Sheria ya Mirathi ya Kiislamu kwa mtoto wa nje ya ndoa ibadilishwe

Uasherati uruhusiwe! Kuna uwezekano pia akawa si mtoto halisi wa marehemu.
 

Wewe umeitaja Quran ndio Watu wanakueleza kuhusu taratibu za dini hizo za Ibrahim.

Suala la kuamini hizo dini ni la mtu binafsi. Kwani wewe au mimi ni lazima kuwa muislamu au Myahudi?
Ukishakuwa kwenye dini za Watu fuata maelekezo ya dini husika. Ukitaja dini fulani fuata maelekezo ya dini husika. Ûsilete maoni yako binafsi kwenye dini za Watu.

Hayo maoni yako binafsi yatumie kuanzisha dini yako ili upate Wafuasi watakaofuata maoni yako.

Unaweza kuwa sawa lakini sio katika dini na imani za Watu. Upo sawa kwenye maoni na mtazamo wako ambao unaweza kûutumia kwa uhuru kuanzisha dini yako au kuacha hizo dini za kigeni ukawa msela nunda
 
Huo ni mtazamo mfupi tu wala hauakisi faida hiyo,hasara anapata mtoto ambaye hajui hata nyege zenu ziliwafika kwa utaratibu upi.

Ni kama ile ya kufunika mwili wote isipokuwa pua,mvuto wa mwanamke hauamui ngono ila mtazamo uliopo kichwani mwa mwanamume na huyo mwanamke husika,naye anawezaona tu kifua cha mwanamume akamtamani.
 
Kuna mtu aliweka uzi kuhusu hili suala na kwenye maelezo ya huo uzi kuna sehemu ya mirathi ya kimila kwa mtoto wa nje ya ndoa.. nalo kalitizame vizuri

The best and only solution for this is to stop what called zinaa
Mila nyingi za africa hazitambui mtoto wa zinaa, jamaa kama yupo huru aombe elimu juu ya hilo .
 
Sasa hivi hakuna mtu anayetaka kutumia sheria zilizopitwa na wakati kama sheria za kidini na za kimila
Huyo baba kama angekua mfuata dini kweli asinge zaa nje ya ndoa at first place
Hakuna mtu analazimishwa kutumia hizi sheria
😛 😛
 
Huyo hajasoma sio dini hata mila kabisa wanakataa , zipo mila ukizaa nje ya ndoa unatengwa wewe na mwanao .
 
Haya zibadilishe,peleka muswada wa kubadilisha hiyo sheria kwenye Quran kwa mwenye Quran yake.
 
MIrathi ya ki-islamu inaongozwa na Quran.
Surat Al Nisa 4: na kuendelea inaongoza na ni muongozo wa "mungu'.
Unataka tu-amend Quran?
 
Katika Uislamu kitendo hicho cha zinaa ambacho kimefanywa na mwanaume na mwanamke ndio makosa na waliofanya wanafaa waadhibiwe hapa duniani ili wasafishwe kwa kosa lao hilo hadharani. Na Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Ametuagizia Tusikaribie kabisa zinaa (17: 32). Lakini tufahamu ya kwamba yule mtoto anayezaliwa hana hatia yoyote. Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema:

“Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Naye Atakuambieni mliyo kuwa mkitofautiana” (6: 164).

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) amesema: ((Kila kinachozaliwa kinazaliwa katika Uislamu .....)) l-Bukhaariy).

Na haifai kwa Muislamu kumuita mtoto aliyezaliwa kwa jina la mwana-haramu kwa sababu mtoto mwenyewe si wa haramu bali kitendo chenyewe ndicho haramu. Na ieleweke kuwa mtoto huyu hataitwa kwa jina la huyu mwanaume aliyezini na mamake kwa sababu kisheria si mtoto wake wala hawa wawili hawarithiani kabisa. Mtoto huyu hatamrithi huyo mwanaume na huyo baba hatamrithi mtoto huyo. Lakini mtoto anaweza kumrithi mama yake na mama kumrithi mtoto wake.

Tanbihi kwa kila mmoja wetu ajichunge sana ili asiingie katika madhambi haya ya zinaa. Na ndio sheria ikafanya ndoa kuwa rahisi na ikaweka adhabu kali kwa wenye kuzini.
 
Sioooo babake kwa kutomb..... ovyo
Mtoto wa nje hamfahamu baba'ke mpaka aambiwe na mama'ke, wengi wanabambikiwa tu.

Watoto wengine mpaka wanasikitisha, kila nwanamme anaeingia kwao anaambiwa "mwamkie baba"ko".
 
Kama sheria ndiyo iko hivo basi wasinung'unike ISMAEL (ISHMAEL) kunyimwa urithi wa ardhi ya mzee IBRAHIMU, maana ISHHAKA (ISAKA) ndiye alikuwa mtoto wa ndoa
 
Hizi tamaduni za kigeni wanazoita dini hazitufai kabisa sisi waafrika, tuache kufuata hizi mila zao walizoweka kwenye maandishi na kutudanganya kwamba ni maneno ya Mungu kisa tu walikuta mababu zetu wakiwa wajinga na washukuru Mungu walikuja enzi hizo ingekuwa leo hapangetosha.

Kwa mila zetu sisi waafrika kwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni uamuzi wa mwanamume kuamua aidha anakubali kum-adopt kama baba yake mzazi na kama ni hivyo basi mtoto anakuwa na haki zote kama watoto wengine wa kuzaa huyo mwanamme.

Lakini endapo mwanamme hayuko tayari kum-adopt huyo mtoto basi mama wa mtoto atamuacha huyo mtoto kwa bibi mzaa huyo mama na atalelewa hapo maisha yake yote bila ya kuwa na mafungamano yoyote na yule baba wa kambo na familia yake.

Hivyo ndivyo tunavyofanya sisi waafrika na ni vema tujivunie utamaduni wetu.

Kusema njia ni kuacha zinaa ni kukosa tu uelewa kwani zinaa sawa na dhambi nyinginezo haiwezi kwisha, binadamu tunaishi kwa kufanya makosa na ndio maana tunatofautishwa na malaika na hakuna siku tutaweza kuwa "Perfect" Never on earth na hakuna nchi itakaa isiwe na magereza, hakuna.

Mwisho, tufuate utamaduni wetu waafrika tuachane na tamaduni za kigeni kwani haziendani na utamaduni wetu.
 
Hata wakatoliki ni hivyo hivyo. Mtoto wa kambo hatambuliki.
 
Kuzaa ni maamuzi ya Mwanamke Mkuu.
Sex NI makubaliano ndio lakini kuzaa kupo chini ya mwanamke
Kuzaa ni maamuzi yenu wote wawili pale mnapo amua kufanya unprotected sex

Mwanaume ukivaa condom vizuri mwanamke hawezi kuamua kuzaa na wewe
Mwanaume ukifunga mirija mwanamke hawezi kuamua kuzaa na wewe
Mwanaume usipofanya sex na mwanamke hawezi kuamua kuzaa na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…