Sheria ya ndoa ifanyiwe marekebisho kuruhusu ndoa za mkataba

Sheria ya ndoa ifanyiwe marekebisho kuruhusu ndoa za mkataba

Hiyo mikataba kwa upande mwingine inaweza kutumiwa vibaya nawanaume kunyanyasa wake zao, sijui wahusika watafanya vipi kuhakikisha sababu zinazotolewa na upande wa mlalamikaji ni za kweli, au kama pakiwepo na consent toka pande zote ya kuvunja mkataba hapo itakuwa sawa.
Si mnakubaliana
Ndoa yetu itakuwa miaka 2.
Then tunarenew.
Kama tumeelewana tunaongeza mkataba.
Kama hakuna maelewano tunaishia na kuweka terms za kutunza matokeo ya ndoa.
Basi.
 
Si mnakubaliana
Ndoa yetu itakuwa miaka 2.
Then tunarenew.
Kama tumeelewana tunaongeza mkataba.
Kama hakuna maelewano tunaishia na kuweka terms za kutunza matokeo ya ndoa.
Basi.
Hii ndiyo inatakiwa iwe hivyo kwa kuwa wanawake wa siku hizi wanajifanya wanaharakati; vinginevyo migogoro ya ndoa, talaka na watoto wa mitaani vitaendelea kuwepo ktk nchi hii hadi Yesu atakaporudi.
 
Kwa hiyo unaokoteza kili kilichomo kwenye Biblia kukifanya sheria ya Mungu? Nionyeshe wapi Mungu alimruhusu Lameki kuoa wake wawili, tena aliua, hilo ni la Mungu?

Kwa hiyo Mungu alimwoza Abraham mjakazi? Thibitisha
Unaokoteza tu mandiko ili kuhalalisha sheria mbovu ya ndoa iliyopo. Ni wapi Mungu aliwaonya au kuwalaani hao waliooa wanawake wengi ktk hayo maandiko ya biblia niliyokuwekea hapo?
 
Unaokoteza tu mandiko ili kuhalalisha sheria mbovu ya ndoa iliyopo. Ni wapi Mungu aliwaonya au kuwalaani hao waliooa wanawake wengi ktk hayo maandiko ya biblia niliyokuwekea hapo?
Mkuu, huyajui maandiko, soma kama novel tu inakutosha. Kama huelewi kitu basic kama hicho nina mashaka kama wewe una msingi wa Ukristo, umejengwa kwenye msingi wa wabishani nami sina huo muda. Nadhani umenielewa, asante
 
Mtoa mada kuna mambo muhimu hujayafahamu kuhusu sheria ya ndoa.

Kwanza kabisa, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania, ndoa ni mkataba baina ya watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke. Hivyo sheria ya ndoa ya Tanzania inaruhusu ndoa za mkataba sababu ndoa kwa mujibu wa sheria ni mkataba.

Pili, ndoa zote Tanzania zinaweza kuvunjwa n Mahakama kwa kufuata taratibu za kimahakama, hivyo hakuna ndoa isiyoweza kuvunjwa kisheria Tanzania.

Tatu, hakuna sababu ya kutoa pendekezo ulilolitoa badala yake inapaswa uisome vizuri na kuielewa sheria ya ndoa. Ni muhimu kutoa mtazamo wako lakini ni muhimu zaidi kufahamu vyema kile unacholenga kukitolea mtazamo au maoni yako.

Tatizo ni kuwa watu wengi wanawaachia watu wengine hatima za maisha yao, unakuta mtu anateseka na ndoa kisa ni kuwaridhisha wazazi mara viongozi wa dini ili tu aonekane ana imani.

Huwa nasisitiza ukiona ndoa imegoma tafuta amri ya Mahkama kuivunja ndoa na talaka.
 
Hii ndiyo inatakiwa iwe hivyo kwa kuwa wanawake wa siku hizi wanajifanya wanaharakati; vinginevyo migogoro ya ndoa, talaka na watoto wa mitaani vitaendelea kuwepo ktk nchi hii hadi Yesu atakaporudi.
😂😂😂
 
Ukristo unasema ndoa ya mke mmoja, lakini ni wakristo wangapi wameishi na mke mmoja, na tuelewe kinachomaanishwa na ukristo hapa ni kwamba ukizaliwa usijishughulishe na jambo lolote linalohusiana na zinaa, mpaka utakapo oa mke mmoja na udumu nae huyohuyo maisha yako yote.
 
Serikali haijakukataza kuvunja ndoa, inavunja...

Na kama tatizo ni imani, Kama MUNGU anasamehe wauaji, atashindwaje kusamehe kuachana na mke pasua kichw na kuoa mwingine hata kama ni ndoa ya serikalini tu? Usifungwe na minyororo ya imani, kama humuelewi we muache GOD will understand.
 
Duuu hapa kwa kitabu cha kipagani uko sahihi100%, dini wakati mwingine ni nadharia tu ambazo ukiziweka kwenye vitendo haiendani na uhalisia
 
Duuu hapa kwa kitabu cha kipagani uko sahihi100%, dini wakati mwingine ni nadharia tu ambazo ukiziweka kwenye vitendo haiendani na uhalisia
Boss, hata dini sio ngumu hivi bali ni binadamu ndo wanaweka ugumu na kwa sababu tunataka kutafsiriwa kila kitu kweli mambo yanakuwa magumu.

Mfano: Kwenye ndoa imeandikwa ni kifo tu kitawatenganisha, hapo hapo kuna andiko limeandikwa ombeni nanyi mtapewa.

Sasa hapa ni ww tu na namna utakavyoyatumia maandiko. Mm ndoa ikinisumbua nitaomba kuvunjika kwa ndoa na nitapewa huo mvunjiko na sitataka mchungaji aje anielekeze kuwa hilo andiko la ombeni halihusu kuvunja ndoa, hayo maelezo nitayapata kwa BABA siku ya hukumu na nitajieleza na kwa sababu imeandikwa MUNGU ni pendo atanielewa tu.
 
Mtoa mada kuna mambo muhimu hujayafahamu kuhusu sheria ya ndoa.

Kwanza kabisa, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania, ndoa ni mkataba baina ya watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke. Hivyo sheria ya ndoa ya Tanzania inaruhusu ndoa za mkataba sababu ndoa kwa mujibu wa sheria ni mkataba.

Pili, ndoa zote Tanzania zinaweza kuvunjwa n Mahakama kwa kufuata taratibu za kimahakama, hivyo hakuna ndoa isiyoweza kuvunjwa kisheria Tanzania.

Tatu, hakuna sababu ya kutoa pendekezo ulilolitoa badala yake inapaswa uisome vizuri na kuielewa sheria ya ndoa. Ni muhimu kutoa mtazamo wako lakini ni muhimu zaidi kufahamu vyema kile unacholenga kukitolea mtazamo au maoni yako.

Tatizo ni kuwa watu wengi wanawaachia watu wengine hatima za maisha yao, unakuta mtu anateseka na ndoa kisa ni kuwaridhisha wazazi mara viongozi wa dini ili tu aonekane ana imani.

Huwa nasisitiza ukiona ndoa imegoma tafuta amri ya Mahkama kuivunja ndoa na talaka.
Mkuu nadhani bado hujaelewa hoja yangu na kama umeielwa basi umeilewa nusu.

Kwanza, ndoa ni mkataba lakini sio mkataba wa kudumu na kumbuka kwamba kila aina ya ndoa (ndoa ya kimila, kikristo au kiislamu) ina masharti yake na namna ya kuivunja. Ninachojaribu kusema ni kwamba kuwepo na sheria itakayo harmonize ndoa zote ili kusiwe na mkwamo pindi mwanaume anashindwa kuishi na mke. Kwa kuwa mume ndiye atakuwa anasaini na ku renew mkataba, pindi mke akikengeuka hakuna haja ya kwenda mahakamani. Simply unasubiri mkataba (mfano wa miaka mitatu, mitano, etc) una expire kisha una terminate contract kwa kuto renew mkataba mpya. Huhitaji kupoteza muda na pesa kwenda mahakamani kujieleza au kupeleka mashahidi. Tupo pamoja?

Pili, sitaki ndoa zifike mahakamani.....mashataka yanapoteza muda na pesa.....nataka ndoa iishie mikononi mwa mume (anayesaiani mkataba). Hivi wachezaji wa mpira wasipoongezewa mkataba huwa wanakimbilia mahakamani? La hasha! Timu isipokuongezea mkataba unatafuta timu nyingine au unastaafu (ikiwa umri umeenda).

Tatu, nimetoa pendekezo hili kwa sababu sheria ya ndoa ya Tanzania haisemi ukomo wa ndoa ni kila baada ya miaka mingapi. Haisemi chochote kuhusu ukomo wa ndoa. Serikali itakapoanza kutumia sheria ya ndoa ya mkataba hapa nchini lazima itataja muda wa mkataba (mfano miaka mitatu. mitano, kumi, etc).
 
Serikali haijakukataza kuvunja ndoa, inavunja...

Na kama tatizo ni imani, Kama MUNGU anasamehe wauaji, atashindwaje kusamehe kuachana na mke pasua kichw na kuoa mwingine hata kama ni ndoa ya serikalini tu? Usifungwe na minyororo ya imani, kama humuelewi we muache GOD will understand.
Sawa lakini kukiwepo na sheria ya ndoa ya mkataba huhitaji hata kufika mahakamani. Unaacha tu ku renew mkataba au una terminate mkataba, kwisha habari. Wanawake wa siku hz wana ngebe sana, dawa yao ni hii tu!
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Boss, hata dini sio ngumu hivi bali ni binadamu ndo wanaweka ugumu na kwa sababu tunataka kutafsiriwa kila kitu kweli mambo yanakuwa magumu.

Mfano: Kwenye ndoa imeandikwa ni kifo tu kitawatenganisha, hapo hapo kuna andiko limeandikwa ombeni nanyi mtapewa.

Sasa hapa ni ww tu na namna utakavyoyatumia maandiko. Mm ndoa ikinisumbua nitaomba kuvunjika kwa ndoa na nitapewa huo mvunjiko na sitataka mchungaji aje anielekeze kuwa hilo andiko la ombeni halihusu kuvunja ndoa, hayo maelezo nitayapata kwa BABA siku ya hukumu na nitajieleza na kwa sababu imeandikwa MUNGU ni pendo atanielewa tu.
Ndio maana nashauri kuwepo na sheria ya kurahisisha hili jambo ili kuepuka usumbufu wa kwenda mahakamani.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Sio ya mkataba Bali ya mitara!!

Ndoa zinazosumbua Sana ni za wakristo coz Hazina mitara NDANI yake!!

Za waislamu hazisumbui Sana!!coz Zina kadi ya kijani,njano na nyekundu!!

Pia zinaoption ya kuongeza changamoto ya mapenzi kea kuongeza mke wa pili!!
 
Imezuka tabia ya hovyo kujaribu kushambulia ndoa zenye msingi wa Ukristo, mke mmoja na mume mmoja. Wengi wanaojenga hoja za mashambulizi ama hawajui msingi wa ndoa za kikristo, ama wanafanya kusudi kutetea madhaifu ya imani zao.

Model pekee ya ndoa bora kabisa duniani mpaka sasa ni ile aliyoanzisha Mwenyezi Mungu, mke mmoja mume mmoja. Hii ni ndoa inayojenga amani kwa pande zote mume, mke na Mwenyezi Mungu. Hii ni ndoa iliyokusudiwa kwa kiasi kikubwa kumlinda mwanamke ambaye thamani yake kimwili hushuka kadri miaka inavyoyoma.

Sasa kwako mwandishi potofu:

Kutaka ndoa iliyoasisiwa na Mwenyezi Mungu ipatiwe ufumbuzi kwa sheria za mwanadamu ni upuuzi mkubwa sana. Rais Samia pamoja na mamlaka yake kikatiba hana uwezo wa kuamua kuibatili sheria ya Mungu eti kuwakomesha wanawake kwenye ndoa ya mke mmoja. Huu ni ufinyu wa fikra na ukurupukaji wa kiwango cha juu mno!!

Kwa kifupi tu, ndoa nyingi za nyakati zetu zinazoitwa "za kikristo" kiukweli SIO ZA KIKRISTO, ni za mataifa tu ila zimefungwa makanisani. HAKUNA NDOA AMBAYO NI AGANO MBELE YA MUNGU yenye migogoro ya kijinga kama tunavyo shuhudia hii leo. Migogoro mingi ya ndoa ni upumbavu wa 1. Zinaa 2. Mali 3. Haki sawa. Katika haya yote hakuna ndoa ya sheria ya Mungu, kwani kwa Mwenyezi Mungu yote hayo yamewekwa wazi. Hakuna sehemu imeachwa ili WANANDOA WENYEWE WAJADILI NJIA BORA. Kwenye ndoa inayofuata sheria ya Mungu mume amepewa majukumu yake na mke kadhalika. Huu uchafu mnaouona siku hizi huko makanisani mkauita ndoa sio kweli, ni uhuni kama wahuni wengine tu.

Ndoa ya kweli inaanza kwa msingi mkuu, kumheshimu Mungu kwa kuishika sheria yake. Mume akimpenda Mungu hatozini, mke akimpenda Mungu hatozini. Mke akimpenda Mungu atamheshimu mume kwa ajili ya sheria ya Mungu, tena ita-flow naturally toka moyoni, pia mume akimpenda Mungu atampenda mkewe kwa ajili ya neno la Mungu.

Ni heri kujifunza sheria ya Mungu kuliko kukimbilia kuleta upuuzi kama huu ulioandika. Ndoa za mikataba SIO WAZO LAKO kwani kwa miongo mingi tu huu upumbavu unafanyika Ulaya. Nasema upumbavu kwa sababu ni mambo kama haya yamepelekea wanaume wengi huko Ulaya na Marekani wameacha kuoa, MGTOW.
Ingawa unetumia lugha kali kidogo, ila uko sahihi,
Chanzo cha ndoa nyingi kuingia kwenye mafarakano ni kwasababu ya kumuasi Mungu na kuishi kiholela bila kufuata sheria ya ndoa iliyowekwa na Mungu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Malaki 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
¹⁵ Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
¹⁶ Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.

Mkuu, Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa halafu anasema anachukia kuachana, wewe ni nani utoe talaka? Mke wa ujana ni yule uliyemwoa kwanza kabisa tena katika ubikira wake ndio akaitwa MKE WA AGANO LAKO.

Hii ndiyo aina ya ndoa aliyoiasisi Mwenyezi Mungu na hivyo ndio ndoa bora kabisa sawasawa na kusudi lake. Labda kama unaamini kuwa Mungu anaweza kukuletea mpango mbovu wa maisha.

Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
⁵ akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
⁶ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe
.

Unaamini mwanadamu anaweza kuwa na mtazamo bora zaidi kuliko Mungu hata amkosoe?
Ubarikiwe sana mtumishi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom