Malaki 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
¹⁵ Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
¹⁶ Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.
Mkuu, Mungu ndiye mwanzilishi wa ndoa halafu anasema anachukia kuachana, wewe ni nani utoe talaka? Mke wa ujana ni yule uliyemwoa kwanza kabisa tena katika ubikira wake ndio akaitwa MKE WA AGANO LAKO.
Hii ndiyo aina ya ndoa aliyoiasisi Mwenyezi Mungu na hivyo ndio ndoa bora kabisa sawasawa na kusudi lake. Labda kama unaamini kuwa Mungu anaweza kukuletea mpango mbovu wa maisha.
Mathayo 19 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
⁵ akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
⁶ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Unaamini mwanadamu anaweza kuwa na mtazamo bora zaidi kuliko Mungu hata amkosoe?