diggymkula
Member
- Jan 10, 2014
- 10
- 3
Naomba mnifahanishe iwapo mke ndio kataka kukatiza ndoa YAKE namaanisha kuomba talaka bila Kuwa na ugomvi Kati YAKE na mumewe je hapo kunahitajika kigawana Mali? Na je mtoto ataenda kuishi na mama au Baba?
Kumbuka sheria haijaundwa ili kuvunja ndoa, bali ni kutatua matatizo ktk ndoa...lazima kuna sababu ya mke kuomba talaka.....
Na kama mali mlichuma wote lazma mgawane.... Bt kama alikukuta nazo... Hakuna kugawanywa...
ili talaka itolewe, zinatakiwa ziwepo sababu zitakazothibitisha kuwa ndoa hiyo imevunjika pasipo kuwepo na nafasi ya kusimama tena. na hii ni baada ya kupitia kwenye balaza la usuluhishi na kupatiwa cheti ambacho wasuluhishi wenyewe wamenyoosha mikono kuwa kati yenu hamuwezi kuishi pamoja milele kutokana na sababu zilizopo. katika sheria zipo sababu kadhaa zimeorodheshwa ambazo mmoja wenu anaweza kuzitumia....nitakuwekea link ya kupata sheria hizo hapa ukaifuate na uzisome. kuna kitabu cha sheria kimeandikwa kwa kiswahili, ukikisoma utaelewa na hutakuwa na maswali. hata hivyo kwa harakaharaka unavyoeleza naona kama hapo kati yenu hakuna sababu yeyote itakayofanya mpate talaka....labda kama umemung'unya maneno. kwa ufafanuzi zaidi bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILINaomba mnifahanishe iwapo mke ndio kataka kukatiza ndoa YAKE namaanisha kuomba talaka bila Kuwa na ugomvi Kati YAKE na mumewe je hapo kunahitajika kigawana Mali? Na je mtoto ataenda kuishi na mama au Baba?
Hakuna ukweli wowote hapo Mkuu Daata. Kifungu cha 160 cha Sheria husika kinatoa Dhanio la Ndoa.Hili huwepo pale ambapo mwanamke na mwanaume huishi kama mke na mume kwa miaka miwili au zaidi.Wakati wa kuishi kwao na kupata heshima ya jamii kama mke na mume wanaweza kuchuma mali mbalimbali.Sasa katika kuhitilafiana kwao,mwanamke hataondoka mikono mitupu. Hiyo ni dhana tu ya Dhanio la Ndoa na hutumika hivyo na si vinginevyo
Asante Mkuu alteza kwa swali lako. Umri wa wa kiume ni miaka 18 na wa kike ni miaka 15.Lakini,Mahakama yaweza kuwaruhusu wanaotaka kuoana kuoana hata bila kuwa na umri huo endapo: kwanza,wote wamefikisha umri wa miaka 14,na pili kama Mahakama imekubaliana na mazingira yaliyopo na kuiona ndoa husika inayotakiwa kufungwa.
Hello! Je inawezekana mahakama kuvunja ndoa pale inapotokea mmoja wa wanandoa amepoteza mapenzi kwa mwenzake kwa kiwango ambacho yeye hawezi kuvumilia na hakuna mtu au taasisi inayoweza kubadili mtazamo wake wa kimapenzi kwa mwenzie? Otherwise nipe sababu za msingi za kisheria zinazoweza sababisha ndoa kuvunjika, in details please.
Kwanza samahani kwa kuchelewa kufuatilia munakasha huu....Pole kwa majukumu haya Wakili msomi.
Katika hili naomba tusaidiane kuliweka sawa....Umri wa ndoa ni miaka 18 kwa mke au mume.....ila mke anaweza kuolewa katika umri wa 15 kwa Ridhaa ya Baba..kama hayupo basi mama na kama hawapo wote basi mlezi.....Binti anaweza kuolewa katika umri 14 iwapo mahakama itaona inafaa...e.g akiwa mjamzito tayari.
Mvulana anaruhusiwa kuoa katika umri wa 16 iwapo mahakama itaona inafaa e.g akiwa amempa binti mwenye umri wa ndoa (18+) ujauzito na anatambua majukumu ya ndoa.
Mkuu petro naomba kuuliza, kwa mfano mtu kafunga ndoa nje ya nchi na ndoa yenyewe ilikuwa kwenye moja ya makubaliano ya pre nuptials, je wanandoa hao wanatakiwa wafenyeje warudipo nchini ili ndoa yao itambulike kisheria na labda pre nuptial agreement yao iweze kutambulika kisheria
Awali nakupongeza kwa kuchukua jukumu la kutuelimisha sisi wenye ufahamu mdogo kuhusu mambo haya.
Swali langu linahusu mabaraza ya usuluhishi. Nafamu (sina uhakika kama ndivyo kisheria), mabaraza ya usuluhishi ni pamoja na Bakwata, Baraza la kata na mabaraza ya usuluhishi makanisani.
Mimi ni muumini wa dhehebu fulani na ndoa ilifungwa huko ninako abudu (mathalani msikitini/kanisani). Ninapotaka kuvunja ndoa, ili niweze kupata baraka za baraza la usuluhishi, natumia baraza lipi?
- Kama mume/mke wote ni wakristu wanatumia baraza lipi (la kata, la kanisa)?
- Kama mume/mke wote ni waislamu wanatumia baraza lipi (la kata, bakwata)?
- Kama mume/mke wote ni dini mchanganyiko wanatumia baraza lipi?
NB: Kwa ndoa za kikiristu, ni vigumu sana baraza la kanisa kutoa kibali ya kuwa ndoa hairekebishiki tena. Mbadala wake ni upi?
Asante, kazi njema