Sheria ya Jeshi kuhusu mavazi ni ya kishamba na kizamani sana

Hivi imagine Kila kitu kinafanana kasoro nembo huoni Kwa tz inaweza kutumika kutapeli au kuonea watu...huko vijijini raia wanajua kweli mambo ya nembo?
 
Ni za mtumba lakini, Gwanda za.Jeshi zinajulikana
Kuna kaujinga, kaushamba na kaulimbukeni fulani kanatusumbua watanzania.

Nakumbuka hata prof. Ndalichako kwa umbumbumbu huu huu kama walionao wanajeshi alipiga marufuku wanafunzi wa sekondari , msingi na chekechea kuvaa majoho wakati mahafali. Ni upuuzi.
 
Nakubaliana yaani Kila mtu katimba mabaka mabaka eti kisa marekani wanavaa! Mbona tunapinga ushoga na marekani wanaukubali?
 
Hivi imagine Kila kitu kinafanana kasoro nembo huoni Kwa tz inaweza kutumika kutapeli au kuonea watu...huko vijijini raia wanajua kweli mambo ya nembo?
Kumbe tungejikita kuwaelimisha watu. Nguo za migambo waliotapakaa nchi nzima kila mtaa zinafanana na sare za polisi mbona haziongelewi?

Wanaotapeli kwa kofia ya kujifanya maafisa usalama wanatapeli mpk ofisini za serikali huko. Kwann hawaongelewi?

Kuna ka ujinga fulani ka wanajeshi kutaka kujiona wako tofauti kwa mavazi peke yake badala ya maarifa.
 
Mtu unavaa nguo inayofanana na ya jeshi ili nini? Kwamba umekosa nguo nyingine kabisa?
Acha wapigwe tu ili akili iwakae sawa. Tz ukijifanya unaijua sheria kuliko sheria yenyewe ilihali umekosea utajua hujui. Huku sheria zipo kama ushahidi tu, ukileta ujuaji utabondwa tu na baada ya hapo hata hiyo sheria utakua umesahau.
 
Kwanini uvae nguo ya jeshi? kwamba umekosa nguo nyingine kabisa wapigwe tu hakuna namna.
 
I agree. Ni ushamba na kukosa majukumu ya kufanya ya jeshi letu.
 
Nilitegemea wanajipanga kama walinzi wa taifa kukemea uwekezaji bandari loh! Kumbe wenzetu wanafikiria mambo tofauti kabisaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Kukataza watu kutumia nembo zao za taifa kama bendera, wimbo wa taifa na tunu zingine ilikua ujinga wa kiwango cha lami ndo maana wabongo wengi hawana uzalendo na nchi yao. Leo hii mtu akimaliza shule ya msingi anasahau kabisa wimbo wa taifa, ukienda nchi zingine zinapigwa kila kona, kila mtu ana bendera ya nchi yake. Bongo unafundishwa kuichukia nchi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…