Prof. Palamagamba Kabudi
Sehemu ya Kumi na Nne ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania, Sura ya 425 ambapo kifungu cha 2
kinarekebishwa kwa kubainisha watu wanaosimamiwa na Sheria hiyo. Vilevile, kifungu cha 9 kinapendekezwa kurekebishwa ili kumuondoa Mkuu wa Shule ya
Sheria katika Kamati ya Mitihani na badala yake kumjumuisha Naibu Mkuu wa Shule anayehusika na masuala ya mafunzo ya sheria kwa vitendo. Aidha, muda wa Kamati unapendekezwa kuongezwa ili wajumbe wake waweze kuteuliwa kwa awamu nyingine. Madhumuni yamarekebisho haya ni kuweka mazingira
wezeshi kwa Kamati kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Kifungu cha 15
kinapendekezwa kurekebishwa kwa kubadili muundo wa Bodi ya Shule ili kuwajumuisha wajumbe ambao si wanasheria. Madhumuni ya marekebisho haya ni kuiwezesha Bodi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.
Sehemu ya Kumi na Tano ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho..
MADHUMUNI NA SABABU
__________________
Muswada huu unapendekeza marekebisho katika Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania, Sura ya 425. Kwa ujumla marekebisho yanayopendekezwa yana kusudia kuboresha changamoto mbalimbali zilizobainika katika
utekelezaji wa masharti ya Sheria.
Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Mbili.
Sehemu ya Kwanza inahusu masharti ya utangulizi ambayo yanajumuisha jina la Muswada na namna ambavyo masharti mbalimbali ya Sheria yana pendekezwa kurekebishwa.
Sehemu ya Pili ya Muswada inahusu marekebisho yana yopendekezwa katika vifungu mbalimbali vya Sheria kama ifuatavyo:
Kifungu cha 2
kinarekebishwa ili kubainisha watu wanaosimamiwa na
Sheria hiyo.
Kifungu cha 5
kinapendekezwa kurekebishwa kwa kupanua wigo wa majukumu ya Shule ya Sheria ili kujumuisha jukumu la kutoa mafunzo mengine mahsusi katika sekta ya sheria.
Kifungu cha 8
kinapendekezwa kurekebishwa kwa kuondoa takwa la majukumu ya Wakurugenzi kuainishwa katika kanuni na badala yake kuainishwa katika
skimu ya utumishi. Lengo la marekebisho haya ni kuhakikisha kuwa Sheria
inarejea nyaraka sahihi inayoainisha majukumu ya Wakurugenzi.
Kifungu cha 9(2) kinapendekezwa kurekebishwa kwa kumuondoa Mkuu
wa Taasisi kuwa katibu wa Kamati ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo
na Mitihani na badala yake kumuweka Naibu Mkuu wa Taasisi anayehusika na mafunzo.
Madhumuni ya marekebisho haya ni kuimarisha
utekelezaji wa majukumu ya Kamati kwa kuwa Naibu Mkuu wa Taasisi anayehusika na mafunzo ndiye mwenye jukumu mahsusi la kusimamia
masuala ya mafunzo na mitihani katika Shule ya Sheria.
Kifungu cha 9(4)
kinapendekezwa kurekebishwa kwa kubainisha muda wa ujumbe wa wajumbe wa Kamati ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Mitihani.
Lengo la marekebisho haya ni kuhakikisha kuwa muda wa wajumbe kuhudumu unatamkwa bayana katika Sheria.
Kifungu kipya cha 13A
kinapendekezwa kuongezwa ili kutambua katika Sheria nafasi ya Naibu
Ukurasa wa 6
Mkuu wa Taasisi anayehusika na mafunzo na Naibu Mkuu wa Shule ya Sheria anayehusika na utawala. Marekebisho haya yanalenga kutambua
nafasi hizi muhimu katika uongozi wa shule hiyo ambazo kwa sasa hazijatambuliwa katika Sheria.
Kifungu cha 15 kinapendekezwa kurekebishwa kwa kubadili muundo wa Bodi ya Shule ya Sheria ili kujumuisha wajumbe ambao si wanasheria.
Aidha, kifungu kidogo cha (3) cha kifungu hicho pia kinarekebishwa ili kuainisha mamlaka ya uteuzi ya wajumbe wa Bodi ambao hawaingii kwa
nafasi zao za madaraka.
Kifungu cha 17 kinapendekezwa kurekebishwa kwa kubainisha kuwa wajumbe wa Bodi watalipwa ada kadri
itakavyoamuliwa na Msajili wa Hazina. Lengo la marekebisho haya nikutambua nafasi ya Msajili wa Hazina katika kuamua ada na stahili za wajumbe wa Bodi.
Dodoma, PINDI H. CHANA,
7th January, 2024 Minister for Constitutional and
Legal Affairs
OBJECTS AND REASONS
___________________
This Bill proposes to amend the Law School of Tanzania Act, Cap. 425.
Generally, the proposed amendments aim at addressing various challenges
observed in the implementation of the Act.
The Bill is divided into Two Parts.
Part I deals with preliminary provisions which include the title of the Bill
and the manner in which the laws proposed to be amended are amended in
their respective Parts.
Part II of the Bill deals with amendments proposed to various sections of
the Act as follows:
Section 2 is proposed to be amended by specifying the persons to whom the
Act applies. Section 5 is proposed to be amended so as to widen the scope
of functions of the Law School to include provision of other specialised
training in the legal sector. Section 8 is proposed to be amended by
removing the requirement of prescribing for functions of the Directors in
by-laws and stating that such functions shall be stated in the Scheme of
Service of the School. The purpose of this amendment is to make reference
to the correct instrument which provides for the functions of the Directors.
Section is 9(2) is proposed to be amended by removing the Principal from
being the Secretary of the Practical Legal Training and Examination
Committee and replacing with the Deputy Principal responsible for
training. The purpose of this amendment is to enhance the functions of the
Committee as the Deputy Principal responsible for training is particularly
responsible for training and examination matters of the School. Further,
section 9(4) is proposed to amended by specifying the tenure of office of
the members of the Practical Legal Training and Examination Committee.
The purpose of this amendment is to define the term of service of the
members of the Committee. Section 13A is proposed to be added in order
to recognize in the Act the positions of Deputy Principal responsible for
training affairs and the Deputy Principal responsible for administrative
affairs. The purpose of this amendment is to recognise key positions in the
Page 6