Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Ndoa ni baraka, na watoto ni zawadi kutoka kwa MUNGU,

kutengana au kuachana si jambo zuri, huenda umefanya suluhu ikawa ngumu kwako, nakusihi usichoke, uko ktk vita dhidi ya shetani, anataka kuiangamiza baraka yako(ndoa) lakini pia anataka umwage zawadi(watoto) uliopewa na Mungu, kisha aokote awe wake.

Ila kuna wakati yote hayo kibinadamu huisha, uvumilivu wa roho na moyo wa nyama unashindwa kuhimili maumivu unayopata. Hakuna namna inalazimu tu kuharibu.

Unaweza anza mahakamani, huku ukitambua kuwa mahakama inaweza kubatilisha au kuvunja ndoa kwa sababu za msingi tu kama vile.
UZINZI, mmoja kutokuwa na uwezo wa kumpa "haki kuu" ya ndoa mwenzi wake, mmoja kuthibitika kuwa na ugonjwa wa zinaa, mmoja kuugua kichaa, mmoja wenu akapata kifungo gerezani. Nyingne ni minor sana huenda usifikiriwe.

Pole sana kwa mapito na maumivu uliyonayo. Hiyo ni sehemu ya pili ya ndoa, sehemu ya kwanza ni pale mlipofurahi.
 
Nilitaka mti anayefaham sheria anieleze nini mama anatakiwa kudai kisheria na NN sio haki Yale. Ni hayo tu wana jf
 
Nenda baraza la usuluhishi la kata ukiwa na sababu zako za msingi! Baada ya hapo utaenda mahakama ya mwanzo uta file petition for divorce ukiwa na ushahidi wa kwamba ndoa yenu haisuluhishiki kutoka baraza la usuluhishi!
 
Safi GreenCity hiyo unayonipa ni procédure ya kuacha kisheria .Nashukuru kwa hilo ila mm shida yangu kubwa ni mgawanyo wa haki za msingi. Il kuokoa muda na usumbufu, na zaidi kutoa haki.
 
Wakati unaoa ulipata ushauri huku? Nani anataka laana zenu sasa? Alichounganisha Mungu, mwanadamu asitenganishe.
 
Habari wana forum naombeni mnisaidie kisheria ukitaka kumwacha Mke inakubidi umfanyie NN na NN au ni utaratibu upi unatumika kisheria na sio ki dini Aksanteni
Chukua demu mtaa wa pili
 
Kifupi ni kuwa ndoa kwa tz zinaongozwa na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kadhaa. Sheria ya ndoa inataka watu waape kuishi pamoja mpaka kifo kiwatenganishe, lakini hiyo haizuii watu kufuata utaratibu wa sheria kutalikiana. Kwa masuala ya talaka unaweza kufungua kesi katika mahakama yoyote kati ya hizi; mahakama ya mwanzo, ya wilaya, ya hakimu mkazi au hata mahakama kuu. Sharti la kuomba talaka ni lazima ndoa iwe na zaidi ya miaka miwili. Kabla ya kwenda mahakamani lazima uwe na nyaraka ya uthibitisho kutoka serikali ya mtaa au ustawi wa jamii au kanisani/ msikitini/bakwata kuwa mgogoro ni mkubwa na usuluhishi umeshindikana. Mahakama itapokea shauri na kusikiliza pande zote mbili na kama ikiridhika kuwa upendo haupo tena basi itaivunja hiyo ndoa na kuamuru mgawanyo wa mali zilizopatikana wakati wa ndoa kwa uwiano wa mchango wa kila mmmoja. Elewa kuwa kwa tz mgawo wa mali sio nusu kwa nusu. Hata hivyo mahakama ya rufaa kwenye kesi maarufu sana ktk tasnia ya sheria ya Bi. Hawa Mohamed ilisema hata mama wa nyumbani zile kazi zake za nyumbani ni mchango tosha kusitahili mgao wa mali za mme wake, ila ni kiwango gani hiyo itategemea mazingira ya kila kesi.

Upande wa kiroho; Haivutii wanandoa kutalikiana.
 
Nenda kwa wazee kwanza ukapate ushauri nasaha ndiyo urudi humu baada ya miezi 6 ili tukushauri vizuri
Wazee ndio waliowakutanisha. Kumbuka hayo ni makubaliano ya watu wawili tu, hata mchungaji, padri, shekhe hausiki. Maamuzi unayo wewe mwenyewe mkubwa. Wazee wa nini, ni uoga huo. Kwani wao ndio wanaoteseka au muoaji. Mvaa kiatu.......
 
Mtu kauliza jambo jingine watu wanaleta mambo mengineee...
 
Huyu kaomba ushauri wa kuacha kwa sheria sasa nyinyi wengine story ndefu za nini?
 
Kama ni MUNGU wa kweli ndiye aliyewaunganisha, nakushauri umshukuru MUNGU huyo na kumtukuza. Kwani, MUNGU ni MWEMA na tendo la kukuunganisha na kuwa na Mke mwema ni UPENDO MKUU.

Kama wewe ni wa upande mwingine, yaani wa giza, basi pole sana. Huko kwa wenye kutawaliwa na dhambi pia tamaaa za mwili isiyo kuwa na kibali toka kwa BWANA MUNGU tunda lake ni mauti " mshahara wa dhambi ni mauti"
Mungu hahusiki mkuu,hats Mimi kuna jitu Niko nalo him silihitaji tena.
 
Safi GreenCity hiyo unayonipa ni procédure ya kuacha kisheria .Nashukuru kwa hilo ila mm shida yangu kubwa ni mgawanyo wa haki za msingi. Il kuokoa muda na usumbufu, na zaidi kutoa haki.
Usikubali kumalizana kienyeji,atachukua Mali halafu atakugeuka refer,zamoyoni mogela na mkewe nenda tu mahakamani
 
kwa kifupi sheria ya ndoa haizuii watu walioko kwenye ndoa kuachana isipokuwa kuwe kuna sababu za MSINGI zinazosababisha muachane na kwamba mahakama ijiridhishe kwamba kuishi katika ndoa hiyo haivumiliki.
hatua za kufuata.
1 anzia baraza la ndoa kama kuna mgogoro wowote kwajili ya usuluhishi. mabaraza ya ndoa yapo kila kata na kwenye makanisa pia hivyo hayo hutoa huduma ya usuluhishi. ikishindikana kusuluhishwa lazima baraza la ndoa litoe hati au certificate ya kuthibitisha kuwa limeshindwa kuusuluhisha mgogoro husika.
2 baada ya kupata hati hiyo ya baraza la ndoa utakwenda mahakamani kufungua shauri la ndoa kuiomba mahakama itoe ridhaa ya kuvunja ndoa hiyo. mahakama ikiridhia yatafuata masuala mengine yanayohusiana na ndoa kama 1 sehemu ya kuishi watoto 2 mali za wanandoa na mgawanyo wake.
lakini yote hayo ni lazima suala la msingi limalizike kwanza yaani divorce.
USHAURI. mimi kama mwanasheria sikushauri sana kuvunja ndoa yako kwa sababu madhara ya kuvunja ndoa ni makubwa sana kuliko madhara ya kuivumilia labda iwe imefikia kiwango cha kuwa MATESO na siyo ndoa tena

MBADALA. badala ya kufungua shauri la kuvunja ndoa ni bora ukafungua shauri la kutenganishwa kwa muda, hili hutolewa mahakamani kuwatenganisha wanandoa kwa muda fulani wakitazamia kurudisha mapenzi yao tena,kwa mfano kwa muda wa miaka mitatu au mitano.
hapa mume atalazimika kutoa huduma zote kwa mke na watoto isipokuwa kumtumia wakati wa usiku tu.
utapaswa kutoa.
1 matunzo kwa watoto na mama
2 kumtembelea mwenzi wako pamoja na watoto
3 kuwa katika ndoa na kuiheshimu ndoa husika
4 kuishi mbali na mkeo au mmeo
5 hautaruhusiwa kumtumia mkeo wakati wa judicial separation.
masharti mengine yatatolewa na mahakama kutegemea na sababu zilizowatenganisha.
separation ikishindwa kuwarudisha katika msitari mnaweza kufungua shauri mahakamani kudai talaka.
kwa maswali zaidi karibu.
 
Mr chapa nalo jr umenigusa kwe'ye mgawanyo mfano kuna ishu kama hii
Mtu kaishi na Mike kwa mda mrefu kapata watoto wengi tu bahati mbaya mama kafariki.
Baba kaoa Mike mwingine kaishi naye kwa mda kama miaka 5iv sa sa ndo wanaachana mgawanyo wa mali unakuaje hapo na kama mama uyu wa piliers hajabahatika kupata moto asanten.
 
Naona hutaki tukuPM,nina swali la haraka kidogo hivi Baraza la Usuluhishi wa NDOA LA KAMISHNA WA USTAWI WA JAMII NI HALALI! AU kazi inayofanywa na Ofisi za ustawi wa jamii kuhusu usuluhishi wa ndoa ni halali?
Mkuu,sasa ni takribani miaka miwili uulize,nijibu?
 
Kwa mfano mme anaoa mke mwingine kisiri,ilhali alifunga ndoa ya mke mmoja.Mke wa kwanza akigundua anaweza kwenda mahakamani kumshitaki mme ili amlipe fidia? i mean ma milioni ya pesa
Hapana. Ndoa hapo ni moja tu. Ile ile ya kwanza
 
Ndoa ya kiserikali taraka lazima itolewe mahakamani?
 
Samahani mkuu; dada yangu yupo kwenye ndoa, mwaka wa tatu sasa na hawajabahatika kupata mtoto.. Tatizo lililopo ni kwamba dada Hana tena mapenzi na mumewe, je hiyo nayo inaweza kuwa sababu ya kuombea talaka? Ndoa ni ya kiislam
 
Back
Top Bottom