Shida ya ukosefu wa ajira sio mfumo wa elimu tu, watanzania wengi hawaajiriki, ni wavivu na wezi

tehama

Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
72
Reaction score
107
Majaliwa ametaja njia moja wapo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira ni kwenda Veta, yawezekana ila shida kubwa iko kwenye sisi wananchi wenyewe.

Visa vingi sana vimeletwa humu ndani kuhusu namna waajiriwa walivyo rudishwa nyuma kwa wizi. MImi binafsi nina mifano mingi sana.

Lakini pia walioajiriwa, hawafanyi kazi kwe weledi,

1. Kila siku ni kuomba ruksa mara anaumwa, mara shangazi kafiwa n.k.
2. Wengi hawafanyi kazi kwa maono na kuangalia namna ya kuboresha kazi zao, wapo tu
3. Kuchelewa mno kufika kazini au kutokuwepo eneo la kazi
4. Uchawa na majungu kazini (Wakiona unasonga mbele na kufanya kazi kwa weledi, wanakupiga vita)

Watanzania wengi wanataka kazi kidogo, pesa nyingi kitu ambacho hakiwezekani

Lazima tubadilike ili kukabiliana na janga la ajira nchini

Post zinazoendana

Serikali iingilie kati watanzania wafanyakazi wanaofilisi makampuni sekta binafsi

Simbachawene alikiri 40% ya Watumishi wa Umma ni Wazembe, Wavivu, incompetents, kwanini Serikali iendelee kuwabeba?

Mrejesho : Mawazo kadhaa kutoka kwa wadau

1. Sheria kali kuhusu watumishi wa umma. Unapofanya kosa, unatakiwa kufukuzwa na kufunguliwa mashtaka na sio kuhamishwa kituo cha kazi kama ilivyo sasa

2. Kuboresha mfumo wa elimu. Uwe katika critical & first principle thinking ya namna mtu anaweza kujisimamia pamoja na kutatua matatizo yanayomzunguka

3. Malezi bora kutoka kwa wazazi na jamii
 
Kuna branch moja ya TRA nimeenda juzi ilikua saa 6 mchana yule staff ananiambia kua nimechoka na KAZI. Kisha akasema bro naomba usiondoke hapa kwenye meza yangu akaingia mteja mpya. Na mm nikamwambia km ndio ivyo na mm naomba makadilio yasipande mwaka huu ibakize ile ile ya mwaka jana. UWEZI AMINI KAKUBALI.Nq mm nikabakia kanq kwamba jambo langu bado hajatatua mpk baaaaadae akasema bro asante unaweza kwenda.
Nakubalina n ww kuhusu watanganyika na UVIVU sehemu ya KAZI. Staff saa 6 mchana anasema amechoka kazi nimeshangaa MNO.
KAZI NI KIPIMO CHA UTU
 
Sababu ya uvivu zinaweza kuwa:
1. Kamshahara kadogo, ambako pengine nako kanakuja na masimango kibao. Uvuvi hapo lazima.

2. Kusomea nyanja isiyoendana na mtu mwenyewe. Naweza kuwa mtaalamu wa financial services ama daktari au mhandisi kwa vile tu mzazi alitaka nisomee kitu hicho - lakini hakiko damuni. Uvivu lazima.

3. Mazingira ya kazi yasiyo rafiki.

4. Mazoea ya kutojisimamia mwenyewe. Kwa wengi, hii hutokana na spoon-feeding na kukariri mambo tangu wakiwa shule. Hawa bila kusukumwa, hawaendi.

5. Kutotambulika. Wengine wanakuwa wavivu kwa sababu hawaoni kama mchango wao wa kitaaluma unathaminiwa. Kuna msemo: ^Politicians have mastered the art of arriving late only to claim all the credit.^

6. Kufanya kazi kwa mazoea. Hakuna ubunifu. Hakuna ushindani. Hakuna changamoto mpya za kushughulikia. Hakuna mipango ya muda mfupi wala mrefu. Mambo ya jana ndiyo yaleyale ya leo na kesho. Hapo lazima akili isinzie na kazi iwe ngumu. Uvuvi hutokea hatimaye.

7. Mshahara mnono usiowiana na kazi yenyewe. Hii pia inasababisha uvuvi. Plus marupurupu kibao.

8. Ajira za kujuana zisizozingatia vigezo, weledi na taaluma.
 
Kuna branch moja ya TRA nimeenda juzi ilikua saa 6 mchana yule staff ananiambia kua nimechoka na KAZI. Kisha akasema bro naomba usiondoke hapa kwenye meza yangu akaingia mteja mpya. Na mm nikamwambia km ndio ivyo na mm naomba makadilio yasipande mwaka huu ibakize ile ile ya mwaka jana. UWEZI AMINI KAKUBALI.Nq mm nikabakia kanq kwamba jambo langu bado hajatatua mpk baaaaadae akasema bro asante unaweza kwenda.
Nakubalina n ww kuhusu watanganyika na UVIVU sehemu ya KAZI. Staff saa 6 mchana anasema amechoka kazi nimeshangaa MNO.
KAZI NI KIPIMO CHA UTU
Mkuu, jamaa akiusoma huu ujumbe wako, umekwisha.
 
kama ni mwanaume alilala kwenye mashindano na alikozaliwa
 
Majaliwa ametaja njia moja wapo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira ni kwenda Veta, yawezekana ila shida kubwa iko kwenye sisi wananchi wenyewe.

Visa vingi sana vimeletwa humu ndani kuhusu namna waajiriwa walivyo warudisha nyuma kwa wizi. MImi binafsi nina mifano mingi sana.

Lakini pia walioajiriwa, hawafanyi kazi kwe weledi,

1. Kila siku ni kuomba ruksa mara anaumwa, mara shangari kafiwa n.k.
2. Wengi hawafanyi kazi kwa maono na kuangalia namna ya kuboresha kazi zao, wapo tu

Watanzania wengi wanataka kazi kidogo, pesa nyingi kitu ambacho hakiwezekani

Lazima tubadilike ili kukabiliana na janga la ajira nchini
Kila mkoa ingekuwa na viwanda kama vilivyokuwepo wakati wa Nyerere ungeandika ulichoandika?
 
Kwamba hao wavivu na wasio waaminifu wachache wakibadilika tutakuwa na ajira za kutosha?? Kwamba hatuhitaji maboresho ya mitaala yetu ya elimu??? Bwanyenye tunaheshimu mawazo yako japo yana najisi.
 
Mkuu, jamaa akiusoma huu ujumbe wako, umekwisha.
Hahahah!! Atakua amekwisha YY bro!! Mm mkongwe wa MUJI. Siendagi kinyonge sehemu muhimu.full ushahidi upo sehemu salama.kama ni ww kinukishe au umetumwa kinukisheni.Mm kufunga ofisi sioni hatari KABISA ila na YY anaondoka ofisi ya uma!!Na huu ndio ukweli watanganyika ni wavivu.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Wengi hatuna commitment tupo ili mradi tulizaliwa tukue, mshahara upo, nijibu vibaya mteja , ama huduma mbovu n basi hatujali sana. Na mifumo yetu unaajiriwa unaenda unakuta mazingira ya kazi yalivyo na wewe unaendana nayo.
 
Kila mkoa ingekuwa na viwanda kama vilivyokuwepo wakati wa Nyerere ungeandika ulichoandika?
Jiulize kwa nini vilikufa. Na kwa namna wengi wetu wanafanya kazi, hatuwezi fika huko
 
Kuna branch moja ya TRA nimeenda juzi ilikua saa 6 mchana yule staff ananiambia kua nimechoka na KAZI. Kisha akasema bro naomba usiondoke hapa kwenye meza yangu akaingia mteja mpya. Na mm nikamwambia km ndio ivyo na mm naomba makadilio yasipande mwaka huu ibakize ile ile ya mwaka jana. UWEZI AMINI KAKUBALI.Nq mm nikabakia kanq kwamba jambo langu bado hajatatua mpk baaaaadae akasema bro asante unaweza kwenda.
Nakubalina n ww kuhusu watanganyika na UVIVU sehemu ya KAZI. Staff saa 6 mchana anasema amechoka kazi nimeshangaa MNO.
KAZI NI KIPIMO CHA UTU
Inahuzunisha sana. Afu unakuta watu wanalalamika wageni wanajazana nchini. Waje tu kwa sababu hakuna wazawa makini wa kufanya nao kazi
 
Majaliwa ametaja njia moja wapo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira ni kwenda Veta, yawezekana ila shida kubwa iko kwenye sisi wananchi wenyewe.

Visa vingi sana vimeletwa humu ndani kuhusu namna waajiriwa walivyo warudisha nyuma kwa wizi. MImi binafsi nina mifano mingi sana.

Lakini pia walioajiriwa, hawafanyi kazi kwe weledi,

1. Kila siku ni kuomba ruksa mara anaumwa, mara shangari kafiwa n.k.
2. Wengi hawafanyi kazi kwa maono na kuangalia namna ya kuboresha kazi zao, wapo tu

Watanzania wengi wanataka kazi kidogo, pesa nyingi kitu ambacho hakiwezekani

Lazima tubadilike ili kukabiliana na janga la ajira nchini
Utatukanwa japo umeongea ukwel mtupu ,nkiwepo mm ila nitabadilika sana
 
Kwamba hao wavivu na wasio waaminifu wachache wakibadilika tutakuwa na ajira za kutosha?? Kwamba hatuhitaji maboresho ya mitaala yetu ya elimu??? Bwanyenye tunaheshimu mawazo yako japo yana najisi.
1. Wavivu na wasio waaminifu ni wengi mkuu kuliko wachapakazi na waaminifu.

2. NImesema shida sio mfuo wa elimu pekee, mfumo wa elimu unachangia kiasi fulani
 
Back
Top Bottom