Tunatambua taasisi ya urais ina kila taarifa muhimu juu ya suala zima la matumizi ya chanjo ya COVID-19. Pengine hii ndiyo ikawa sababu ya Rais wetu kutilia mashaka juu ya uharaka wa mchakato wa kuanza kuwachanja raia zake.
Mimi nafikiri kujenga mashaka juu ya uharaka huu si kitu kibaya, lkn kutoa kauli zenye kuonyesha msimamo wa serikali majukwaani mbele ya vyombo vya habari, ni jambo ambalo linapaswa kuepukwa. Kwa kuwa kama nchi tulikwisha ridhia masuala ya afya ya kimataifa, eneo hili linapaswa kufanyiwa kazi na kutolewa na wataalamu wetu wa afya na wala si wanasiasa.
Uzoefu unatuonyesha mwishoni na mwanzoni mwa miaka ya 1970s & 1980s, aliyekuwa Rais wetu Mwl Nyerere wakati huo alikwaruzana mara kwa mara na mashirika ya fedha ya kimataifa ya fedha na hata wataalamu wa ndani kutokana na misimamo na mawazo yake binafsi. Alipinga kila "expert opinions" zilizotolewa ili kusimamia mageuzi ya sera za fedha na kiuchumi hapa nchini Tanzania. Kilichotokea kila mtu anakitambua kupitia historia.
Tunatambua Rais ana taarifa, hisia, misimamo na hata uelewa wake binafsi juu ya suala zima la COVID-19 hapa nchini. Lakini anapaswa kulishugulikia kitaasisi zaidi kuliko ilivyokuwa sasa ambapo inaonekana yupo kibinafsi zaidi. Masuala nyeti ya afya aiache Wizara ya Afya ndiyo ibebe jukumu nyeti la kukabiliana na gonjwa hili nyeti.
Mbele ya jicho la kimataifa na mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeridhia, inakuwa ni kichekesho kukwepa kuwajibika eti kwa kisingizio cha sisi kama taifa tupo salama zaidi kuwa tunategemea maombi na kupiga nyungu. Hata kama tunaona ni muhimu mno hapa nchini tuliweke tu kama "peripheral tool"