-4A4A-96CE-FE2895435319.jpeg


 
Afu nimekumbuka western Union haijadhibitisha 😂na xmass hii, wacha nifanye makeke.
 
Back
Top Bottom