Shida ya ukosefu wa ajira sio mfumo wa elimu tu, watanzania wengi hawaajiriki, ni wavivu na wezi

Shida ya ukosefu wa ajira sio mfumo wa elimu tu, watanzania wengi hawaajiriki, ni wavivu na wezi

Mkuu, point yangu ni kwamba mshahara hauwezi tosha, mahitaji yanakua kadri pesaanyway lila.mtu atakuls ana inavyo ongezeka

Kuna watu wanapata 500k au chini ya hapo kama take home lakini wanaweza kuendesha maisha yao.

Wakati naanza mapambano, nilianza kwa kuajiriwa, nilikua nalipwa mshahara mdogo sana lakini nilipambana na kufanya kazi kwa uaminifu na bidii kubwa sana. Nilitafuta kazi za kando na bado nilihakikisha nafanya kwa weledi wa hali ya juu

Wote waliokua wanaendekeza uvivu na wizi, bado wapo wanaganga njaa hadi sasa na kulalamika kila siku
Anyaway Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake
 
Na ulifanya vyema kumsikiliza mkuu, la sivyo ungedumaa kiakili na kubaki kulalamika. Ukikutana na vijana, jaribu kuwaelewesha, labda baadhi watakuelewa na tutasonga mbele
Kabisa kuna mmoja kaajiriwa kama muhasibu kule(since niliacha alama isiyofutika) amekutana na habari zangu akanitafuta nimempa mwanga mzuri sana.
 
Kazi yangu ya kwanza nilikuta wamama wana magodoro kabisa ofisini, baada ya chai analala zake anasubiri muda wa kutoka v8 ipo nje anaenda zake nyumbani. Nilishangaa sana. Nachoshukuru Boss wangu aliziona jitihada zangu na kunitia moyo.
Mhh ya kweli haya? Huku kwetu kwenye diplomatic mission na international organisation tunapiga kazi kwelikweli. Kuna kautamaduni ka uvivu hasahasa serikalini. Watu hawajali kazi zao ,ni mpaka wasukumwe. Mimi saa moja kasoro niko ofisini na kazini kwetu hupangiwi kazi na mtu, unajipangia mwenyewe ilimradi uwe na deliverables na ku meet deadlines. Ukisubiri upangiwe utasubiri sana maana hakuna mwenye muda huo.
 
Majaliwa ametaja njia moja wapo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira ni kwenda Veta, yawezekana ila shida kubwa iko kwenye sisi wananchi wenyewe.

Visa vingi sana vimeletwa humu ndani kuhusu namna waajiriwa walivyo warudisha nyuma kwa wizi. MImi binafsi nina mifano mingi sana.

Lakini pia walioajiriwa, hawafanyi kazi kwe weledi,

1. Kila siku ni kuomba ruksa mara anaumwa, mara shangazi kafiwa n.k.
2. Wengi hawafanyi kazi kwa maono na kuangalia namna ya kuboresha kazi zao, wapo tu

Watanzania wengi wanataka kazi kidogo, pesa nyingi kitu ambacho hakiwezekani

Lazima tubadilike ili kukabiliana na janga la ajira nchini
Acha jumwagia povu la sabuni ya magadi hapa..
Mnataka watu wafanye kazi za kinyonyaji yaani degree analipwa 300k na bado mnataka afanye kazi kama mbwa ***** acheni muuibiwe hadi maji muite mma..
 
Sababu kuu, almost 90% ya watu wanafanya kazi wasizozipenda..wapo hapo ili wapate chochote.
Ukiwa unafanya kazi unayoipenda raha sana na ni kama ibada..unaweza kukesha nayo ukienjoy.
 
Sababu kuu, almost 90% ya watu wanafanya kazi wasizozipenda..wapo hapo ili wapate chochote.
Ukiwa unafanya kazi unayoipenda raha sana na ni kama ibada..unaweza kukesha nayo ukienjoy.
Yawezekana mkuu ila kumbuka dunia haina usawa, tunatakiwa tuishi nayo kama tulivyo ikuta na sio namna tunapenda.

Ni wajibu wa mtu kupenda anachofanya hadi pale atakapoweza kufanya anachopenda

NI wachache sana dunia hii wamefanikiwa kufanya wanachokipenda
 
Tatizo lingine kubwa sana fanya kazi kwa kujituma na uaminifu uone majina utakayo kutana nayo, sisi waafrika bado hatujui nini tunahitaji.
 
Sababu ya uvivu zinaweza kuwa:
1. Kamshahara kadogo, ambako pengine nako kanakuja na masimango kibao. Uvuvi hapo lazima.

2. Kusomea nyanja isiyoendana na mtu mwenyewe. Naweza kuwa mtaalamu wa financial services ama daktari au mhandisi kwa vile tu mzazi alitaka nisomee kitu hicho - lakini hakiko damuni. Uvivu lazima.

3. Mazingira ya kazi yasiyo rafiki.

4. Mazoea ya kutojisimamia mwenyewe. Kwa wengi, hii hutokana na spoon-feeding na kukariri mambo tangu wakiwa shule. Hawa bila kusukumwa, hawaendi.

5. Kutotambulika. Wengine wanakuwa wavivu kwa sababu hawaoni kama mchango wao wa kitaaluma unathaminiwa. Kuna msemo: ^Politicians have mastered the art of arriving late only to claim all the credit.^

6. Kufanya kazi kwa mazoea. Hakuna ubunifu. Hakuna ushindani. Hakuna changamoto mpya za kushughulikia. Hakuna mipango ya muda mfupi wala mrefu. Mambo ya jana ndiyo yaleyale ya leo na kesho. Hapo lazima akili isinzie na kazi iwe ngumu. Uvuvi hutokea hatimaye.

7. Mshahara mnono usiowiana na kazi yenyewe. Hii pia inasababisha uvuvi. Plus marupurupu kibao.

8. Ajira za kujuana zisizozingatia vigezo, weledi na taaluma.
No 6 100% yani ubunifu ni kama dhambi watu wanafanya kazi kwa mazoea na hawataki ubunifu,no 1 nayo 100%mshahara baada ya kukupa furaha unakupa stress,mishahara ni midogo mno yani ikifika tarehe 10,idara nzima wanalia ukata
 
1. Wengi hawaajiriki ndo maana baadhi ya shule za private zinaajiri walimu kutoka nchi za jirani

2. Kusuhu data, sijafanya utafiti rasmi lakini nina experience yangu mwenyewe, mifano ya kutosha kutoka kwa watu walionizinguka na kupitia mada kadhaa za huku jamii forum
Fanya utafiti kidogo kabla ya kuandika hapa.
 
Fanya utafiti kidogo kabla ya kuandika hapa.
Usijifiche kwenye kivuli cha utafiti rasmi mkuu. Tumia akili yako kidogo kwenye mazingira yanayokuzunguka.

Usikariri kila kitu kinahitaji utafiti rasmi. Shida ipo na lazima tupambane kuitatua
 
Kuna branch moja ya TRA nimeenda juzi ilikua saa 6 mchana yule staff ananiambia kua nimechoka na KAZI. Kisha akasema bro naomba usiondoke hapa kwenye meza yangu akaingia mteja mpya. Na mm nikamwambia km ndio ivyo na mm naomba makadilio yasipande mwaka huu ibakize ile ile ya mwaka jana. UWEZI AMINI KAKUBALI.Nq mm nikabakia kanq kwamba jambo langu bado hajatatua mpk baaaaadae akasema bro asante unaweza kwenda.
Nakubalina n ww kuhusu watanganyika na UVIVU sehemu ya KAZI. Staff saa 6 mchana anasema amechoka kazi nimeshangaa MNO.
KAZI NI KIPIMO CHA UTU
Ndo hivyo boss, Hapo kuna watu walikuwa wanahitaji huduma ila kupitia wewe na nia yako ya kulipa kodi ile ile ukawezesha wao kutohudumiwa kwa wakati.
 
Usijifiche kwenye kivuli cha utafiti rasmi mkuu. Tumia akili yako kidogo kwenye mazingira yanayokuzunguka.

Usikariri kila kitu kinahitaji utafiti rasmi. Shida ipo na lazima tupambane kuitatua
Matumizi ya akili hudhihiri zaidi pale unapojengwa kwa kuwa na uwezo wa kufanya utafiti, utafiti ni akili. Kusema shida ipo bila kubainisha ubayana (kufanya utafiti) "sio akili"
 
Majaliwa ametaja njia moja wapo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira ni kwenda Veta, yawezekana ila shida kubwa iko kwenye sisi wananchi wenyewe.

Visa vingi sana vimeletwa humu ndani kuhusu namna waajiriwa walivyo rudishwa nyuma kwa wizi. MImi binafsi nina mifano mingi sana.

Lakini pia walioajiriwa, hawafanyi kazi kwe weledi,

1. Kila siku ni kuomba ruksa mara anaumwa, mara shangazi kafiwa n.k.
2. Wengi hawafanyi kazi kwa maono na kuangalia namna ya kuboresha kazi zao, wapo tu
3. Kuchelewa mno kufika kazini au kutokuwepo eneo la kazi
4. Uchawa na majungu kazini (Wakiona unasonga mbele na kufanya kazi kwa weledi, wanakupiga vita)

Watanzania wengi wanataka kazi kidogo, pesa nyingi kitu ambacho hakiwezekani

Lazima tubadilike ili kukabiliana na janga la ajira nchini
Tupo watu milioni 60+, vijana, ni 60% watu 30 milioni hawawezi, kuwa, wezi wote,wizi, ni tabia, ipo duniani, kote,swala, la, wizi, uvivu, ni hulka ya binadamu, linatatuliwa, kwa, sheria, Kali, shida kwenye serikali, watu wanapewa, kazi, kwa, kujuana, sheria, hazifuatwi, kwenye makampuni ya simu, unapewa SOP, standard operation procedure, mwongozo wa kufanya kazi, sio, kila wakati kuuliza uliza, na, unajua kila kosa na, adhabu yake, watu wanapiga kazi, na unakua na home, u kufanya kosa, hakuna tume inaundwa,upo mtwara mtambaswala, superviser wako yupo mbeya, boss yupo Dar, unawekwa ktimoto kwenye conference call, unaadhibiwa, ikibidi kazi Keisha, inaisha,unatimuliwa, anachukua mwingine,
Sio, serikalini,mijitu inafsnya kosa, kwenye mizani, eti inaundwa tume kuchunguza! Fukuza hao, kenge,
Kwa, uzoefu wangu, nidhamu ya, wafanyakazi, inaletwa, na, sheria Kali, ziwepo, na, zionekane zinafatwa, sio, zinapindishwa, kisa,aliyefsnya kosa, ni dem wa boss,
 
Yes, sio wote ila asilimia kubwa wana hulka hizo kwa Tanzania.

Nakubaliana na wewe, inahitajika sheria kali katika watumishi wa umma katika kukabiliana na janga hili
 
Naafikiana na issue ya uvivu pahala pa kazi. Watumishi walio wengi wamejisahau kabisa..nadhani ingefaa kusiwepo na ajira ya kudumu. Mtumishi awe anapewa mkataba kila mwaka ili ikitokea output yake imekua ndogo anapumzishwq anakuja mwingine hii itasaidia kupunguza mazoea ya kazi na kujisikia
 
Yaani ukiwa na kazi inayo kupeleka kwenye maofisi mbalimbali kutaka huduma utashangaa sana
Watu wapo wapo tu...unaambiwa subiri hapo unaishia kukaa masaa 3 na hujajuliswa chochote
simu hawana/mbovu/hazipokelewi
Email hazijibiwi.... halafu utasikie wako Digital

Wasomi wanapewa ofisi lakini HAWATUMII AKILI ZAO kubadilisha Idara ziendane na wakati ...
Kazi kuwazia posho za mchongo na kutaka mshahara upande..wakati hakuna matokeo....
Unaweza kuona kabisa ofisi inayosimamiwa na mtu wa Diploma na mtu wa Masters...hakuna tofauti
 
Back
Top Bottom