Nafikiri ungesoma kisa chote ungeelwa uridhi unao zungumziwa
Mwanzo 12:2
[2]nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
Mwanzo 15:18
[18]Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Mwanzo 13:14-16
[14]BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi;
[15]maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.
[16]Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika.
Abrahamu anakata tamaa baada ya kuona umri wake na Sarah inasonga hakuna mridhi wa ahadi aliyopewa na Mungu, mpaka Abramu anapata hofu huenda Mtumishi wake Eliezeri Mdomeski angekuja kuridhi ahadi hiyo.
Mwanzo 15:2-4
[2]Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?
[3]Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
[4]Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.
Kumbuka Sara naye alishakata tamaa kuona ahadi ya Mungu haitimii umri imesonga miaka 90, ndipo anamuomba Mumewe Abrahamu azae na Majazi wake Hajiri, Akiwa na Mimba mahusiano ya Sarah na Mjakazi yake yakawa Mabaya kwani Mjakazi wake alianza kumsimanga Sarah kubwa ni Ugumba, hapo ndipo alipomtaka mume wake Abrahamu amfukuze,
Mungu alisikia kilio cha Sarah akamwambia Abrahamu afanye kama alivyoambiwa na Sarah.
Baada ya Mfukuza Hajiri anakutana na Malaika naye anamsihi amuombe msamaha Sarah na anampa Ahadi ya kuwa kupitia Mtoto wake Ismail na yeye atapata Uridhi
Mwanzo 16:9-12
[9]Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.
[10]Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
[11]Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.
[12]Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.