Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

The Law is the reflection of peoples culture, when the law comes into being it intends to be a servant of man and not making men servants of the law thus the law will regulate the conduct of the society,protect individuals and also give retribution or redress to the people whose rights are violated, therefore I will speak on the issue of law being the custodian of marriage.

First of all family is one of the most basic pillar of the society, strong nations are built on firm families therefore the state has a sacred duty to protect families. It allows for divorce just as the Tanzanian Law of Marriage Act says but it has made it a very hard thing to attain, it starts with the requirement of two years prolonged cohabitation.

Also it demands the families to visit the marriage reconciliation board which is vested with power under the Act to give room for couples to talk openly on issues pertaining their marriage, remember the marriage reconciliation board is created by the Minister Responsible and if the board fails to keep the marriage intact there will be a presumption that the board if failing to do the job it was assigned to do.

But comes circumstance where one party suffers unnecessarily and excessively that he or she cannot bear it anymore, here also the Act mentions of things like cruelty and many things just find the Act. Kumbuka ndoa inalindwa sana na serikali hivyo huwezi kuamua kutoka bila kutoa sababu za msingi za kwanini unataka talaka na pia hiyo bodi ya usuluhishi ni laziama iwe imeridhia kwamba ndoa yenu haiwezi kuendelae teena hivyo kuwaruhusu muende mahakamani kwa ajili ya talaka.

Kama nilivyosema kwamba serikali inalinda saana ndoa ndiyo maaana kabla hata ya kutoa talaka wanandoa wanaweza kukubaliana kupeana mapumziko ambayo kwa lugha ya kiingereza we call it Separation,haya yanaweza kuwa ni uamuzi wenu au mahakama yenyewe ikawaamulia. This action have a psychological impact on the both couples kwasababu kama mnapendana mtatafutna Japo kama muda wa zaidi ya miaka mitatu itapita bila nyinyi wajamaa kukumbukana then tutajua marrige is irreparably broken down therefore lazima talaka itolewe kama moja atadai.

Suala la mali siku hizi limekuwa utata because women are highly protected na kumbuka kabla hamjaona kama huna nia ya kuifanya mali yako kuwa ya familia or Matrimonial property then inabidi utamke kabisa na kama hutasema basi kwenye kugawana ni lazima mwanamke aangaliwe saana kwasababu kumbuka hata kama umejenga nyumba wakati wa ndoa ikatokea upepo makali ukaja ukavunja madirisha basi mke wako akanunua vioo vipya then her contribution will be put into consideration ila hii ni pale ambapo mali haijasemwa ni ya nani.

On the other hand kumbuka hata pale ambapo unaenda kazini mkeo anakuamsha na kukwambia baba fulani maji tayari,kakunyooshea nguo na unakuta chai iko mezani unakunywa unaondoka na kwenda kazini kwa furaha na unapata mshahara by one way or another her contribution made you get the salary running through your wallet therefore lazima alindwe.

Pia mtoto kama ni mdogo kama ni chini ya miaka saba lazima akakae na mama yake huko hata kama atampendaje baba yake here what is put into consideration is the best interest of a child lakini kama ni zaidi ya hapo pia itaangaliwa ni mzazi yupi ambaye anaweza kuishi vizuri na mtoto kumbuka kama mama ni wa hovyo kama mlevi sugu hawezi kukaa na mtoto hapo mahakama itaweza kumruhusu baba kama utakuwa na uwezo ila kwa

Uingereza mtoto akiwa mdogo halafu wazazi hamueleweki then serikali itamchukua kwa nguvu mtoto akikaa na mama ni lazima uwe unapeleka hela za mahitaji, tafuat Marriage Act na Usome yote ni rahisi kueleweka saaana.
 
Naomba mnifahanishe iwapo mke ndio kataka kukatiza ndoa YAKE namaanisha kuomba talaka bila Kuwa na ugomvi Kati YAKE na mumewe je hapo kunahitajika kigawana Mali? Na je mtoto ataenda kuishi na mama au Baba?

Tukianza na hilo la kukatisha ndoa bila ugomvi.

1. Sheria ya ndoa hairuhusu mahakama kuvunja ndoa na kutoa talaka bila sababu za msingi zilizoanishwa.

2. Kimsingi huyo mwanamke ndiye mwenye shida na kwakuwa kaona mume wake hana mpango wa kumpa talaka anataka yeye ndiye aombe talaka mahakamani kitu ambacho hakiwezekani kwani atakuwa anjishitaki mwenyewe.

3. Sio kila ugomvi unapelekea kuvunjika kwa ndoa lazima hali iwe imefikia ndoa kuwa imevunjika na haiwezi kurekebishika " broken down irreparably" na kuwe na ushahidi wa kutosha kuhusu say adultery, physical and mental torture, kutelekezwa e.t.c

4. Imekuwa ni tabia ya wanawake wengi siku hizi kwenda kuomba talaka mahakamani bila sababu za msingi akifikiri atapata mgawo wa mali. Wengi wanafikiri waki fall out of love (kuisha kwa mapenzi kati ya wanandoa) inaweza kuwa sababu tosha , sio rahisi Mahakama hazikuwekwa kuvunja ndoa.

5. Kama mama ndio mkosaji esp tabia za kikahaba, ukatili and other moral issues hawezi pewa mtoto hata kama ana mwaka 1.

Kuweni makini sana. Taasisi ya ndoa inalindwa sana kisheria si kama watu wanvyofikiri eti naenda kuomba talaka mahakamani akijua ni kitu rahisi kupewa.
 
Kumbuka sheria haijaundwa ili kuvunja ndoa, bali ni kutatua matatizo ktk ndoa...lazima kuna sababu ya mke kuomba talaka.....
Na kama mali mlichuma wote lazma mgawane.... Bt kama alikukuta nazo... Hakuna kugawanywa...

Mkuu nakubaliana nawe. Wenzetu Kyle america wana makubaliano ya mgawanyo wa Mali katika ndoa , yaani prenuptial agreement. Kwamba wanandoa wanakubaliana kuwa Mali za mume ni za mume kabla na baada ya talaka. Au za mke ni mke kabla na baada ya talaka.
 
Hii kitu bongo watu wakidivorce wanagawana mali 50/50 ilikuwa inanishangaza sana sema sikupata nafasi ya kuuliza, kwa iyo bongo hakuna marriage agreements zitakazosimamia mali za wanandoa, kabla ya ndoa kufungwa na baada ya ndoa kuvunjika au raia hawajui kuhusu iyo option na wengi wanaoa in community of property.
 
Mkuu petro naomba kuuliza, kwa mfano mtu kafunga ndoa nje ya nchi na ndoa yenyewe ilikuwa kwenye moja ya makubaliano ya pre nuptials, je wanandoa hao wanatakiwa wafenyeje warudipo nchini ili ndoa yao itambulike kisheria na labda pre nuptial agreement yao iweze kutambulika kisheria
 
Naomba mnifahanishe iwapo mke ndio kataka kukatiza ndoa YAKE namaanisha kuomba talaka bila Kuwa na ugomvi Kati YAKE na mumewe je hapo kunahitajika kigawana Mali? Na je mtoto ataenda kuishi na mama au Baba?
ili talaka itolewe, zinatakiwa ziwepo sababu zitakazothibitisha kuwa ndoa hiyo imevunjika pasipo kuwepo na nafasi ya kusimama tena. na hii ni baada ya kupitia kwenye balaza la usuluhishi na kupatiwa cheti ambacho wasuluhishi wenyewe wamenyoosha mikono kuwa kati yenu hamuwezi kuishi pamoja milele kutokana na sababu zilizopo. katika sheria zipo sababu kadhaa zimeorodheshwa ambazo mmoja wenu anaweza kuzitumia....nitakuwekea link ya kupata sheria hizo hapa ukaifuate na uzisome. kuna kitabu cha sheria kimeandikwa kwa kiswahili, ukikisoma utaelewa na hutakuwa na maswali. hata hivyo kwa harakaharaka unavyoeleza naona kama hapo kati yenu hakuna sababu yeyote itakayofanya mpate talaka....labda kama umemung'unya maneno. kwa ufafanuzi zaidi bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI
 
Hiyo talaka unataka kwa sababu gani..
1;Je mwenzi wako ana gonjwa la zinaa?
2; Je mwenzi wako amepata ugonjwa wa kichaa?
3;Je mwenzi wako hawezi kabisa kufanya tendo la ndoa?
4;Je mwenzi wako amepata ana maradhi ya kifafa ambayo hayatibiki na imekuwa kero?
5; Je mwenzi wako umegundua kuwa ni mwenzi wa mtu mwingine tena kwa ndoa?
 
Hakuna ukweli wowote hapo Mkuu Daata. Kifungu cha 160 cha Sheria husika kinatoa Dhanio la Ndoa.Hili huwepo pale ambapo mwanamke na mwanaume huishi kama mke na mume kwa miaka miwili au zaidi.Wakati wa kuishi kwao na kupata heshima ya jamii kama mke na mume wanaweza kuchuma mali mbalimbali.Sasa katika kuhitilafiana kwao,mwanamke hataondoka mikono mitupu. Hiyo ni dhana tu ya Dhanio la Ndoa na hutumika hivyo na si vinginevyo

Umesahau na kuwa lazima wawili hao wawe wametimiza umri stahiki yaani miaka 18.
Na pia wasiwe wanandoa wa ndoa nyingine....na wawe wameishi pamoja consecutively sio mara huyu yuko kwao miezi minne halafu anarudi.
 
Asante Mkuu alteza kwa swali lako. Umri wa wa kiume ni miaka 18 na wa kike ni miaka 15.Lakini,Mahakama yaweza kuwaruhusu wanaotaka kuoana kuoana hata bila kuwa na umri huo endapo: kwanza,wote wamefikisha umri wa miaka 14,na pili kama Mahakama imekubaliana na mazingira yaliyopo na kuiona ndoa husika inayotakiwa kufungwa.

Kwanza samahani kwa kuchelewa kufuatilia munakasha huu....Pole kwa majukumu haya Wakili msomi.
Katika hili naomba tusaidiane kuliweka sawa....Umri wa ndoa ni miaka 18 kwa mke au mume.....ila mke anaweza kuolewa katika umri wa 15 kwa Ridhaa ya Baba..kama hayupo basi mama na kama hawapo wote basi mlezi.....Binti anaweza kuolewa katika umri 14 iwapo mahakama itaona inafaa...e.g akiwa mjamzito tayari.
Mvulana anaruhusiwa kuoa katika umri wa 16 iwapo mahakama itaona inafaa e.g akiwa amempa binti mwenye umri wa ndoa (18+) ujauzito na anatambua majukumu ya ndoa.
 
Last edited by a moderator:
Awali nakupongeza kwa kuchukua jukumu la kutuelimisha sisi wenye ufahamu mdogo kuhusu mambo haya.

Swali langu linahusu mabaraza ya usuluhishi. Nafamu (sina uhakika kama ndivyo kisheria), mabaraza ya usuluhishi ni pamoja na Bakwata, Baraza la kata na mabaraza ya usuluhishi makanisani.

Mimi ni muumini wa dhehebu fulani na ndoa ilifungwa huko ninako abudu (mathalani msikitini/kanisani). Ninapotaka kuvunja ndoa, ili niweze kupata baraka za baraza la usuluhishi, natumia baraza lipi?
  1. Kama mume/mke wote ni wakristu wanatumia baraza lipi (la kata, la kanisa)?
  2. Kama mume/mke wote ni waislamu wanatumia baraza lipi (la kata, bakwata)?
  3. Kama mume/mke wote ni dini mchanganyiko wanatumia baraza lipi?

NB: Kwa ndoa za kikiristu, ni vigumu sana baraza la kanisa kutoa kibali ya kuwa ndoa hairekebishiki tena. Mbadala wake ni upi?

Asante, kazi njema
 
Hello! Je inawezekana mahakama kuvunja ndoa pale inapotokea mmoja wa wanandoa amepoteza mapenzi kwa mwenzake kwa kiwango ambacho yeye hawezi kuvumilia na hakuna mtu au taasisi inayoweza kubadili mtazamo wake wa kimapenzi kwa mwenzie? Otherwise nipe sababu za msingi za kisheria zinazoweza sababisha ndoa kuvunjika, in details please.
 
Mkuu Baba Kisura, naomba nikupe 'homework' kidogo. Swali lako lilishajibiwa humu. Tafadhali pitia majibu husika humu.Ikishindikana,nitakujibu tena Mkuu.Naomba nitumie rasilimali hii ya muda kujibu maswali mpya.Kumradhi!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza samahani kwa kuchelewa kufuatilia munakasha huu....Pole kwa majukumu haya Wakili msomi.
Katika hili naomba tusaidiane kuliweka sawa....Umri wa ndoa ni miaka 18 kwa mke au mume.....ila mke anaweza kuolewa katika umri wa 15 kwa Ridhaa ya Baba..kama hayupo basi mama na kama hawapo wote basi mlezi.....Binti anaweza kuolewa katika umri 14 iwapo mahakama itaona inafaa...e.g akiwa mjamzito tayari.
Mvulana anaruhusiwa kuoa katika umri wa 16 iwapo mahakama itaona inafaa e.g akiwa amempa binti mwenye umri wa ndoa (18+) ujauzito na anatambua majukumu ya ndoa.

Mkuu Benaire,hivyo ulivyoandika ndivyo Sheria ilivyo. Na kwakuwa ni Sheria,ndiyo kinachoruhusiwa hapa nchini kwasasa. Naweza kuikosoa Sheria niwezavyo lakini siwezi kuibadili.Nawe pia.
 
Mkuu petro naomba kuuliza, kwa mfano mtu kafunga ndoa nje ya nchi na ndoa yenyewe ilikuwa kwenye moja ya makubaliano ya pre nuptials, je wanandoa hao wanatakiwa wafenyeje warudipo nchini ili ndoa yao itambulike kisheria na labda pre nuptial agreement yao iweze kutambulika kisheria

Mkuu mjasiriamalidzamani,ndoa zinazofungwa nje ya Tanzania zinatambuliwa na Sheria ya Ndoa ya Tanzania,1971. Ni chini ya kifungu cha 36 cha Sheria tajwa. Kikubwa ni kuwa ndoa husika iwe imezingatia masharti ya sheria ya ndoa ya nchi husika.Pia,kama wanandoa wote ni watanzania, lazima wanandoa wawe na sifa za kufunga ndoa ambazo zinatanabaishwa na Sheria yetu ya ndoa niliyoitaja hapo mwanzo.

Hivyobasi,ndoa tajwa itatambulika na itachukuliwa halali pamoja na mambo yake yote ikiwa ni pamoja na makubaliano ya mgawanyo wa mali uliouulizia hapo kwenye swali lako. Asante Mkuu
 
Awali nakupongeza kwa kuchukua jukumu la kutuelimisha sisi wenye ufahamu mdogo kuhusu mambo haya.

Swali langu linahusu mabaraza ya usuluhishi. Nafamu (sina uhakika kama ndivyo kisheria), mabaraza ya usuluhishi ni pamoja na Bakwata, Baraza la kata na mabaraza ya usuluhishi makanisani.

Mimi ni muumini wa dhehebu fulani na ndoa ilifungwa huko ninako abudu (mathalani msikitini/kanisani). Ninapotaka kuvunja ndoa, ili niweze kupata baraka za baraza la usuluhishi, natumia baraza lipi?
  1. Kama mume/mke wote ni wakristu wanatumia baraza lipi (la kata, la kanisa)?
  2. Kama mume/mke wote ni waislamu wanatumia baraza lipi (la kata, bakwata)?
  3. Kama mume/mke wote ni dini mchanganyiko wanatumia baraza lipi?

NB: Kwa ndoa za kikiristu, ni vigumu sana baraza la kanisa kutoa kibali ya kuwa ndoa hairekebishiki tena. Mbadala wake ni upi?

Asante, kazi njema

Mkuu Sharp Observer, usuluhishi hufanyika katika Baraza lenye uhusiano wa moja kwa moja na ndoa husika. Kwa mfano, kwa waislamu Mbaraza ya BAKWATA yanapaswa kutumika.Kwa wakatoliki,Mabaraza ya wakatoliki,Walutheri ya kilutheri na kadhalika. Ya Kata, kadiri nijuavyo, yapo kwa ajili ya kimila na zile za kiserikali.
 
Last edited by a moderator:
Nauliza hivi, eti kumnyonya mkeo sehemu zake za tendo la ndoa kwa ulimi inaruhusiwa? Kama vijana wengi sikuhizi wanavtofanya?
 
vp ndugu mwanasgeria mtoto alizaliwa kabla ya ndoa je ana haki sawa na yule baada ya ndoa?, je n percent gan inatakiwa kutoka kwa mzaz kwa mtoto aliyezaliwa kabla ya ndoa
 
je unaeza fafanua kidogo kuhusu mgawanyo wa mali mlizochuma pamoja?,mathalani baba ni mfanyakazi/biashara na mama ni mama wa nyumbani?.Vigezo gani hutumika katika mgawanyo wa mali(kama wanandoa hao pia walibalikiwa watoto)?
 
Back
Top Bottom