Awali nakupongeza kwa kuchukua jukumu la kutuelimisha sisi wenye ufahamu mdogo kuhusu mambo haya.
Swali langu linahusu mabaraza ya usuluhishi. Nafamu (sina uhakika kama ndivyo kisheria), mabaraza ya usuluhishi ni pamoja na Bakwata, Baraza la kata na mabaraza ya usuluhishi makanisani.
Mimi ni muumini wa dhehebu fulani na ndoa ilifungwa huko ninako abudu (mathalani msikitini/kanisani). Ninapotaka kuvunja ndoa, ili niweze kupata baraka za baraza la usuluhishi, natumia baraza lipi?
- Kama mume/mke wote ni wakristu wanatumia baraza lipi (la kata, la kanisa)?
- Kama mume/mke wote ni waislamu wanatumia baraza lipi (la kata, bakwata)?
- Kama mume/mke wote ni dini mchanganyiko wanatumia baraza lipi?
NB: Kwa ndoa za kikiristu, ni vigumu sana baraza la kanisa kutoa kibali ya kuwa ndoa hairekebishiki tena. Mbadala wake ni upi?
Asante, kazi njema